Uchaguzi 2020 Hesabu zinambeba Membe awe mgombea pekee kwa tiketi ya Upinzani

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,310
12,607
Kwenye uchaguzi wa 2020 Ni vigumu kusema CCM itashindwa na chama cha upinzani, lakini Vyama vya upinzani vinaweza kupata viti vingi vya ubunge na udiwani kama watamwachia Mh. Membe awe mgombea pekee kwa niaba ya vyama vya upinzani kuliko wakimsimamisha mgombea mwingine akiwemo mh. Lissu.

Baba wa taifa alishawahi kusema kuwa mgombea atakayekuja kuiangusha CCM madarakani atatoka CCM.

Hesabu ni rahisi tu, wasioipenda CCM na wanaoipenda chadema wapo tayari kumchagua yeyote hata kama ni kiazi.

Mh. Membe kama akigombea ataungwa mkono pia na wana CCM wengi na mashuhuri ambao ni rafiki zake na wale ambao wanakerwa na jinsi CCM ilivyo na inavyoendeshwa kwenye awamu ya tano.

Hivyo basi Membe atapata kura za marafiki zake na wanaokerwa na mambo ndani ya awamu ya tano na atapata kura za wasioipenda CCM, wanaotaka mabadiliko na wanaoipenda chadema au ACT, au NCCR.

Shida pekee ya Membe ni ya kile kilichotokea kwa Lowassa na Sumaye kurudi tena CCM.

Kupanga ni kuchagua, maoni tyuu.
 
Yaani wewe bure kabisa. Unaonaje Membe amuunge mkono Lissu ili kura za wanachadema wote azipate, kura za wanaccm wasiopenda mambo yanayofanyika CCM azipate? Maana wanamageuzi wa kweli hawawezi kumchagua mgombea yoyote aliyetoka CCM.

Ukiumwa na nyoka hata ukiguswa na jani lazima uruke. Lowassa katuuma hatuko tayari kutake risk anymore, hivyo hata jani likitugusa lazima turuke.
 
Hizo hesabu ziko wapi ?
(CCM - Membe) < (Membe + CDM+ACT+ spana + wapenda mabadiliko)

Make Membe equals to Membe + Makamba + Kinana + January + Nape + relatives + wasiopandishwa mishahara + wafanyakazi hewa + wafanyabiashara + waliotumbuliwa + maisha magumu +others.
 
Yaani wewe bure kabisa. Unaonaje Membe amuunge mkono Lissu ili kura za wanachadema wote azipate, kura za wanaccm wasiopenda mambo yanayofanyika ccm azipate? Maana wanamageuzi wa kweli hawawezi kumchagua mgombea yoyote aliyetoka ccm. Ukiumwa na nyoka hata ukiguswa na jani lazima uruke. Lowassa katuuma hatuko tayari kutake risk anymore, hivyo hata jani likitugusa lazima turuke.
Shida ni kwamba Membe hawezi kuwashawisha wana CCM (wasioipenda CCM ya awamu ya tano) na rafiki zake wampende Lissu, kwao wao Membe is well known and secure than Lissu; fear of both known and unknown origin.
 
Membe hanalolote alilofanya akiwa serikalini kwa miaka yote aliyo kua uko hana lolote la kuwaeleza wananchi, Lisu kwa miaka yote akiwa mbunge yeye sikuzote amekua anaipinga serikali bila kutoa suluhisho la nini kifanyike.

Jambo kubwa nililoliona kwa Lisu ni kauliyake ya kuwapa Uhuru wapenzi wa jinsia mmoja wajisikie wapo salama ndani ya Tanzania.

Kwa ujumla awa wote hawataweza kuongeza chochote kwa upinzani.
 
Shida ni kwamba Membe hawezi kuwashawisha wana CCM (wasioipenda CCM ya awamu ya tano) na rafiki zake wampende Lissu, kwao wao Membe is well known and secure than Lissu; fear of both known and unknown origin.
Wana CCM gani wapo na Membe wewe kavulana?
 
Hata zikija propaganda gani Magu lazima apambane na Lissu! pole sana! hii story ni obsolete!
 
Hakuna cha Membe wa Lissu, hesabu zilishakamilika prezidaa ni JPM na wabunge kibao.
 
Membe hanalolote alilofanya akiwa serikalini kwa miaka yote aliyo kua uko hana lolote la kuwaeleza wananchi, Lisu kwa miaka yote akiwa mbunge yeye sikuzote amekua anaipinga serikali bila kutoa suluhisho la nini kifanyike. Jambo kubwa nililoliona kwa Lisu ni kauliyake ya kuwapa Uhuru wapenzi wa jinsia mmoja wajisikie wapo salama ndani ya Tanzania.
Kwa ujumla awa wote hawataweza kuongeza chochote kwa upinzani.
Lissu Asirogwe akaanza kukejeli ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli na barabara, vituo vya afya na ukarabati wa shule uliofanywa kwenye awamu hii atajikuta akipingwa na wananchi wengi. Ni kweli sasa hivi kero ya rushwa imepungua hata wananchi wanafahamu hili. Hivyo laZIMA ACHAGUE LA KUZUNGUMZA AKIWA JUKWAANI, ASIFOKEFOKE HAITAMSAIDIA.

AKITAKA MAMBO YAMNYOOKEE ANGALau KIDOGO AsIBEZE JUHUDI ZILIZOFANYWA NA CCM, BADALA YAKE ATOE NJIA MBADALA YA KUENDELEZA KILICHOANZISHWA NA CCM MAANA NI KODI ZETU. Hakuna mtu atamuelewa kama atasimama jukwaani na kusema kujenga reli ni makosa, kujenga bwawa la umeme ni makosa, kujenga hospitali ni makosa, kutokomeza ujangiri ni makosa, kununua ndege ni makosa, kukomesha safari nyingi mno za nje ni makosa, kutoa elimu bure ni makosa, kusambaza maji ni makosa, kununua meli mpya ni makosa, hataeleweka kaabisa kama atatumia muda mwingi kusema hivyo. Badala yake ajikite kwenye nini yeye atafanya kuyafanya hayo aliyofanya magufuli kwa haraka na namna bora zaidi.
 
Shida yako ipo hivi "hujui kuwa wananchi tumeichoka CCM"

Hayo maujenzi hata mkoloni alijenga miundo mbinu mizuri na imara kuliko hii inayojengwa na CCM via kodi zetu huku wakiiba kodi zetu

Tukutane October 28
Lissu Asirogwe akaanza kukejeli ununuzi wa ndege, ujenzi wa reli na barabara, vituo vya afya na ukarabati wa shule uliofanywa kwenye awamu hii atajikuta akipingwa na wananchi wengi. Ni kweli sasa hivi kero ya rushwa imepungua hata wananchi wanafahamu hili. Hivyo laZIMA ACHAGUE LA KUZUNGUMZA AKIWA JUKWAANI, ASIFOKEFOKE HAITAMSAIDIA.

AKITAKA MAMBO YAMNYOOKEE ANGALI KIDOGO AZIBEZE JUHUDI ZILIZOFANYWA NA CCM, BADALA YAKE ATOE NJIA MBADALA YA KUENDELEZA KILICHOANZISHWA NA CCM MAANA NI KODI ZETU. Hakuna mtu atamuelewa kama atasimama jukwaani na kusema kujenga reli ni makosa, kujenga bwawa la umeme ni makosa, kujenga hospitali ni makosa, kutokomeza ujangiri ni makosa, hataeleweka kaabisa
 
tatizo la kuandika huku unavuta mibange ndilo hilo! wewe unafahamu kuwa akili na uwezo wako wa kufikiri ni mdogo bado ile akili ndogo uliyo nayo unaiharibu kwa mibange!
 
Back
Top Bottom