Hazina Haina Mpunga. Imefulia. Inapumulia Mashine

WAna JF , kuna uvumi kuwa HAZINA IMEKAUKA, na BUDGET ZILIZOPITISHWA ZINATAKIWA KUKATWA KWA ASILIMIA NYINGI. Hizi taarifa zimezagaa kila kona nchini......Je, watoto wetu watasoma tena wakati tunalipa ada kwa installments? Je, familia zetu zitaendelea kuwepo?

tafadhali mwana jamii yeyote mwenye news atujuze.

TRA kila siku wanakusanya, Hazina haiwezi kwisha labda vipaumbele ndivyo vimebadilika
 
WAna JF , kuna uvumi kuwa HAZINA IMEKAUKA, na BUDGET ZILIZOPITISHWA ZINATAKIWA KUKATWA KWA ASILIMIA NYINGI. Hizi taarifa zimezagaa kila kona nchini......Je, watoto wetu watasoma tena wakati tunalipa ada kwa installments? Je, familia zetu zitaendelea kuwepo?

tafadhali mwana jamii yeyote mwenye news atujuze.

Mimi naona hii serikali imekwisha na kama hawana pesa basi ni uzembe. kwani pale TRA makao makuu kuna watu wameingiza mizigo yao maelfu kwa maelfu TRA hawatoi bei kwa msingi huo serikali itapata mapato vipi?. Iwapo mteja ameingiza mzigo anasubiri akadiriwe kodi then inachukua miezi kutoa makadirio ya bei kama TRA ndiyo sehemu nyeti ya kukusanya mapato wazembe pesa itatoka wapi??
 
Japokuwa sina data juu ya hilo lakini hali serikalini ni mbaya, labda ndiyo wanavuta pumzi ili DOWANS ilipwe au wafadhili ndiyo wamegoma. Tutakula nyasi mwaka huu, mvua zimechelewa.

Na hiyo mvua ikija inyeshe Mwanza mjini, Mbeya mjini, Iringa mjini, Dar (Kawe na Ubungo), Arusha mjini, etc.. mashambani kote walaaniwe isipokuwa tu kule kwa wateule...nafikiri nimeeleweka vizuri
 
Pesa zipo bana. Pengine huu uvumi unalenga kujenga hoja ya kuahirisha kikao cha bunge cha February!
 
Hakuna uthibiti na nidhamu ya matumizi ya Fedha serikalini..,serikali imekuwa kama ufalme wa Kambare kila mtu sharubu,kila mwenye upenyo anakomba,matumaini yanabaki kwa wabunge je wataweza kuibana serikali kuelezea wapi fedha zinakwenda ? na kuwawajibisha watendaji wabadhirifu??? wacha tusubiri tuone ila hali ya kifedha ni mbaya..
 
Mimi naona hii serikali imekwisha na kama hawana pesa basi ni uzembe. kwani pale TRA makao makuu kuna watu wameingiza mizigo yao maelfu kwa maelfu TRA hawatoi bei kwa msingi huo serikali itapata mapato vipi?. Iwapo mteja ameingiza mzigo anasubiri akadiriwe kodi then inachukua miezi kutoa makadirio ya bei kama TRA ndiyo sehemu nyeti ya kukusanya mapato wazembe pesa itatoka wapi??

Wewe hujawahi sikia serikali inaishiwa pesa?? Au unafikiri kukulikotokea hayo TRA yao haikusanyi siyo?? Kama ni kweli TRA inakusanya za kutosha kila siku kama unavyotaka tuamini, unafikiri inakuwaje bado serikali inategemea wafadhiri??
 
Naomba niamini hii kama taarifa na sio tetesi kwa sababu moja hii hapa Chini.
Hivi majuzi nimesikia serikali itawalipa watumishi wake dirishani ili kubaini watumishi hewa!

MY TAKE:
Hazina itakua haina hela za kutosha so wameamua kupunguza zigo la kulipa na watumishi hewa, Kumbe walikua wanajua kuna watumishi hewa wanakujla mshahara?
Mkiona hivyo jueni kweli fungu la mshahara hautoshi. Nawashauri mtakaolipwa dirishani muwahi foleni kwasababu unaweza kuwa kwenye foleni ukasikia mapesa yameisha.

SWALI:
Hivi hzi foleni zitakua ndefu kama zile za NMB mwisho wa Mwezi?
 
Msiseme sana, mtasababisha jamaa akimbilie Saudia kama yule mwenzake wa Tunisia!
 
WAna JF , kuna uvumi kuwa HAZINA IMEKAUKA, na BUDGET ZILIZOPITISHWA ZINATAKIWA KUKATWA KWA ASILIMIA NYINGI. Hizi taarifa zimezagaa kila kona nchini......Je, watoto wetu watasoma tena wakati tunalipa ada kwa installments? Je, familia zetu zitaendelea kuwepo?

tafadhali mwana jamii yeyote mwenye news atujuze.

Kwa matumizi yasiyokuwa na mpangilio kwa muda mrefu hili jambo ni lazima litokee. Hata hivyo lilichelewa sana kujitokeza. Kilichochelewesha jambo hili ni ule ukweli kwamba nchi yetu ni tajiri na ina vyanzo vingi vya mapato.

Hata hivyo, hii management crisis inaweza kuangusha serikali ya sasa...kama hali haitadhibitiwa kwa hekima
 
Mi naona system nzima ingolewe tu kama tuunisia no way hawataendelea kula na kujilimbikizia jaman, its hard to go on top but much harder to stay there, ndio washapanda kushukka itakua ngumu mpk washushwe....:disapointed:
 
hela hamna? nini .....
acheni utani benki zimejaaa, watu wanalipa kodi za mapato,waajiri wanawakilisha makusanyo+..........
 
Back
Top Bottom