Hayati Mwalimu Nyerere alionya juu ya Katiba iliyopo; Awamu ya 6 inaogopa nini kuendeleza mchakato wa Katiba Mpya?

Lord OSAGYEFO

JF-Expert Member
Feb 19, 2021
3,086
4,881
Nimekuwa anafuatilia baadhi ya hotuba za Hayati Baba wa Taifa hili Mwl. Julius Nyerere

Moja ya hotuba yake ni ile aliyoizungumzia Katiba liliyopo kuwa ni Katiba ambayo ikimpata Rais atakayeitumia vibaya basi atakuwa Dikteta kwa wananchi anaowaongoza.

Nampongeza sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete kwa uthubutu wake wa kuanzisha mchakato wa Katiba Mpya lakini mahafidhina ndani ya CCM waliuvuruga mchakato ule.

Awamu ya 5 ilipoingia madarakani haikuitaka kabisa Katiba Mpya na kudai sio kipaumbele na wote ni mashahidi namna utawala wa Rais wa awamu ya 5 ulivyokuwa mgumu hasa kwa wapinzani hususani CHADEMA kutokana na matumizi mabaya ya Katiba

Rais wa 6 naYe inaonekana hana kabisa mpango wa kuendeleza mchakato wa katiba mpya jambo ambalo tunashindwa kuelewa hivi kauli ya Hayati Baba wa Taifa juu ya ubovu wa katiba iliyopo hawauoni ?

Pili kwanini hawataki kuendeleza mchakato wa katiba mpya aliouacha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete ?
 
Kwani yeye alishindwa kubadili katiba kipindi akiwa mtawala shida ya viongozi wengi wa Afrika ni kuwa wanafiki hasa pale wakiwa nje ya mfumo.
 
Kabla ya kupamba kupata katiba mpya kwanza tujue huo mchakato wa katiba mpya utaanza upya au laaa! Au tutaendeleza mchakato wa ile rasimu ya warioba au tutaendelea kupiga kura ile rasimu inayo pendekezwa iliyo najisiwa na CCM? Tuanzie hapo kwanza
 
Pili kwanini hawataki kuendeleza mchakato wa katiba mpya aliouacha Rais Mstaafu Jakaya Kikwete
Mkuu 'Lord', hivi kweli hujui kwa nini hawataki katiba mpya au unajifanya tu kinafiki kuuliza swali lililo na jibu wazi kabisa?

Ingekuwa ni wewe katika nafasi yake ungeanzisha mchakato wa kupata katiba mpya, hasa baada ya kujua kwamba kutokana na mambo mengi mabaya wanayoyafanya kwa wananchi hawana njia ya kurudi madarakani kama katiba mpya itakuwepo na kutekelezwa ipasavyo!

'Maza Mizinguo' hawezi kuruhusu mchakato wa katiba mpya huku akijua katiba hiyo hiyo itamwondoa madarakani hapo 2025.

Njia pekee ni kumlazimisha, vinginevyo sahau kabsa yeye kufanya kazi hiyo kwa hiari yake mwenyewe.
 
Kwani yeye alishindwa kubadili katiba kipindi akiwa mtawala shida ya viongozi wengi wa Afrika ni kuwa wanafiki hasa pale wakiwa nje ya mfumo.
Kila jambo na wakati wake. Yeye hakushindwa, bali haikuwa wakati wa kufanya kazi hiyo kutokana na hali iliyokuwepo wakati huo.

Kuna viongozi wenye "unafiki", lakini hiyo haikuwahi kuwa sifa moja aliyokuwa nayo Mwalimu.

Inaonekana huna hata chembe ya ufahamu juu yake.
 
Kila jambo na wakati wake. Yeye hakushindwa, bali haikuwa wakati wa kufanya kazi hiyo kutokana na hali iliyokuwepo wakati huo.
Kuna viongozi wenye "unafiki", lakini hiyo haikuwahi kuwa sifa moja aliyokuwa nayo Mwalimu. Inaonekana huna hata chembe ya ufahamu juu yake.
Kama mwenyewe aliona katiba ilikuwa mbovu na kukiri kwa kinywa chake yanini alishindwa kutatua shida ambayo alikuwa kasha iona kwamba ni shida ukweli utabaki kuwa ukweli viongozi wengi hasa Afrika hujifanya na maono mazuri hasa pale mfumo unapo watupa nje
 
Kama mwenyewe aliona katiba ilikuwa mbovu na kukiri kwa kinywa chake yanini alishindwa kutatua shida ambayo alikuwa kasha iona kwamba ni shida ukweli utabaki kuwa ukweli viongozi wengi hasa Afrika hujifanya na maono mazuri hasa pale mfumo unapo watupa nje
Sasa ukweli ni upi?
Mwalimu alijua ubovu wa katiba iliyokuwepo wakati huo, na akaeleza. Yaani baada ya wakati huo, miaka yoooote hii iliyopita, bado unang'ang'ania ni yeye tu alitakiwa arekebishe hiyo katiba mbovu?
 
Back
Top Bottom