MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,783
UTANGULIZI
Mambo mengi sana yameongelewa, lakini kuna yaliyofichika nyuma ya pazia. Unapoangalia mgogoro wa Ukraine na kuuchambua hebu tujitahidi kuzingatia haya mambo muhimu yafuatayo. Tuzingatie umuhimu wa kiuchumi wa nchi ya Ukraine kwenye siasa za Urusi, Marekani na Ulaya. Hapa nazungumzia utajiri wa rasilimali ambao nchi ile inayo, halafu mwishoni pima mwenyewe:
NAFASI YA UKRAINE KIUCHUMI BARANI ULAYA NA DUNIANI:
1. Ukraine ndiyo taifa kubwa zaidi barani Ulaya (Ukiitoa Urusi)
2. Ukraine inauwezo wa kufanya kilimo (Agricultural Potential) chenye kulisha watu milioni 600, bara zima la Ulaya.
3. Ukraine ndiyo taifa la kwanza barani Ulaya kwa kuwa na madini mengi ya Uranium (Ukiitoa Urusi)
4. Ukraine ndiyo taifa la pili barani Ulaya kuwa na madini mengi ya Tinanium (Duniani ni taifa la 10)
5. Ukraine ndiyo taifa la pili duniani kuwa na madini mengi ya Mangenese (Explored Manganese Reserves)
6. Ukraine hadi kufika mwaka 2020 lilikuwa ni taifa la saba lenye madini mengi ya chuma (2022 Imegundulika ni la pili duniani)
7. Ukraine ni taifa la pili barani Ulaya kuwa na madini mengi ya Mercury.
8. Ukraine ni taifa la kumi na tatu duniani lenye gesi nyingi (Shale Gas Reserves).
9. Ukraine ni taifa la saba duniani kuwa na hifadhi kubwa ya makaa ya mawe.
10. Ukraine ni taifa la tano kuwa na watu wengi barani Ulaya (Watu milioni 44).
MUHIMU KUFAHAMU:
Nchi ya Ukraine ilitaka kujiunga na Umoja wa Ulaya miaka ya 2010's lakini Raisi Viktor Yanukovich alikataa na kusema kamba tatizo ni kukuza uchumi basi ataenda kuomba mkopo wa dola za kimarekani bilioni 15 (Bail-Out) kutoka Urusi. Jambo hili, mazingira makubwa ya rushwa, pamoja na kukataa kuiingiza Ukraine NATO vilipelekea maandamano makubwa mwaka 2014. Yanukovich aliponea chupuchupu kuuawawa hadi alipokuja kuokolewa na kukimbiziwa nchini Urusi ambako yuko uhamishoni mpaka leo hii.
Endapo nchi ya Ukraine itajiunga na Umoja wa Ulaya, ukizingatia ina rasilimali nyingi na nguvu kubwa sana kiviwanda na kiteknolojia, hasa vile vilivyoacha na jamhuri ya kisovieti basi Ulaya inaweza ikapata utajiri mkubwa sana. Ukraine ikifanikiwa kiuchumi na kujiunga na NATO: Je, nchi ya Urusi itakuwa kwenye nafasi ipi (Hapa jawabu sina kabisa)
Is Ukranian Crisis a symptom of resource curse?