Uchaguzi 2020 Hesabu zinambeba Membe awe mgombea pekee kwa tiketi ya Upinzani

(CCM - Membe) < (Membe + CDM+ACT+ spana + wapenda mabadiliko)
Hesabu yako kiusahihi iko hivi: (CCM - Membe) < (CDM+ACT+ spana + CCM wapenda maendeleo).
Tatizo langu ni huyo Membe. CCM watakapo muona kuwa Membe ndio tatizo lao, watamrudisha kwao ki Lowasalowasa, jambo ambalo nae atalifurahia sana.
 
JPM 5 tena

Wapinzani mkajipange upya

Tukutane Oktoba 28 2020
Mkuu usiwabeze sana wapinzani, hata CCM hakuko shwari. Hebu Ona wale waliounga juhudi kutoka upinzani walivyogaragazwa na wajumbe kwenye kura za maoni. Hii ni ishara tosha kuwa kule juu na huku chini ya chama hakuna mawasiliano yenye afya kwa chama.
 
Hesabu yako kiusahihi iko hivi: (CCM - Membe) < (CDM+ACT+ spana + CCM wapenda maendeleo).
Tatizo langu ni huyo Membe. CCM watakapo muona kuwa Membe ndio tatizo lao, watamrudisha kwao ki Lowasalowasa, jambo ambalo nae atalifurahia sana.
Ndiyo maana nikasema tatizo la Membe ni Lowassa na Sumaye. Membe anafanana na CCM zaidi kuliko ACT na upinzani. mtu kama huyu kurudi CCM hakuhitaji kupiga ramli
 
Kwenye uchaguzi wa 2020 Ni vigumu kusema CCM itachindwa na chama cha upinzani, lakini Vyama vya upinzani vinaweza kupata viti vingi vya ubunge na udiwani kama watamwachia Mh. Membe agombea pekee kwa niaba ya vyama vya upinzani kuliko wa wakimsimamisha mgombea mwingine akiwemo mh. Lisu.

Baba wa taifa alishawahi kusema kuwa mgombea atakayekuja kuiangusha CCM madarakani atatoka CCM.

Hesabu ni rahisi tu, wasioipenda CCM na wanaoipenda chadema wapo tayari kumchagua yeyote hata kama ni kiazi.

Mh. Membe kama akigombea ataungwa mkono pia na wana CCM wengi na mashuhuri ambao ni rafiki zake na wale ambao wanakerwa na CCM ilivyo na inavyoendeshwa kwenye awamu ya tano.

Hivyo basi Membe atapata kura za marafiki zake na wanaokerwa na mambo ndani ya awamu ya tano na atapata kura za wasioipenda CCM, wnaotaka mabadiliko na wanaoipenda chadema au ACT, au NCCR.

Shida pekee ya Membe ni ya kile kilichotokea kwa Lowassa na Sumaye kurudi tena CCM.

Kupanga ni kuchagua
Mmeshahama tena kutoka kwa Nyalandu? Ama kweli mtatangatanga mpaka ndala ziwakatikie njiani.
 
Kwani wajumbe wamesoma hizo mahesabu zenu?

Hesabu achia shule
wajumbe wapeyapinga maamuzi ya ngazi za juu ya chama kuwaleta wapinzani CCM kuunga juhudi. Hawakuunga mkono fikra za akina Polepole. Kama akina Bashiru watapingana na maoni ya wajumbe wao kuhusu matokeo ya kura za maoni kwa visingizio mbalimbali basi watakiona cha mtema kuni na wapinzani wakae mkao wa kula, maana wajumbe hawa wanazo clips za matusi kwa CCM ya akina Lijualikali na Nasari wakati wanagombea ubunge kwa tiketi vyama vya upinzani.
 
tatizo la kuandika huku unavuta mibange ndilo hilo! wewe unafahamu kuwa akili na uwezo wako wa kufikiri ni mdogo bado ile akili ndogo uliyo nayo unaiharibu kwa mibange!
Nisamehe mkuu, ila ujumbe si umeupata?
 
Mkuu usiwabeze sana wapinzani, hata CCM hakuko shwari. Hebu Ona wale waliounga juhudi kutoka upinzani walivyogaragazwa na wajumbe kwenye kura za maoni. Hii ni ishara tosha kuwa kule juu na huku chini ya chama hakuna mawasiliano yenye afya kwa chama.
Huko sio kubeza ni kuwaambia ukweli

Huwezi kufananisha chama kubwa na upinzani unakosea sana
 
Huko sio kubeza ni kuwaambia ukweli

Huwezi kufananisha chama kubwa na upinzani unakosea sana
Bila akina "Jecha" dhana ya chama kubwa na upinzani isingekuwa halisia. Upinzani una watu wengi saaana kaka, shida yao ni wasimamizi wa uchaguzi tu basi na matumizi mabaya ya vyombo vyetu. Hata wapinzani wanafahamu kuwa hawatashinda uchaguzi, ila wanatafuta ruzuku kubwa na ajira za ubunge na udiwani.
 
Kwenye uchaguzi wa 2020 Ni vigumu kusema CCM itachindwa na chama cha upinzani, lakini Vyama vya upinzani vinaweza kupata viti vingi vya ubunge na udiwani kama watamwachia Mh. Membe awe mgombea pekee kwa niaba ya vyama vya upinzani kuliko wakimsimamisha mgombea mwingine akiwemo mh. Lissu.

Baba wa taifa alishawahi kusema kuwa mgombea atakayekuja kuiangusha CCM madarakani atatoka CCM.

Hesabu ni rahisi tu, wasioipenda CCM na wanaoipenda chadema wapo tayari kumchagua yeyote hata kama ni kiazi.

Mh. Membe kama akigombea ataungwa mkono pia na wana CCM wengi na mashuhuri ambao ni rafiki zake na wale ambao wanakerwa na jinsi CCM ilivyo na inavyoendeshwa kwenye awamu ya tano.

Hivyo basi Membe atapata kura za marafiki zake na wanaokerwa na mambo ndani ya awamu ya tano na atapata kura za wasioipenda CCM, wanaotaka mabadiliko na wanaoipenda chadema au ACT, au NCCR.

Shida pekee ya Membe ni ya kile kilichotokea kwa Lowassa na Sumaye kurudi tena CCM.

Kupanga ni kuchagua, maoni tyuu.
Wana CCM watamshabikia Membe tu, SIYO kumuunga mkono kwani wanajua hana uwezo, ubavu, ujasiri wala "nia" ya kushinda; Membe kaenda kutia fujo tu kwenye karatasi za kuoigia kura (ballot papers) kwani hata vyama vingine vinajua hilo ndio maana, pamoja na kampeni yake ya "Grand Coalition" hakuna nayajibu; wote ni vyao vyao na wanangoja kuchukua fomu zakugombea urais kila mmoja kivyake vyake. Hapa umoja wa vyama vya upinzani hauwezekani kwani CDM walisha "umwa na nyoka" hawakubali. Vivyo hivyo akina CUF na wengine.
 
Kama unataka kujua ccm itashindwa fanya hesabu hii
1. Idadi ya wapiga kura vijijini
2. Idadi ya wapiga kura mjini
3. Idadi ya wanaccm kindakindaki
4. Idadi ya chadema wa yeye2020
5. Idadi ya Act
6. Idadibya Cuf ya mendechalii.

Then ujue kuwa
Majority ya watu kijijini ni ccm
Majority ya miji kadhaa upinzani

Itabidi tuziite hizi factors majina ya ×,y,z na C
Pia kura ya ushindinkama P

Then tuta calculate with simple deferential eqn
Kabla ya kuja kwenye Summation

Ni hesabu hakuna ramli wizi au Uchawi.

Narejea.....
 
Unadhani wasipoungana na Chadema ACT itasikilizwa na nani?!
Muulize Mrema kuwa kwenye chama kisichokuwa na wafuasi hata ukiitisha mkutano wa ndani ni ngumu wajumbe kujitokeza.
 
Shida ni kwamba Membe hawezi kuwashawisha wana CCM (wasioipenda CCM ya awamu ya tano) na rafiki zake wampende Lissu, kwao wao Membe is well known and secure than Lissu; fear of both known and unknown origin.

Na sisi hatumtaki Membe! msitukumbushe machungu ya awamu ya kina membe. Mkimweka huyo sote tunapigia ccm. tumechoka kuchezewa,
 
Kama unataka kujua ccm itashindwa fanya hesabu hii
1. Idadi ya wapiga kura vijijini
2. Idadi ya wapiga kura mjini
3. Idadi ya wanaccm kindakindaki
4. Idadi ya chadema wa yeye2020
5. Idadi ya Act
6. Idadibya Cuf ya mendechalii.

Then ujue kuwa
Majority ya watu kijijini ni ccm
Majority ya miji kadhaa upinzani

Itabidi tuziite hizi factors majina ya ×,y,z na C
Pia kura ya ushindinkama P

Then tuta calculate with simple deferential eqn
Kabla ya kuja kwenye Summation

Ni hesabu hakuna ramli wizi au Uchawi.

Narejea.....
Umesahau kuwa Kanda ya ziwa Ni wengi na hii ndio finali yao?
 
Unadhani wasipoungana na Chadema ACT itasikilizwa na nani?!
Muulize Mrema kuwa kwenye chama kisichokuwa na wafuasi hata ukiitisha mkutano wa ndani ni ngumu wajumbe kujitokeza.
Wananchi wameshaanza kufahamu kuwa Cha kinachoandamwa Sana na dola ndio Cha halisi Cha upinzani, wanataka hichohicho
 
Hivi wadau masoud kipanya alitengeneza kibonzo kimoja kinauliza nani tumtume term hii...kuna mtu ancho akitupie humu
 
Back
Top Bottom