Here is Russia's Response to NATO’s activities near Its borders

Here is Russia's Response to NATO’s activities near Its borders

Sio kweli kwamba Russia hana presence karibu na marekani.
Pili mafanikio ya Russia hapo syria sio kiduchu na ceasefire agreement says it all.
Tatu, sio wakati wote lazima uwe offensive japo sio kweli kwamba Russia hawezi kuwa offensive. Ni busara tu kuwa deffensive karibu na goli lako.
Nne, NATO sio taifa moja na hivyo sio busara kuwa-much kwenye kila military hardware, japo unaweza kuwa outsmart kwenye inteligence na tactics.
Tano, nchi nyingi zilizoshiriki kwa kina kwenye vita kuu ya pili ya dunia zimeamua military policy zao ziwe defensive. Majuzi tu kulikuwa na bill kwenye bunge la Japan ya kubadili military policy from defensive to offensive na watu wakachapana ngumi vibaya sana ndani ya bunge.
Sita, Russia ana allies ambao kijiografia hawako mbali sana hivyo hahitaji kuwa concerned peke yake na threats zote zinazomlenga.
Kaka naheshimu mawazo na uchambuzi wako kuhusu jambo hili,

Labda tu nifafanue kidogo kuhusu hayo unayoyaita mafanikio makubwa ya Russia katika kampeni yake ya Syria

Nimesoma chambuzi nyingi na kuwasikiliza wazungumzaji wengi wakiongea jambo hili na karibu wengi wanasema kampeni ya Russia nchini Syria ni partial success, ni mafanikio kiduchu

Kwa nini yanaitwa ni partial success?

Vita ya Syria ina umri wa miaka mitano, kabla ya warusi kuja, waasi hawakua na mafanikio ya kutisha katika mstari wa mbele wa mapambano, nazungumzia free Syrian army inayoungwa mkono na nchi za magharibi,
Hawa fsa kabla ya warusi kuja walikua wanashikilia maeneo mengi ya jimbo kubwa la Aleppo

Maeneo mengine walikua wamegawana makundi mengine madogo madogo yanayoitwa ya kigaidi nayo ni alnusra front, jaish Al Islam, jaish Al maidy na mengine kadhaa katika maeneo ya hama na homs
Maeneo yaliyo baki yalikua yakishikiliwa na daesh au ISIS, nako ni Palmyra na viunga vyake miji mingine yote iliyobaki ilishikiliwa na serikali ya Syria, hii ni kusema serikali ilishikilia 45% ya nchi na 65% ilishikiliwa na vikundi mbali mbali vya waasi na vile vya kigaidi

Warusi walipoingilia kati serikali imerejesha au kufikisha 65%ya nchi na sasa 45% ndio inashikiliwa na waasi, kwa hiyo difference hapo ni 20% kwa hiyo kama 20%ndio unaita mafanikio makubwa ni ajabu sana, na jeshi la serikali ndilo lilishikilia ardhi nzima ya nchi hapo kabla, labda wengi mtakua mnachanganywa na kelele za propaganda kutoka kwenye chombo cha propaganda cha Kremlin, sputniknews.com ambayo ndio mara nyingi sana ina exergerate russian success hapo Syria

Lakini kiukweli, ni mji mmoja tu wa Palmyra ndio ambao serikali iliukomboa wote kutoka kwa magaidi wa ISIS lakini miji mingine karibu yote iliyobaki ilikombolewa nusu, karibu kila mji nusu unashikiliwa na serikali na nusu waasi mbali mbali, mfano ni mji wa Aleppo ambao hadi sasa kaskazini Kuna serikali na kusini Kuna waasi ambako ndio supply line ya waasi ndio njia kuelekea mpaka wa turkey

Ni kweli kuwa mwezi January vikosi vya serikali viliwabana sana waasi na kuwapokonya baadhi ya waasi lakini maeneo yenyewe sio makubwa ki vile, tafuta ramani au mchoro wa maeneo ya Syria kwa sasa uone jinsi mgawanyo wa maeneo ulivyo, Kuna mashirika ya kimataifa yaliyo na watu wanaochukua takwimu ndani ya Syria, yanayoripoti UN, kazi zake ni hizi kujua Hali halisi ya vita, na Hali ya raia
Maeneo mengi yaliyokombolewa na serikali ni vijiji pembezoni mwa miji makubwa isipokua Palmyra na homs ndio wameikomboa yote, hata hivyo huko Palmyra na homs na jirani DAESH wamejazana vijijini na bado wanashikilia maeneo mengi

Kwa upande wa diplomacy, hakuna kitu kikubwa cha kujivunia kilichopatikana huko Geneva, wote tunajua mazungumzo yamevunjika kwa kushindwa kuelewana, misimamo waliyonayo kila upande tangu kuanza kwa vita 2011 ndio hiyo hiyo hadi leo
Cha ziada labda hiyo ceasefire tena inakua ni ya masaa 48, hivi sasa ndio kerry na lavrov wanajaribu kupata ya Muda mrefu kama ile ya February ambayo imevunjwa Muda mrefu

Hivyo hata tunavyoongea mapigano yanaendelea ndani ya Syria, hivi sasa serikali ya Syria inaweza kusimama kifua mbele kudai imeshinda vita hiyo? Wakati 45% ya nchi inakaliwa na waasi?

Kabla ya Russia kuja vita ilikua kama ipo stalemate, hakuna aliekua anachukua maeneo mapya, Russia ilipokuja serikali ikafanikiwa kurudisha baadhi ya vijiji na huo mji wa Palmyra na homs
Sasa hayo huwezi kuita ni mafanikio makubwa,

Na sasa hivi kama diplomacy itashindikana Russia itajikuta kwenye mazingira magumu sana, maana putin hataki kujikuta Russia imeingia kwenye ule mtego kama wa marekani kule Afghanistan, ni kweli America iliwashinda wataliban kwenye conventional war lakini wataliban wanaendelea kupambana kupitia gorilla warfare ambayo haiishi

Mgogoro wa Syria unaelekea huko, na putin hataki hilo ndio maana halali usiku na mchana anamtuma lavrov afanye juu Chini yeye na kerry wamalize mgogoro huo kwa mazungumzo, anajua fika ni vigumu kupata ushindi wa moja kwa moja kwenye gorilla warfare, hapo hapo yupo under pressure kutaka kuwafurahisha West ili wa muondolee vikwazo,

Kama kerry na lavrov watafanikiwa katika juhudi zao na kufanikisha kufunga mkataba wa kudumu hapo ndipo Russia atazoa credit zote
Kwa sasa tunaita mafanikio kiduchu yaani partial success
 
iran hajapata kubabaishwa na vile vikwazo,actually vikwazo havikuizuia iran kupiga hatua zake za kiuchumi duniani.
Na kuhusu russia usidhani kuja kwa delegation yao hapa ndo wanashida mno,utawapa nini labda wale maana kama ni resource,hakuna nchi ina maliasiri nyingi kama russia.
Ile haihitaji kuja kuchukua raw material wanajitosheleza
Mapenzi ni kitu kibaya sana, mapenzi yamekupofusha kabisa

Sharti kubwa kabisa la Iran kwa marekani ili kuachana na Mpango wake wa nuclear ni kuondolewa vikwazo vya kiuchumi, hii ina maana kuwa vikwazo viliiumiza Iran beyond repair

Hivi sasa Iran inalalamikia marekani kuwa haijatimiza wajibu wake kuiondolea vikwazo Iran, kwamba Iran inadai bado Kuna nchi nyingi zinaogopa kufanya biashara na Iran, na zaidi malalamiko ya Iran ni katika mifumo ya fedha, Iran inadai speed ya marekani na washirika wake kuruhusu Iran kuwa intergreted kwenye international financial system ni ndogo hivyo baadhi ya wabunge wa Iran wametaka Iran ijitoe kwenye mkataba ule
Hii yote ni desperation ya Iran kwamba vikwazo hivi vimeitesa sana na bado wanateseka

Naomba ufuatile kwa nn aviation industry ya Iran ilikufa kabisa, wakati majirani zake wa ghuba mashirika yao ya ndege yame boom, etihad, Emirates, na kadhalika, Iran kwenye sekta hiyo ni Hoi kabisa, kwa sababu ya vikwazo

Mafauta ya Iran yalikua na wanunuzi wachache sana wakati wa vikwazo, zaidi yaliuzwa kwenye black market
Sasa hivi ndio unaona rais wa Iran anakwenda italia France na kwingineko kutafuta upya wateja wa Mafauta na fursa zingine

Halaf wewe umekaa manzese dar es salaam unadai Iran unadai Iran haijawahi kubabaishwa na hivyo vikwazo?
Are you serious?
 
pendo shununu umekumbuka ku calculate myda ambao hiyo 20% ya ardhi ulitumika kuirejesha?
Na ungetueleza ni kwa nini mapambano ya kukomboa ardhi zaidi yamesimama.
 
pendo shununu nashindwa kuku quote kwasababu natumia simu yenye uwezo mdogo.
Kwanza nimefurahi kuona unainterest na international politics.
Dada yangu, vita ya Syria ilikuwa project ya USA kutokea mwanzo na hakuwa peke yake.
Kushindwa kwa project ni pale unaposhindwa kuifanikisha kwa wakati.
Angalia project ya Russia crimea ilivyoisha kwa wakati.
USA ameshakuwa wa kufail kwenye project nyingi za kijeshi, anashindwa kuwa clinical kwenye execution.
Ukifuatilia resources na muda alioutumia kwa FSA utaona margin ya failure. Hata mpaka sasa FSA inakuwa regurded kama motley collection of fighters.
Lengo la Russia Syria ilikuwa kuondoa jeshi la Syria kwenye deffensive position kwenda offensive na amefanikiwa, lengo lingine ni kumpa Bashar nguvu kwenye meza ya makubaliano na amefanikiwa.
USA sasa wamelegeza msimamo kuhusu Bashar, sasa wanamuona kama necessary evil.
Dada yangu, mimi ninafuatilia sana siasa za kimataifa na sichukui taarifa biased, naangalia ISNA, RT,CNN,TELEGRAPH,BBC,AL JA ZEERA, na hayapiti masaa 24 kabla sijafuatilia development ya taarifa.
 
iran ilikua under resistance economy na wangeendelea hivyo hata kwa miaka 100 bila tatizo lolote,waliojipendekeza kufanya mazungumzo ni wamarekani na wala iran hakua desperate kama unavyodai,ndo maana hakukubali kusitisha majaribio yake ya makombora,
licha ya vikwazo iran imekuwa na project kubwakubwa na nchi rafiki,kama kuwajengea power plants,rail etc,na hiyo maanake sio kwamba irani ilikuwa imekufa kiuchumi,
sawa iran atafaidika kama vikwazo vitaondoka na linaweza kuwa taifa lenye maendeleo sana lakini wairan wana utaifa sana na hawajikombi kwa mtu ,kumbuka iran ipo hapo tangu miaka 3000 nyuma,kwahiyo challenge ya vikwazo haziwezi kuitisha kivile
 
Ombi la ajabu kabisa hili! Ulitakiwa uiombee dunia ili vizazi viendelee kuishi kwa amani hata baada ya kuondoka kwako na sio yatokee ukiwa kaburini. Huo ni ubinafsi wa kiwango cha juu sana; kwamba maadamu haupo yatokee yoyote tu alimradi hayana madhara kwako. Kwa kweli hata huyo Mungu wako anakushangaa kwa ombi hilo la ajabu kwake.
Imeandikwa yatatokea na Mungu huwa habadiliki lazima yatokee. Ni unabii wa Mungu ambao haina budi utokee. Pona yetu ni Rehema zake zituguse Mimi na wewe mkuu.
Huwezi kuomba eti yasitokee wakati ni unabii na maovu yanazidi kuongezeka tuombe Mungu akingali bado kwenye kiti cha Rehema aturehemu. Hatuwezi nilibadili hilo
 
pendo shununu umekumbuka ku calculate myda ambao hiyo 20% ya ardhi ulitumika kuirejesha?
Na ungetueleza ni kwa nini mapambano ya kukomboa ardhi zaidi yamesimama.
Asante mkuu wa comment yako

Nimezingatia suala la Muda uliotumika kuikomboa ardhi, na hiyo ni sehemu ya success ambayo nimezungumzia hapo juu

Umeuliza kwa nn

Sababu kubwa ya ushindi au success hiyo katika Muda mfupi ni firepower ya Russia, kabla Russia hajaingia Syria vita vilipiganwa ardhini zaidi, jeshi la anga la Syria halikua na capabilities za kuwashinda waasi, Russia iliingia na nguvu kubwa, huwezi kulinganisha Russia na waasi, ndege za Russia ambazo ni sophisticated zinaruka umbali mrefu na kushambulia juu sana, na hii air campaign ndio ilileta hayo mafanikio niliyoyataja
Hapo kabla waasi pia walipata msaada kutoka turkey, saudia na Qatar, hata hivyo silaha hizo ni light arms, Silaha ndogo ndogo

Kulikua na mgawanyiko kati ya marekani na hao akina turkey kuhusu ni silaha gani waasi wapewe, maafisa wengi katika marekani hadi sasa wana hofu ya kuwapa waasi sophisticated weapons kwamba zinaweza kurudi kwenye mitaa ya nchi za magharibi

Kwa sasa marekani na washirika wanasema kama jitihada za kumaliza mgogoro zitakwama wataenda kwenye plan b ambao wengi wanasema itakua ni kuwapa waasi sophisticated weapons mfano MANPADS
MANPADS inazuia access kwa ndege za kisasa, hazitaweza tena ku operate kwa Uhuru
Wachambuzi wengi wa naamini tayari waasi wamepewa na America silaha hiyo ya MANPADS, wanasema hivyo Kutokana na hivi karibuni waasi kuitungua helicopter ya kisasa kabisa ya Russia, na kuzishusha ndege karibu nne za jeshi la Syria
 
baada ya marekani na washrika wake kuzindua mfumo mpya wa kinga dhidi ya makombora karibu na mipaka ya russia, rais wa nchi hiyo vladimir putin na viongozi waandamizi wa taifa hilo waliapa kujibu mapigo, kwamba russia itajibu mapigo kwa kiwango cha ajabu, kwa kweli walitoa matamshi makali sana na ya kuogofya

lakini kinyume na matarajio ya wengi wetu jana wizara ya ulinzi ya russia imetoa tamko kuwa itapeleka vikosi vipya katika mipaka yake yote inayopakana na nchi zote kulikowekwa mfumo huo wa kinga dhidi ya makombora kama majibu ya hatua hiyo ya NATO
kwa lugha rahis ni kwamba russia itapeleka kikosi mpakani na romania, croatia, slovakia na poland na vitakaa huko permanently, pia russia ita deploy radar na sencor kwenye maeneo hayo ya mipaka yake na NATO

kwa wale mashabiki wote wa taifa hili la russia nadhan watakua dissapointed na majibu haya ya russia kwa NATO na america, kwa mujibu wa wachambuzi hatua hii ni kama diffensive zaidi, maadui zako wanazidi kukuzunguka kila kukicha na wanaleta silah nzito jirani na wewe, halaf unajibu kwa kupeleka vikosi jirani na uchokozi huo ili kujilinda, ni ishara ya udhaifu
wengi tulitegemea majibu makali ikiwezekana russia nae apeleke vifaa jirani na marekani lakini imekua kinyume

sababu zinazofanya russia isichukue hatua kali

(1) russia imeumizwa kwa kiwango kikubwa na vikwazo vya EU na marekani , EU na marekani ni chumi kubwa dunuani kama zinakuwekea vikwazo ni lazima utaathirika sana, hapa unazungumzia mataifa 28 ya ulaya ambayo russia kwa miaka amekua akifanya nayo biashara mbali mbali ,leo ghafla biashara hizo zinakua restricted na accounts kuwa frozen ni lazima uchumi uyumbe sana,hali ya russia kiuchumi kwa sasa ni mbaya kutokana na vikwazo hivyo, na russia kwa siku za karibuni imekua ikihaha vikwazo hivyo viondolewe, imekua ikizitumia baadhi ya nchi kama france,germany na greece kushawishi wenzio wa EU Kuiondolea russia vikwazo, na wote mmeona jinsi france inavyowabembeleza wenzao ktk EU kuviondoa vikwazo hivyo
ndio maana vladimir putin na wenzie wameshindwa kuchukua hatua kali dhidi ya NATO Wakiogopa kuiudhi EU isije ikaongeza muda wa vikwazo ambao una expire mwishoni mwa mei

(2) kutokana na hali ngumu ya russia kiuchumi haiwezi kumudu kufungua kambi ya kijeshi katika nchi za latin america jirani na marekani, kitendo cha kwenda kumsaidia dikteta bashal al asad pia kimeigharimu russia kiuchumi, gharama ya vita kwa siku ni kubwa mno, bei ya kombora au bomu moja linalorushwa na ndege vita ni kubwa mno na russia imerusha kupitia ndege karibia mabomu laki moja na kitu tangu september last year, ndio maana ikadai kujiondoa haraka syria bada ya mafanikio kiduchu ya awali, hivi sasa kuna mvutano, asad anaiomba russia iendelee na mashambulizi huku russia ikikataa kufanya hivyo, ikimlazimisha assad afikie makubaliano na wapinzani haraka badala ya kuendelea kutegemea msaada wa kijeshi, maana russia pia ina maslahi yake mengine ikiwemo uhusiano mzuri na EU

HIVYO kwa sasa hivi russia hana janja mwingine zaidi ya kuwaangalia tu maadui zake wakimzunguka kwa vifaa na wanajeshi labda zaidi anaweza hapa na pale kujitutumua kwa kuzi intercept ndege za marekani na washirika wake katika eneo la baltic mbinu ambayo ni ya kawaida , hata wao NATO wana intercept sana ndege za russia katika anga la NATO

NATO is continuing its military buildup along Russia’s borders. However, Russia is responding to every step the alliance takes by deploying new defensive weapons at its borders.

According to an article on the foreign affairs analysis website Voltaire Network, Washington in fact will not attack Russia. Its military buildup is rather aimed at provoking Moscow, in order to justify NATO’s expansion in Central Europe.

Amid NATO’s increased military activities near Russian borders, Moscow has announced the creation of two new units in the Western Military District (in Smolensk and Voronezh) as well as a new division in the South Military District (Rostov-on-Don).

Service combat surveillance vehicle SBRM

At the same time, along the Russian borders with Finland, the Baltics and Poland Russia is now deploying Sova anti-intrusion networks. This equipment allows the surveillance and monitoring of several moving targets and their trajectories.

The Sova-SBRM (stands for Combat Surveillance Vehicle) is operated by a group of servicemen. It is based on the chassis of the GAZ-233036 Tigr combat vehicle.

The Sova-SBRM is equipped with up to 50-80 magnetic, seismic and acoustic sensors. The sensors can be integrated into a network in designated areas and are controlled remotely. Each sensor is designed to recognize the frequencies of a number of sound vibrations, including those produced by helicopters, aircraft and armored vehicles.

The sensors can detect a target at a distance of up 15 kilometers, with a maximum accuracy of two degrees. They also indicate the trajectory of a moving target.

The vehicle itself is equipped with a telescopic antenna, with an operational range of 40 km. It also has an eight-channel electro-optical system comprising video cameras, thermal imaging devices and laser range finders.

The crew of the vehicle also operates two mini-drones, with a flight time of 60 minutes.

The Sova-SBRM was designed and produced by the defensive company Almaz-Antey in the city of Tula. It underwent tests in 2013-2015. It was deployed to the Hmeymim airbase in Syria as part of its defense system.

Hivi members wakisoma maelezo yako yaliyo andikwa kwa lugha ya kiswahili tukilinganisha na yanayo semwa kwa lugha ya kingereza si inaonekana ni vitu viwili tofauti - sasa tuamini lipi tuache lipi?
 
Hivi members wakisoma maelezo yako yaliyo andikwa kwa lugha ya kiswahili tukilinganisha na yanayo semwa kwa lugha ya kingereza si inaonekana ni vitu viwili tofauti - sasa tuamini lipi tuache lipi?
Mwanzo ametoa uchambuzi wake kwa kiswahili hajasema ni direct translation
 
Putin anajua kuwa siku moja atalazimika kukabiliana na USA uso kwa uso. Putin is a pure soviet na mmoja kati ya watu walioumizwa sana na kusambaratika kwa USSR. Wamarekani wanamuogopa sana, Bush alisema dont trust those little blue eyes. Putin anataka kujenga taifa kubwa linaloheshimika na anataka ulimwengu uwaelewe warusi hivyo na uwakubali.
Hapa tuna watu wanaimba taarabu kwamba ukileta fyokofyoko tunakufyokoa ila hawajui waendeshe vipi nchi. Putin ni rafiki na wafanya biashara na marafiki zake wakubwa ni wafanyabiashara wakubwa.
Putin ana aproval ratings za juu mno Russia.
Putin haiwazii sana Marekani japo wao hawalali wakimuwaza. I like the man, he has a pokal face.
 
That's good
 
Asante mkuu wa comment yako

Nimezingatia suala la Muda uliotumika kuikomboa ardhi, na hiyo ni sehemu ya success ambayo nimezungumzia hapo juu

Umeuliza kwa nn

Sababu kubwa ya ushindi au success hiyo katika Muda mfupi ni firepower ya Russia, kabla Russia hajaingia Syria vita vilipiganwa ardhini zaidi, jeshi la anga la Syria halikua na capabilities za kuwashinda waasi, Russia iliingia na nguvu kubwa, huwezi kulinganisha Russia na waasi, ndege za Russia ambazo ni sophisticated zinaruka umbali mrefu na kushambulia juu sana, na hii air campaign ndio ilileta hayo mafanikio niliyoyataja
Hapo kabla waasi pia walipata msaada kutoka turkey, saudia na Qatar, hata hivyo silaha hizo ni light arms, Silaha ndogo ndogo

Kulikua na mgawanyiko kati ya marekani na hao akina turkey kuhusu ni silaha gani waasi wapewe, maafisa wengi katika marekani hadi sasa wana hofu ya kuwapa waasi sophisticated weapons kwamba zinaweza kurudi kwenye mitaa ya nchi za magharibi

Kwa sasa marekani na washirika wanasema kama jitihada za kumaliza mgogoro zitakwama wataenda kwenye plan b ambao wengi wanasema itakua ni kuwapa waasi sophisticated weapons mfano MANPADS
MANPADS inazuia access kwa ndege za kisasa, hazitaweza tena ku operate kwa Uhuru
Wachambuzi wengi wa naamini tayari waasi wamepewa na America silaha hiyo ya MANPADS, wanasema hivyo Kutokana na hivi karibuni waasi kuitungua helicopter ya kisasa kabisa ya Russia, na kuzishusha ndege karibu nne za jeshi la Syria

Labda nisahihishe kidogo, ni kweli ndege za Syria zilitunguliwa na waasi lakini helicopter hakutunguliwa ilipata matatizo ya kiufundi na hilo ni jambo la kawaida - eye witness wanasema hukuna missile yoyote iliyo tumika kudondosha helicopter ya jeshi la anga la Urusi - ni vizuri wakati mwingine kuwa wakweli.
 
Hivi members wakisoma maelezo yako yaliyo andikwa kwa lugha ya kiswahili tukilinganisha na yanayo semwa kwa lugha ya kingereza si inaonekana ni vitu viwili tofauti - sasa tuamini lipi tuache lipi?
Mkuu maelezo ya kiswahili ni uchambuzi wangu ambao ni mjumuisho wa habari hiyo kubwa iliyotoka last week, ni baada ya kusoma na kufuatilia uchambuzi kutoka vyombo vya kimataifa, Russia today, sputniknews.com, the National interest, defense magazine na aljazeera

Chini nikaweka habari yenyewe kama ilivyoripotiwa ili mtu upate picha ya ninachokizungumzia

Asante
 
Asante mkuu wa comment yako

Nimezingatia suala la Muda uliotumika kuikomboa ardhi, na hiyo ni sehemu ya success ambayo nimezungumzia hapo juu

Umeuliza kwa nn

Sababu kubwa ya ushindi au success hiyo katika Muda mfupi ni firepower ya Russia, kabla Russia hajaingia Syria vita vilipiganwa ardhini zaidi, jeshi la anga la Syria halikua na capabilities za kuwashinda waasi, Russia iliingia na nguvu kubwa, huwezi kulinganisha Russia na waasi, ndege za Russia ambazo ni sophisticated zinaruka umbali mrefu na kushambulia juu sana, na hii air campaign ndio ilileta hayo mafanikio niliyoyataja
Hapo kabla waasi pia walipata msaada kutoka turkey, saudia na Qatar, hata hivyo silaha hizo ni light arms, Silaha ndogo ndogo

Kulikua na mgawanyiko kati ya marekani na hao akina turkey kuhusu ni silaha gani waasi wapewe, maafisa wengi katika marekani hadi sasa wana hofu ya kuwapa waasi sophisticated weapons kwamba zinaweza kurudi kwenye mitaa ya nchi za magharibi

Kwa sasa marekani na washirika wanasema kama jitihada za kumaliza mgogoro zitakwama wataenda kwenye plan b ambao wengi wanasema itakua ni kuwapa waasi sophisticated weapons mfano MANPADS
MANPADS inazuia access kwa ndege za kisasa, hazitaweza tena ku operate kwa Uhuru
Wachambuzi wengi wa naamini tayari waasi wamepewa na America silaha hiyo ya MANPADS, wanasema hivyo Kutokana na hivi karibuni waasi kuitungua helicopter ya kisasa kabisa ya Russia, na kuzishusha ndege karibu nne za jeshi la Syria
Aisee dada upo vizuri kwenye haya mambo
Uchambuzi wako unaeleweka kwa urais kabisa

Najua kwamba kwenye mjadala kama huu haiwezi kutokea wote tukawa upande mmoja au tukawa na hitimisho moja, msomaji mwenyewe ataamua achukue lipi, hata kwa nondo hizi ulizotoa ni wazi wengi tutachukua msimamo huu
 
pendo shununu nashindwa kuku quote kwasababu natumia simu yenye uwezo mdogo.
Kwanza nimefurahi kuona unainterest na international politics.
Dada yangu, vita ya Syria ilikuwa project ya USA kutokea mwanzo na hakuwa peke yake.
Kushindwa kwa project ni pale unaposhindwa kuifanikisha kwa wakati.
Angalia project ya Russia crimea ilivyoisha kwa wakati.
USA ameshakuwa wa kufail kwenye project nyingi za kijeshi, anashindwa kuwa clinical kwenye execution.
Ukifuatilia resources na muda alioutumia kwa FSA utaona margin ya failure. Hata mpaka sasa FSA inakuwa regurded kama motley collection of fighters.
Lengo la Russia Syria ilikuwa kuondoa jeshi la Syria kwenye deffensive position kwenda offensive na amefanikiwa, lengo lingine ni kumpa Bashar nguvu kwenye meza ya makubaliano na amefanikiwa.
USA sasa wamelegeza msimamo kuhusu Bashar, sasa wanamuona kama necessary evil.
Dada yangu, mimi ninafuatilia sana siasa za kimataifa na sichukui taarifa biased, naangalia ISNA, RT,CNN,TELEGRAPH,BBC,AL JA ZEERA, na hayapiti masaa 24 kabla sijafuatilia development ya taarifa.
Nashindwa kuelewa mafanikio hayo ambayo mtoa mada anayaita "kiduchu" anataka kumaanisha nini, au comparison yake ipo kwa nani mwenye mafanikio makubwa sana Syria, ni nani huyo NATO? Turudi awali lengo kuu la USA na allies wake wa NATO lilikuwa ni kumfurusha na ikiwezekana wamuangamize Bashar al-Assad kama walivyofanya Libya.
Wakati hilo linakaribia kutimia Urusi ghafla akaingia uwanjani na hiyo ikawa a turning point hakika Urusi imekuwa a game changer kule Syria, ukweli huu hata kama hauwapendezi baadhi ya watu hautageuka na kuwa uongo.

Mosi, Urusi alitaka Assad asiondolewe madarakani kwa kuzuia kinachoitwa a regime change ya NATO, Assad bado yupo amefanikiwa au hajafanikiwa?

Pili kuharibu na kusambaratisha ngome za magaidi, route walizotumia kupitishia silaha, mafuta hilo pia amefanikiwa kwani hivi sasa hizo waasi na magaidi hali yao sio nzuri.

Tatu, kurudisha maeneo muhimu yaliyochukuliwa na magaidi hilo pia amefanikiwa kwa kiwango chake Syrian army linazidi push forward.

Nne, kijeshi Urusi alitaka kujaribu na kutangaza silaha zake kwa soko la silaha alizofanyia upgrade kubwa mfano Kalibr cruise missiles, electronic warfare systems n.k hapo hata NATO officers wanakubali accuracy and efficiency ya silaha hizo ni ya kuogofya ukilinganisha na zile za kwao.

Yote kwa yote Assad bado yupo na ikabidi waanzishe meza ya mazungumzo ili kutatua mgogoro ambao awali NATO hawakutaka hata kusikia hilo. Refugees kama tunavyoona wanazidi kufurika Ulaya na kutoa funzo ukiharibu mataifa ya watu YOU MUST PAY BACK THE PRICE.
Sasa hayo yote mtoa mada unayaita mafanikio "kiduchu"?
 
kwani kujibu mapigo wewe ulitaka afanyaje kwa mfano,ulitaka aishambulie marekani au?.
Putin yuko smart,ukitaka ujue how smart uliza wa ukraine watakwambia namna walivyostukia wanajeshi wa russia wameshainyakuwa crimea wakati wao wamelala,
mrusi anapokusogezea askari wa miguu mpakani mwako unatakiwa usilale hata sekunde kwani waweza stukia wamo ndani ukabaki unashangaa,baada yacrimea nadhani ulicheki kule east ukraine vile iliponea chupuchupu kunyakuliwa kama si wamarekani kujitahidi kuibebembeleza russia iwambie waliotaka kujitenga waweke silaha chini,
bila kusahau kule syria jinsi watu walivyoamka asubuhi na kukuta tayari putin kaingiza ndege zake bila hata ya satelite za marekani kugundua.
Sasa hao Romania wanawezastukia wajamaa wanapatrol ndani ya romania kama kukipatikana ulazima na wataidisable hiyo system mda wowote wakijisikia

habari ya kushambulia marekani umezitoa wapi?! putin hawazi kuthubutu kufanya huo upuuz unaofikiria make anajua mziki ulivyo mzito. mapigo anayojibu ndo hayo kusogeza majeshi mpakani, mapigo ya kitoto kweli. mwambie huyo putin amege nchi mwanachama wa nato akione cha moto teh!
 
putin kaingiza ndege zake bila hata ya satelite za marekani kugundua.
Sasa hao Romania wanawezastukia wajamaa wanapatrol ndani ya romania kama kukipatikana ulazima na wataidisable hiyo system mda wowote wakijisikia

hahaa! we balaa! afu kumbuka sisi humu sio wale uliozoea kuwaokota pale kijiwen kwenu,
mods watu vichwa panzi kama huyu tafuteni namna ya kuwafanya
 
Back
Top Bottom