Hayati Dkt. Magufuli anapohukumiwa kwa kifo chake

Wilderness Voice

JF-Expert Member
May 19, 2016
921
1,638
Kifo ni tukio la kiasili. Katika imani kadhaa za kidini zina elezea kifo kilitokea baada ya Adamu na Hawa (Eva) kwenda kinyume na mapenzi ya muumba wao (MUNGU). Ndipo Mungu alitamka kuwa tutakufa, au kurejea katika mavumbi.

Binadamu wa kwanza kufa alikuwa Abeli. Ambaye aliuliwa na kakaye aitwae Kaini. Kaini japo alimuuwa Abeli, bado Mungu alimlinda Kaini na hata akasema atakae muuwa kaini basi atalaaniwa. Hivyo Mungu alimpeleka Kaini nchi ya mbali. Hii yote kumuepusha na kumlinda na mabaya. Mungu alifanya haya yote japo Kaini alikuwa na dhambi ya kumuuwa nduguye.

Mungu utazama tofauti, na macho ya binadamu. Na Mungu ndiye mwenye uweza wa kuhukumu. Siku hizi Tanzania hii kumezuka, tabia ambayo inaonesha watu kufurahia kifo au vifo vya watu wengine. Na kama walikuwa hawampendi huyo mtu au watu; ndo watazusha mengi. Wabaya wake watajifanya wao ni mungu (Mungu), watahukumu, watasema huyu alifanya mabaya ndo maana kafa.

Watajiona wao waliobaki ndo wajanja, hawana makosa au dhambi mbele ya Mungu. Najiuliza hivi kuna mahala popote pale iwe katika misaafu au maandiko yoyote ya kidini na imani zinginezo, pana sema mtu anae kufa mapema au kabla ya wenzie ana dhambi na Mungu kaamua kumkomoa?

Nachojua Mungu alisema tutakufa, hakuna atakaeishi milele hapa duniani. Ndo maana watu ufa wakiwa watoto wachanga, wakiwa vijana, wakiwa wazee, na hata watoto wengine ufia tumboni mwa mama zao kabla ya kuzaliwa.

Tukidai kufa mapema ni kukomolewa na Mungu, ebu tuangalie, hawa mitume wetu, walikufa bado wakiwa vijana, na walikuwa na maadui wengi, hawakupendwa. Yesu kristo aliishi miaka isiyozidi thelathini na tatu. Na alianza kazi ya kuhubiri akiwa na miaka thelathini tu. Vile vile kwa mtume Muhamad S.W.A alikufa mapema. Si hao tu ni wengi!

Hivyo kifo ni asili. Nachoamini kila mtu anakusudi la kuwepo duniani. Na pia ana muda wake wa kuishi. Haijalishi ni miaka mingapi. Muda ukifika Mungu ndo mwamuzi wa yote, uondoke au aseme bado ubaki.

Katika kila jambo Mungu anamakusudi yake. Laweza kuwa baya au zuri, lakini Mungu anatazama tofauti na tunavyotazama sisi wanadamu.

Kikubwa tusijipe kazi ya Mungu ikawa kazi yetu. Tusijipe kuhukumu kwani hukumu ya maisha yetu utolewa na Mungu. Usihukumu usije hukumiwa.

Nimeongea haya yote ni kutokana na watu wengi, wapinzani na wana CCM kuonekana kumhukumu alie kuwa Rais wa Tanzania, J.P. Magufuli na hata kumzodoa kuwa kafa mapema, yako wapi, kuonesha tu Mungu ati kamuondoa kwa mabaya yake. Nilishangaa hata Mchungaji mmoja anajiita mzee wa upako kuongea kama vile nae anaonesha kufa kwa magufuli ni kama adhabu, eti kisa Lowasa hakuchaguliwa Urais na kuwataka watu wakamuombe Msamaha Lowasa.

Mimi niseme kwa maandiko viongozi wote wakuu wa nchi uwekwa na Mungu. Mungu angeamua Lowasa kuwa Rais angekuwa tu. Mchungaji kasahau maandiko anatumia akili za kibinadamu. Kufa kwa Magufuli si kwamba Mungu hakutaka Magufuli awe Rais, la asha. Mungu hutenda kwa wakati wake.

Jiulize katika maandiko tunaambiwa kuwa Yusufu aliuzwa utumwani na nduguze, bado huyo Yusufu akafungwa gerezani. Lakini cha ajabu akaja kuwa ndiye waziri mkuu wa nchi. Hata nduguze walipojihisi atalipiza kisasi kwa kuwafanyia mabaya, aliwaambia. Mlikusudia mabaya kwangu, lakini katika hayo mabaya Mungu alikusudia mema ili nije niwaokoe katika baa la njaa.

Mungu uona mbali zaid ya binadamu. hatujui ni kwanini Mungu aliepusha Lowasa asiwe Rais japo ilitumika njia mbaya au nzuri, lakini Mungu anakuwa na makusudi yake. Mchungaji katafakari neno la Mungu ndo utoe tamko. Hakuna lifanyikalo duniani bila Mungu kuridhia. Mungu huyo aliruhusu Ayubu apate mateso, akaruhusu watoto wake Ayubu kufa na hata mali kuharibika na kupotea lakini alikuwa na kusudi. Kifo cha Magufuli kinakusudi liwe baya au zuri ila watanzania tutajifunza kutokana na hicho kifo siku moja. Kikubwa tusijichukulie mamlaka ya kuhukumu na kusema kafa kwa sababu alikuwa katiri na kadharika. Mbona Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji?

Hivi kazi yetu ni kuhukumu, kwani tuliobaki hatutakufa? wangapi tumefiwa na ndugu na wazazi, je kutangulia kwao ni kwamba walitenda mabaya Mungu kawahukumu? Kwa uzoefu wa haraka tu mara nyingi watu wema hawadumu? Iwapo hadi sasa unaishi lazima ujiulize, unatakiwa kulifanyia nini Taifa lako la Tanzania, na familia yako. Si kushambulia marehemu, na kujifanya wewe ni mungu unahukumu. Leo hata viongozi wetu utasikia, oooh! Magufuli hakutenda haki, alikuwa kiongozi mbaya, alikuwa muuwaji, alitisha, hakuwa na demokrasia!

Hivi ninyi viongozi mnao sema haya si mlikuwa nae ktk uongozi wa serikali? Kwanini amkumwambia wakati huo akiwa hai kuwa ni kiongozi mbaya.

Nacho jua Magufuli alikubali kukosolewa. Naibu Waziri wa afya kipindi hicho alimkosoa kuhusu matumizi ya kujifukiza. Akamwondoa katika nafasi. Lakini baadae alimrejesha ktk wizara tofauti.

Leo wanao mkosoa magufuli haohao, wanapinga Mhe. Rais Samia kukosolewa. Wakati Rais alidai kuwepo uhuru wa kukosoa. Lakini chama chake na Bunge Wanataka asikosolewe, tumsifie hata kwa yale yasio sifiwa. Wakati wanadai wao ni wanademokrasia. Ukikosoa unahesabika msaliti, Bunge litakuita kwenye Kamati. Chama kitakaa kukuita kikuhoji kwa nini huko kinyume na Rais. Chama kinachoongozwa na mwenyekiti ambae ni Rais alie ruhusu kokosolewa.

Mungu hapendi wafitini na watu waongo, wenye roho za usaliti. Viongozi mjitafakari. Na msijione ninyi hamta kufa. Kifo kipo akijali madaraka yako. Hakuna atakae ishi milele. Kuwepo kwako pengine Mungu anataka utimize mambo fulani. Ghazabu ya Mungu ni kubwa tusihukumu tukaja hukumiwa. Magufuli kaondoka kamaliza yake. Alifanya kwa nafasi yake na kwa staili yake. Watu wote hatufanani.

Tusijione sisi ni bora kwakuwa tu watu wanatuchekea na kutusifia. Tukachekelea na kuota kiburi kuona tuko sahihi na hatukosei! Pamoja na yote Magufuli aliwapenda watanzania. Hakuwahi kusema waondoke wakaishi Burundi.

Leo kauli hiyo inaongewa na kiongozi aliepewa dhamana na watanzania. Viongozi wamejiona wako juu ya sheria, wanauwezo wa kusema chochote. Viongozi wamekuwa na dharau. Wanajiona nchi ni yao. Hata wananchi kulalamika hawaoni haja ya kuomba msamaha.

Hata kiongozi wa nchi hawakanyi anawaacha je naye kafurahishwa na hayo maneno? Je kawatuma?
Harafu hawa hawa ndo wanasema watakuwa wapole na kuwabembeleza wananchi kuliko JPM ambaye kapewa mabaya yote.
Tukumbuke kutangulia kufa si dhambi. Na ukibakia si ujanja wa kufanya kutukana waliotangulia. Bali chukua muda wa kujitafakari.

Mungu alimlinda Kaini japo alikuwa muuwaji wa nduguye. Mungu ndiye mwenye kuhukumu. Na ndiye ajuaye mwisho wa maisha yetu. Jiulize hapo ulipo matendo uyafanyao ktk vificho au wazi, je ni mema? Je wewe ni msafi zaidi ya waliotangulia kufa?

Je, wajua kifo chako kitakuwaje? Lini utakufa? Je utakufa ukiwa na umri gani? Je alie kutangulia kafa akiwa na miaka mingapi?
Si ujanja wala umaarufu kutukana marehemu, au kutafuta umaarufu ati unajilinganisha na marehemu. Huyo kesha maliza wakati wake hayupo tena. Tuache kashfa hatujui kesho yetu. Tanzania ya leo imekuwa na siasa za kujipendekeza, sifa za kijinga, badala ya kufikiria maendeleo ya kweli. Walio tangulia tuwaache, tujenge nchi.
 
Chama chakavu vs chama chakavu

Dodoki refuu la kumsafisha marehemu la nn?

Kama alitenda mabaya atahukumiwa kwa maovu yake haina haja ya dodoki la kumsafisha marehemu

2015-2021 UCHUMI WA NCHI ULIKUWA HATIANI SANA KAMA S MUNGU SIJUI INGEKUWAJE

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Hakuna sehemu aliyosafishwa, na siko kusafisha, bali naongea wazi hakuna chuki ya marehemu duniani. Kujenga chuki kwa mtu alokufa nadhani ni kutokuwa na akili za kufikiri. Nimeongelea kifo chake na yasemwayo kwa hicho kifo. Sasa nimsafishe kwa nani?

Nyie ndo mtakao kufa vifo vya ajabu na vibaya! Wewe si Mungu kuhukumu!

Sasa nimtetee Magufuli kwani anagombea uRais. Soma uelewe mada chuki zako usikimbie na kuandika tofauti ya mada.

Napenda kukukumbusha utakufa pia, je umetafakari maisha yako?
 
Katika mifano yako usisahau kugusia na Ben sanane, Alphonse mawazo, Azory Gwanda, yule diwani wa CCM Kigoma, Akwilina Akwilin, list ndefu sana unaweza kuongezea mwenyewe. Usisahau pia Lissu aliyerudia njiani.
 
Katika mifano yako usisahau kugusia na Ben sanane, Alphonse mawazo, Azory Gwandu, yule diwani wa CCM Kigoma, Akwilina Akwilin, list ndefu sana unaweza kuongezea mwenyewe. Usisahau pia Lissu aliyerudia njiani.
Mada yangu haiongelei hao watu, naongelea mtu kuhukumiwa, je sisi binadamu tuna mamlaka ya kuhukumu? Hata kama mtu alifanya makosa? Soma uelewe mada usikurupuke. Ndo maana nikasema hata Kaini aliuwa kwanini Mungu bado alimlinda Kaini? Watu wengi ukurupuka wajui mada inachosema. Lakini pia hao unao wataja unaushahidi kuwa Magufuli aliwauwa? Mbona kumekuwa na tuhuma za Ben Sanane kuuwawa na Boss wake, Kumekuwa na tuhuma alie kuwa Makamu mwenyekiti wa Chadema kuuwawa na Mwenyekiti?

Lakini watu wangapi wamepoteza maisha nyakati za uongozi tofauti? Hii haiwezi kukufanya uhukumu. Anae hukumu ni Mungu pekee!
 
Hivi ile 'battalion' na 'mitambo' iliyokuwa inamlinda ili asife imehamishiwa wapi?
Kiongozi gani asie lindwa duniani? Hata weye mwenyewe unajilinda. Ila kifo cha mwenzio isiwe kicheko kwako! Kila mtu ana muda na saa yake! Wewe umejiuliza saa ngapi roho yako itatwaliwa, japo unalala kwa kufunga milango ya nyumba na geti juu! Nawe roho yako itaondoka!
 
Pote
Mwenzio unamwona shetani, je wewe Mungu anakuonaje? Umetafakari hilo! Je umewaza juu ya kufa kwako? Unajua roho yako itatwaliwa muda upi?
Potelea mbali sijaiba Cha mtu sijauwa mtu sijateka mtu sijafunga watu kwa kesi za uongo sijaikufuru Wala kuinajisi altare ya Mungu naamini mungu muumba wangu atanipa kifo Cha amani na cha heshima.
 
Kuna baadhi uliyoyasema ni ya kweli tupu, mengine hapana.

Kwa sisi tuliowaumini, kwa ufupi tunajua kuwa:

1) Maisha ya mwanadamu hupangwa na Mungu

2) Kiongpzi awe mbaya au mzuri, Mungu atakuwa ameruhusu, na mara nyingi kwa makusudi fulani

3) Kifo ni kwaajili ya kila mmoja

4) Kifo hakichagui umri

Ambayo hukuyasema:

1) Magufuli alikuwa ni mtawala mbaya sana. Kwa matendo ya kuua, kuteka na kubambikizia watu kesi, alijiweka karibu zaidi na upande ulio kinyume na Muumba wetu aliyetukataza sisi sote kuyatenda hayo aliyokuwa akiyatenda.

2) Mungu huweza kuruhusu hata mtu mbaya kuwa mtawala kwa makusudi yake. Mungu hashindwi kitu. Hachelewi wala hakawii bali hutenda kila jambo kwa wakati ufaao kwa kadiri ya hekima yake. Aliruhusu Yuda awe miongoni mwa wafuasi wa Yesu. Aliruhusu Herode ambaye aliua watoto wote wa kiume ambao umri wao ulikaribiana na umri wa Yesu, kuwa mtawala. Anaruhusu hata majambazi na wauaji waendelee kuishi, lakini haimaanishi kuwa wanampendeza. Bali huruhusu wawepo kwa makusudi maalum. Kuna wakati, mtawala mbaya huja kama adhabu kwa wanaoongozwa kwa sababu wamemsahau Mungu wa kweli. Au kutaka kudhihirisha ukuu wake na jinsi hekima yake ilivyo tofauti na ya mwanadamu. Aliruhusu Hitler na Musollini wawe watawala. **** wakati aliruhusu Taifa lake teule kuingia utumwani, na wakati mwingine kulitoa utumwani kwa mkono wake wenye nguvu.

3) Kifo hakiondoi haki ya watu kukusema iwe kwa mema au mabaya. Matendo mema au mabaya ni shule kwa sisi tunaoendelea kuishi. Ndiyoaana Yida anaendelea kusemwa mpaka leo. Herode anasemwa. Hitler anasemwa. musolini anasemwa.

4) Japo sisi sote mwisho wa maisha yetu hapa Duniani ni kifo, lakini ukweli kifo kilikuja kwetu wanadamu kama adhabu, siyo kama zawadi.7 Na hata kwa hekima ya mwanadamu, adhabu ya kifo ndiyo kubwa kuliko zote (japo mimi sioni kama kifo chenyewe ni adhabu ambayo mwanadamu anaweza kumpa mwanadamu mwenzake). Lakini Kristo alikibadilisha kifo kutoka kuwa adhabu na kuwa ndiyo njia ya kumwendea Mungu aliyetuumba ili tukatoe hesabu ya matendo yetu tulipoishi Duniani. "Kwangu, kuishi ni Kristo, na kufa ni faida zaidi. Lakini, kama kwa kuishi nitaweza kufanya kazi yenye faida zaidi, basi, sijui nichague lipi! Nakabiliwa na haya mawili yaliyo sawa. - Paulo"

5) Funzo tulilolipata kutokana na kifo cha huyu mwenzetu aliyekuwa na mamlaka makubwa ya kibinadamu ni kuwa hata ukiwa na cheo kikubwa kiasi gani, hata uwe na majeshi yenye nguvu kiasi gani, hata uwatishe wanadamu wenzako kiasi gani, bado wewe ni mwanadamu ambaye kuzaliwa kwako na kufa kwako hakuna tofauti ni mwingine yeyote, tuheshimu utu, uhai, haki na heshima ya wanadamu wenzetu. Tutambue pia, maisha yetu Duniani ni ya muda tu, kama huyu aliyeogopwa na akamtisha kila raia kutokana na utawala wake wa mkono wa chumaj, akalindwa kwa majeshi ya wazi na ya siri, mwenye uwezo wa kupata matibabu popote kwa gharama yoyote, ameondoka, sisi tuliobakia tuna nini cha pekee hata tuone tuna uwezo wa kuwadhulumu wanadamu wenzetu kwa vile tu pengine tuna mamlaka fulani, utajiri, n.k?

6) Tumgeukie Mungu, tumshukuru kwaajili ya maisha ya huyo mwenzetu maana kwa kupitia maisha ya huyo mwenzetu, tumejifunza mengi, meme na mabaya. Mabaya yake, yawe onyo kwetu, na mazuri yake tuyaishi.
 
Mungu aliona hatma ya taifa na ndio maana aliingilia Kati ; trust me angeongoza miaka kumi Kuna watu uzalendo ungewashinda na uvumilivu ungeisha watu wangeanza kukinukisha live na damu nyingi ingemwagika magufuli alikuwa analipeleka taifa ukingoni mwa uvumilivu wa kawaida.
Ndo haya nisemayo, kufa kwa mtu ni mpango wa Mungu, hata asingekuwa Rais angekufa. Nawe utakufa!
 
Kiongozi gani asie lindwa duniani? Hata weye mwenyewe unajilinda. Ila kifo cha mwenzio isiwe kicheko kwako! Kila mtu ana muda na saa yake! Wewe umejiuliza saa ngapi roho yako itatwaliwa, japo unalala kwa kufunga milango ya nyumba na geti juu! Nawe roho yako itaondoka!
Bado nasubiri majibu ya swali langu.
 
Back
Top Bottom