Hayo ya mjengoni ni manyunyu tu, nvua yenyewe yaja upesi...!

Siao

Member
Jan 4, 2008
96
3
naamini ni haki ya wananchi kuonyesha pia hisiozao kuwa hawakufurahsihwa na uchakachuaji wa matokeo ya uchaguzi uliopita.

mkwere hatapata shida hapo mjengoni tu, anasubiriwa na ZOMEA ZOMEA MIKOANI...!!

Ni lazima sasa wamtajie "don`t go areas" - Mbeya, arusha, mwanza, moshi, kigoma, nk...! Ziara zitakuwa ngumu mno.

kwani kuchaguliwa waziri kwenye kipindi hiki hata ni raha tena - hiyo ZOMEA ZOMEA itanyima waheshimiwa raha kabisa.

Tena ninavyoona wameanza kutuonyesha sisi ni wajinga - kuchagua marafiki - kuwapa posti - itakuwa ngumu marafiki hawa kupita njiani.

Sijui waziri wa afya au elimu alikuwa arusha, au sijui mbeya - itakuwa sio kitu cha fahari tena.

Ni ngumu kuongoza kwa nguvu watu ambao hukuwa chaguo lao.

Hata hivyo kipimo cha mwisho ni kama wataendeleza uswahili na hadithi kama kipindi kilichopita. Hapa sasa itakuwa ngumu zaidi.
Huu ni ushauri wa bure!!!
 

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,856
399
Kwa mikoa ya mbeya, arusha, mwanza, kigoma, iringa nina wasiwasi hata mawaziri wanaweza wakazomewa pia. Hapo ndipo watakapotambua kuwa kuongoza watu bila ridhaa yao ni sawa na kukalia kaa la moto.
 

rmb

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
223
6
ha ha ha kwani mikoani anafanya safari mara ngapi? hatutampa kirahisi maana atataka kulipizia safari za kwenda nje maana kakaa Bongo sana! kama kuzomea inabidi kwenda kumvizia njia panda ya kuelekea ulaya na marekani (Airport) huko tutampata! sina hakika safari za mikoani atakuwa nazo ngapi ktk miaka 5 ijayo!
 

cammory

Member
Mar 18, 2009
17
0
Jamani wabunge wa CCM wameshaanza kwa kuzomea wabunge wa CHADEMA wakati wakitoka mjengobi. Aanzae mmalizie LONG LIVE CHADEMA
 
0 Reactions
Reply
Top Bottom