Heeee mama kumbe ushenzi uliuanza zamani..........

mahirtwahir

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2013
Posts
614
Reaction score
322
Habari za mda huu wana MMU

Majira haya ya saa 4 usiku natoka kwa mupenzi ninaetarajia kumtia chuo (ndoa) aliniita nimpelekee hela ya kujikimu kwa matumizi.

Nimefika tumekaa barazani mara kapita mama yake alikua ameletewa ugoro akausifu kwa kua ni mwingi akasema enzi anasoma chuoni alikua akibeba na kuenda nao kupiga uraibu huko chuoni na baazi ya wanafunzi walikua wakimuomba na alikua akiwapatia ila ilikua ukiwazingua mara walie,wengine hujikojolea.

"Mama kumbe ushenzi uliuanza zamani" maneno hayo yamemtoka mtarajiwa wangu kumuambia mama ake mzazi tukiwa barazani mi sikupenda nikamfinya kidogo kumuonesha nimechukia na asirejee tena.

"Unanifinya namna hii kwani yule ni mama yako" kauli hii ilizidi kunichoma na kunifanya nichukie zaidi na kujenga masuali yasio na majibu kwa haraka.

Alinyanyuka mchumba wangu kuenda kuchukua chakula ili amletee mtoto ale pale nje aliponyanyuka yeye akaja dada yake kuja kunipa kapani na kunisalimia shemeji yake sikuona vibaya nikamsimulia kisa cha mdogo wake na kumtaka amkanye kwani yule ni mzee wake yapaswa kumuhishimu.

Basi hapo mapenzi yaligeuka yakawa uhasimu alipotuona tunaongea na dada yake yeye hakurudi tena pale akaa pembeni ili kumrizisha nikamuambia njoo tukae wote "Sina ten muda wa kukaa njee naenda kulala" hilo ndilo lililokua jibu lake.

Niliendelea kupiga stori na dada yake na kumuambia unaona majibu ya mdogo wako hayo jeee huko katika ndoa itakuaje " Shem tabia ni kama ngozi mvumilie tuuu" alinijibu

Nikamuita mupenzi aje nimuage niondoke " kama umechoka kutoa umbea nenda zako" mi nikaamua kuwasha usafiri wangu na kuondoka.

Niko njiani kuelekea home sms kibao
Ukikaa na malaya wako mi sitaki kuongelewa km mimi sikufai basi mchukuwe yeye tena namba yake nataka ufute ukome kunidiskasi na mpuuzi yule tabia yako hii sijapenda

Sms ziko kama 10 kapiga simu sijapokea kaengeza na nyengine sms za kulani

"Bby samahani zilikua ni hasira tuuu plz pokea simu yangu"

Mi mawazo yananipa nimwage manyanga hasa kwa vile nishagegeda sana maana naona huko katika ndoa kutakua ni sawa na uwanja wa fujo kwa staili hii

Wadau niambieni munaonaje hii hali?
jaalia imekutokea ww
 
Kaka angalia usije chuma janga, maaana mchuma janga hula na nduguze ni hayo tu.
 
kama mama yake anamwambia maneno ya hovyo mama yako si ndo atakimbizwa na mwiko???
 
Hajafunzwa kutumia nyama ya ulimi na pengine hivo ndio kawaida ya maongezi yao kwao...namaanisha kuwa na kauli nzuri au ni tabia yake tu ya uropokaji...mkanye anaweza kubadilika
 
Habari za mda huu wana MMU

Majira haya ya saa 4 usiku natoka kwa mupenzi ninaetarajia kumtia chuo (ndoa) aliniita nimpelekee hela ya kujikimu kwa matumizi.

Nimefika tumekaa barazani mara kapita mama yake alikua ameletewa ugoro akausifu kwa kua ni mwingi akasema enzi anasoma chuoni alikua akibeba na kuenda nao kupiga uraibu huko chuoni na baazi ya wanafunzi walikua wakimuomba na alikua akiwapatia ila ilikua ukiwazingua mara walie,wengine hujikojolea.

"Mama kumbe ushenzi uliuanza zamani" maneno hayo yamemtoka mtarajiwa wangu kumuambia mama ake mzazi tukiwa barazani mi sikupenda nikamfinya kidogo kumuonesha nimechukia na asirejee tena.

"Unanifinya namna hii kwani yule ni mama yako" kauli hii ilizidi kunichoma na kunifanya nichukie zaidi na kujenga masuali yasio na majibu kwa haraka.

Alinyanyuka mchumba wangu kuenda kuchukua chakula ili amletee mtoto ale pale nje aliponyanyuka yeye akaja dada yake kuja kunipa kapani na kunisalimia shemeji yake sikuona vibaya nikamsimulia kisa cha mdogo wake na kumtaka amkanye kwani yule ni mzee wake yapaswa kumuhishimu.

Basi hapo mapenzi yaligeuka yakawa uhasimu alipotuona tunaongea na dada yake yeye hakurudi tena pale akaa pembeni ili kumrizisha nikamuambia njoo tukae wote "Sina ten muda wa kukaa njee naenda kulala" hilo ndilo lililokua jibu lake.

Niliendelea kupiga stori na dada yake na kumuambia unaona majibu ya mdogo wako hayo jeee huko katika ndoa itakuaje " Shem tabia ni kama ngozi mvumilie tuuu" alinijibu

Nikamuita mupenzi aje nimuage niondoke " kama umechoka kutoa umbea nenda zako" mi nikaamua kuwasha usafiri wangu na kuondoka.

Niko njiani kuelekea home sms kibao
Ukikaa na malaya wako mi sitaki kuongelewa km mimi sikufai basi mchukuwe yeye tena namba yake nataka ufute ukome kunidiskasi na mpuuzi yule tabia yako hii sijapenda

Sms ziko kama 10 kapiga simu sijapokea kaengeza na nyengine sms za kulani

"Bby samahani zilikua ni hasira tuuu plz pokea simu yangu"

Mi mawazo yananipa nimwage manyanga hasa kwa vile nishagegeda sana maana naona huko katika ndoa kutakua ni sawa na uwanja wa fujo kwa staili hii

Wadau niambieni munaonaje hii hali?
jaalia imekutokea ww

hana adabu
 
Kha naweza kuelewa vyote ila binti kumsema mama ake hivyo tena mbele yako...hapana...ngashtuka kwa kweli...
Nu rahisi tu hapo kujua ndoa yenu itakuwa ya namna gani....
Huyu hashindwi kukuchambua mbele ya wageni au mmekosana nyumbani akaja kukunja tai ofisini mbele ya boss wako.
Heshima ya mwanamke ni pamoja na staha ya mdomo wake.....
 
Tafadhali muache mara moja kabla hujajilipuaa kwa risasi kama wa ufoo saro na munisi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom