Kila siku huwa naipitia Rasimu hii nikijiuliza hasa ni kitu gani kinafanya inakosa Uthamani mbele ya Watawala na wapinzani au Ni neno Tanganyika lililosheheni kwenye katiba hiyo?
Au Ni serikali Tatu zilizopo kwenye sura ya Sita na Saba ya katiba hiyo na Ibara ya 60 na kuendelea ya katiba...
Salam zangu ziwafikie Kabudi, Warioba na Polepole.
Sasa nawaelewa rasmi kwamba maoni ya wananchi yalikuwa sahihi.
Muundo wa Serikali tatu Sasa unaanza kuonekana ni mhimu ukawepo. Serikali Moja na hii ya Sasa zinamapungufu mengi.
Ile katiba iliyotokana na tume ya Warioba, watu wengi wanakubaliana nayo na ilitumia gharama kubwa kwenye tume kukusanya maoni na kuiandika. hivi kwanini tusiadopt tu ile katiba iwe ndio katiba yetu mpya ili tumalize ubishi huu wakatiba mpya? maoni yangu tu lakini.
Nimekuwa anafuatilia baadhi ya hotuba za Hayati Baba wa Taifa hili Mwl. Julius Nyerere
Moja ya hotuba yake ni ile aliyoizungumzia Katiba liliyopo kuwa ni Katiba ambayo ikimpata Rais atakayeitumia vibaya basi atakuwa Dikteta kwa wananchi anaowaongoza.
Nampongeza sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete...
Habari Tanzania!
Poleni kwa mihangaiko ya hapa na pale kwa marika yote.
Napenda kutoa wazo kwa Utawala wa sasa na ule ujao kama itawapendeza na kuona inafaa kwao; na wanapenda kuona kesho yao ikiwa nzuri wanapaswa kwanza kulifufua upya Azimio la Arusha na baadae ndio pafanyike kusimikisha...
Muda ni sasa, kesho ipo karibu sana na tutashtukia tayari 2025 hiyo. Hatuna Tume Huru wala Katiba mpya.
Kama tuna pesa za Mwenge wa Uhuru tunakosa vipi pesa ya kumalizia Katiba ambayo ipo tayari kwa 90%?
Kama tuna pesa za kufanya SENSA ya watu na makazi mwaka 2022 tunakosaje pesa ya kumalizia...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.