Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Kifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.

Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.

Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.

Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?

Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.

Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!

Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.

Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.

Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.

Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.

Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.

Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.

Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?

Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!

Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.

Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.

Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.

Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.

Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.

Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.

Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.

Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?

Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
Dah umenitoa machozi mkuu. Hakika ghazabu ya Mungu kwa wanaokebehi kifo cha Dkt Magufuli yaja. Dkt Magufuli kila alilolifanya lilikuwa kwa ajili ya Tanzania na Watanzania. Alipokataa kusafiri nje kwa ajili ya kubana matumizi alimfikiria mwananchi wa kijijini ambaye ni masikini anahitaji dawa, yeye akaone bora niwakilishwe ili hela nitakayoiokoa imsaidie mtanzania maskini. Nadhani nchi kama nchi bado tupo darasani kuhusu kifo cha Dkt Magufuli. Ni Muhimu Mama Samia akaligundua mapema na kulirekebisha. Maana ni ajabu sana aliachia Dkt Magufuli achafuliwe, atukanwe, kudhalilishwa, kudhihakiwa na kupewa adhabu ya kifo na wahusika kama vile wao ndiyo walipanga kifo cha Dkt Magufuli. Mbona Dkt Magufuli alizuia Dkt JK asitukanwe, na mbona Dkt JK alizuia Mkapa asitukanwe. Mama Samia aelewe familia yake itapata tabu sana siku akiondoka madarakani kama hatajenga msimamo wa watangulizi kutokudhalilishwa. Anapoachia kauli zinatolewa kuonesha eti Dkt Magufuli alikuwa katili na yeye siyo katili hiyo haisaidii maana mamlaka ni ile ile na akiondoka na yeye atazodolewa sana.
 
Unajua warusi wamchukuliaje Stallin? Unajua Wajerumani na baadhi ya nchi za Scandinavia zinamchukuliaje Hitler? Unajua Saddam alie hesabika na mmarekani kuwa ni dicteta alichukuliwaje na wa Iraq?

Shida tunadhani hizi nchi zinazojifanya kuwa zinaelewa kila kitu zikisema nasi tunakariri tukidhani wako sawa. Stallin haongelewi vibaya Urusi, bali maadui zake wakiongozwa na wabaya wa Urusi.

Hii misukumo ya kutoka nje kusema fulani mbaya ndo tumerithi waafrika. Tunasubiri kuambiwa kiongozi wenu mbaya. Gadaffi wa Libya pamoja na mazuri yote aliyowafanyia wa Libya wakaambiwa huyo ni dicteta akili zao zikafuata cha kuambiwa wakamuuwa.
Ndipo nampenda KIkwete kwa misemo yake yenye hekima..."Cha kuambiwa changanya na akili zako"
Ubaya au Wema wa mtu ni kama mchana hauhitaji tochi kuumulika
 
Acha kumtisha Mh. Rais,hakuna wa kufanya huu ujinga.
Simtishi, ni uhalisia wa mambo yanavyoweza kutokea. Unadhani urais ni mtu, ni mfumo wa mimi na wewe. Watu watamtukana na kumdhalilisha kama alivyokubali mwenzake aitwe majina yote mabaya na yeye Mama kushangilia as if anafanya kitu kizuri. Kwanza hapakuwa na haja na kujitenga na serikali ya awamu ya Dkt Magufuli. Yeye alipaswa aoneshe msimamo toka mwanzo lakini sasa karuhusu watu eti wamuone yeye ni bora na afadhali Dkt Magufuli alikufa kwa sababu eti alikuwa mkali na kwa sababu eti alikuwa anatuma wawakilishi tu kwenda nje.
 
Watu watamtukana na kumdhalilisha kama alivyokubali mwenzake aitwe majina yote mabaya na yeye Mama kushangilia as if anafanya kitu kizuri.
Mama hakuwahi kushangilia mtangulizi wake akidhalilishwa acha kumzushia uongo.

Kwanza hapakuwa na haja na kujitenga na serikali ya awamu ya Dkt Magufuli.
Hakuwahi kujitenga na serikali ya mtangulizi wake wala hawezi kujitenga nayo maana alikuwa sehemu ya utawala huo, tena kwenye madaraka makubwa ndio maana aliweza kumrithi.


Yeye alipaswa aoneshe msimamo toka mwanzo lakini sasa karuhusu watu eti wamuone yeye ni bora na afadhali Dkt Magufuli alikufa kwa sababu eti alikuwa mkali na kwa sababu eti alikuwa anatuma wawakilishi tu kwenda nje
Huwezi kuzuia watu kukuona bora au hufai, ndio maana wapo wanaompongeza na kumpinga vile vile (kama wewe).

Acha kumtwisha lawama zisizo na ukweli.
 
labda watakuja kukushangaa wewe ulivyokua mjinga Kwa kua na mahaba na chama chakavu kilichofeli kuitoa nchi Kwenye umaskini uliotopea Kwa wananchi wake Kwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru halafu Babu Kama wewe ukawa unatumika na kuhadaiwa Kama toilet paper Kwa kupewa tisheti na kofia ya kijani Ili uwapigie kura
Utashangawa sana!

kila mtu apambane na umasikini wa kwake,hata hao chadema wanaokudanyanya wana nia njema,wanakudharau ndio maana.
 
Bahati mbaya,mabaya ndio hukaa kwenye kumbukumbu kwa muda mrefu zaidi kuliko "mema"
"Heri wafu wafao katika Bwana naam asema roho wapate kupumzika kwa maana matendo yao hufuatana nao" jamaa hataki matendo ya mahaba wake yafuatane nae! Bila kusahau aya "Kuluhakah wanaikarah mulah" sema kweli japo moyo unauma.
 
Kusema mtu alivyo sio kumhukumu, ni kutoa maoni. Hukumu duniani hutolewa na majaji na ya kwenda Jehanamu hutolea na Mungu.
Mada yangu haiongelei hao watu, naongelea mtu kuhukumiwa, je sisi binadamu tuna mamlaka ya kuhukumu? Hata kama mtu alifanya makosa? Soma uelewe mada usikurupuke. Ndo maana nikasema hata Kaini aliuwa kwanini Mungu bado alimlinda Kaini? Watu wengi ukurupuka wajui mada inachosema. Lakini pia hao unao wataja unaushahidi kuwa Magufuli aliwauwa? Mbona kumekuwa na tuhuma za Ben Sanane kuuwawa na Boss wake, Kumekuwa na tuhuma alie kuwa Makamu mwenyekiti wa Chadema kuuwawa na Mwenyekiti?

Lakini watu wangapi wamepoteza maisha nyakati za uongozi tofauti? Hii haiwezi kukufanya uhukumu. Anae hukumu ni Mungu pekee!
 
Simtishi, ni uhalisia wa mambo yanavyoweza kutokea. Unadhani urais ni mtu, ni mfumo wa mimi na wewe. Watu watamtukana na kumdhalilisha kama alivyokubali mwenzake aitwe majina yote mabaya na yeye Mama kushangilia as if anafanya kitu kizuri. Kwanza hapakuwa na haja na kujitenga na serikali ya awamu ya Dkt Magufuli. Yeye alipaswa aoneshe msimamo toka mwanzo lakini sasa karuhusu watu eti wamuone yeye ni bora na afadhali Dkt Magufuli alikufa kwa sababu eti alikuwa mkali na kwa sababu eti alikuwa anatuma wawakilishi tu kwenda nje.
Mama alitaka kujiuzuru huo umakamu wa Rais kwa sababu ya huyu mshamba wenu kama ulikuwa hujui.
 
Simtishi, ni uhalisia wa mambo yanavyoweza kutokea. Unadhani urais ni mtu, ni mfumo wa mimi na wewe. Watu watamtukana na kumdhalilisha kama alivyokubali mwenzake aitwe majina yote mabaya na yeye Mama kushangilia as if anafanya kitu kizuri. Kwanza hapakuwa na haja na kujitenga na serikali ya awamu ya Dkt Magufuli. Yeye alipaswa aoneshe msimamo toka mwanzo lakini sasa karuhusu watu eti wamuone yeye ni bora na afadhali Dkt Magufuli alikufa kwa sababu eti alikuwa mkali na kwa sababu eti alikuwa anatuma wawakilishi tu kwenda nje.
Mnahangaika sana pro Jiwe. Huyo hawezi kurudi wala kudumu kwenye mipango ya nchi hii. Aliupata kwa bahati mbaya na bahati mbaya pia amekomea njiani bila kuacha sumu zaidi .

Mtu yeyote aliye serious ktk kutafuta maisha ya family yake. Hawezi kushobokea mwendazake labda wanyonge waliopumgazwa na propaganda.
 
kama wewe ni zao la ccm,basi ni team mapoda au msoga inc & company.

hakuna mwana ccm au mwanacdm makini na taifa hili anayembeza jpm,ni viazi mbatata wazee wa slope ndio alijua kuwafirigisa.
hahahaaha wazelendo uchwara wa sukuma gang mnateseka Sana Si mlijifanya wajanja nyie yaani mlitoka kwenu kolomije na chattle Kwa kudandia malori kuja town,halafu mnajitia kuujua mji na nchi kiujumla haya Leo ujuaji wenu upo wapi?

Spidi na mbwembwe nyiiingi za kujimwambafai na kutukana wakubwa zenu Leo mmemute Kama Kobe sisi tuliwaambia mapema Kwa ushamba wenu na propaganda uchwara za kianology na mungumtu wenu Jiwe aliejaliwa roho mbaya,katili na ujuaji hamtafika Mbali
Leo Kiko wapi?
Karma!
😁😁😁😁
 
Ndo haya nisemayo, kufa kwa mtu ni mpango wa Mungu, hata asingekuwa Rais ange

Wapo ambao nafahamu walisali sana na kumlilia Mungu kutokana na dhuluma ya utawala wa marehemu dhidi ya wapendwa wao ambao kwa uhakika walijua hawakuwa na hatia.

Hawakuomba kifo cha Magufuli bali waliomba dhuluma na utawala wa dhuluma ukome. Ukome kwa namna gani, walimwachia Mungu. Japo siamini kama kuna aliyedhani ungekoma kwa kifo.

Nilienda Segerea mara 8, kwaajili ya kumwona ndugu yangu. Niliongea na baadhi ya watu, wazee, akina mama, watoto, n.k; ambao ndugu zao walikuwa wamerundikwa ndani kwa kusingiziwa uhujumu uchumi. Wengine walikuwa wanashindwa hata kujizuia kulia. Walisimulia huku wakitokwa machozi kwa namna ndugu zao walivyoonewa, walivyoteswa, walivyotekwa. Wengine walikuja kufahamu ndugu zao wapo Segerea baada ya miezi miwili. Ndugu yangu ambaye alikaa huko kwa zaidi ya mwaka, natambua kwa 100%, hakuwa na hatia. Baadaye aliachiwa. Niliulizia sana kutaka kujua kosa lake, nilichoambiwa baadaye ni kuwa hata ningeuliza vipi hata iwe kwa nani, hakuna atakayeniambia kosa la huyo ndugu yangu. Yalikuwa ni maagizo ya marehemu mwenyewe na ndiye atanayejua aachiwe lini.

Mmoja wa maafisa wa juu kwenye vyombo vya usalama, alieleza kuwa kosa la ndugu yangu, aliwaambia, ni kutaka kushindana naye. Katika nini, hakuna ajuaye.

Bado nasisitiza kuwa kuna watu waliomba sana, siyo kumwombea kifo bali kutaka tuwe na utawala wa haki, utawala usiodhulumu watu.

Pamoja na yote aliyofanyiwa ndugu yangu, sikufurahia kifo cha Magufuli ila ningefurahi kama angeondoka madarakani, ashuhudie watu watakavyofurahi wapatapo mtawala mwenye hekima na upendo, na hata kushtakiwa au kupata nafasi ya yeye binafsi kujutia yale mabaya aliyoyafanya dhidi ya wanadamu wenzake. Lakini ni nani mimi wa kuhoja hekima ya Mungu. Muumba wetu hakosei, hachelewi wala kuwahi kupita kiasi bali huwajalia waja wake kilicho sahihi, kwa wakati sahihi na kwa namna sahihi. Mengine tunafunulia kuyatambua tukiwa hapa Duniani, mengine hatutayajua kamwe ila tujuacho ni kuwa Mungu wetu hakosei, na utawala wake ni wenye hekima kuu.

Tuzidi kuomba kupitia kifo cha huyu mwenzetu na wengine, ili kupitia kwao tuisikie sauti ya Mungu.
Umeongea vyema sana ndugu! Ila mtoa mada huyu siyo bure, utadhani ni kama mzimu wa Magufuli unamtetea Magufuli. Huyu Mtoa mada ni kama aliyevaa miwani ya mbao, hawezi kuona hoja nyingine nzuri ya mtu mwingine kwa vile tu inapingana na hoja yake. Pili, kuna watu wanajua 100% kuwa wameonewa, na Magu mwenyewe alikuwa anajua wameonewa kwa sababu zake tu za kisiasa na masifa yake tu. Lakini yeye Magu alifika mbali kusema uwongo madhabahuni (kwa kitu ambacho sisi tunajua ukweli wake 100%). Yule bwana kulikuwa na kipande cha kichwa chake kilikuwa na kichaa kabisa na alikuwa hajui kama ni kichaa, kama ambavyo kichaa wa kawaida huwa hajui kama yuko uchi, yeye anadhani nyie wenye nguo ndo mko uchi.

Mtoa mada, mshukuru sana Mungu kama hukuwahi kuguswa na negative part ya Magufuli. CCM wenyewe asilimia kubwa walionja shubiri, viongozi hata waliotaka kujiuzulu kupinga dhuluma walishindwa kwa vile wangeonekana wazi wanampinga, na hivyo wangekiona cha mtema kuni wao na ''shangazi'' zao na ndugu zao na network zao zote. Ikabaki kuwa nchi ya unafiki na kusifia kwa kwenda mbele. Critical minds za Vyuo Vikuu zikanyamaza kimyaaa.

Kwa ujumla, tujue tu kuwa hatuwezi kuwazuia watu kuongea ukweli wanaoujua wenyewe, na hata hisia zao. Mungu atajua anayesema ukweli na ayesema uwongo. Tuwaachie waseme mema na mabaya, ili watawala wengine wajifunze. Huhitaji kutumia nguvu nyingi kutetea wema wa Kiongozi- unakuwa uko wazi ; na pia ubaya wa Kiongozi huwezi kuuficha unakuwa uko wazi tu.

Namna unavyoishi, unavyofanya, unavyoongoza, unavyoongea etc- yaani mwenendo na tabia zako wewe, ndizo zinazofundisha watu wengine namna ambavyo wataku-treat. The way you behave, teaches others how they should treat you.
 
Back
Top Bottom