Haya ya Rufiji ni kuichokoza nchi

Lituye

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
1,863
5,694
Ndugu wana jamii kwanza siamini kama kuna mtanzania anashiriki uhalifu huu na Kama yupo basi ipo ajenda ya siri ambayo mizizi yake inaanzia nje ya nchi.

Jambo la MSINGI ni kuwa vita hii sio ya jeshi la polisi, ni vita yetu wote,hao watu wameipiga Tanzania, wanatuchokoza na kutaka kututisha kuzani kuwa tutatishika.

Fyoko fyoko hizi hazivumiliki, wahusika wote hamtakuwa salama, mkono wa sheria utawakumba. Mtashindana lakini hamtashinda, tutawapiga popote mlipo, uwezo tunao na sababu ipo, Watanzania ni wamoja ktk mambo ya MSINGI hatuta yumbishwa.

Vijana na RAIA wema wote huko rufiji lindeni uhuru na Amani ya taifa hili kwa ghara zote mkishirikiana na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.

Mkishindwa mjue mtabeba dhamana ya uhalifu huu mikononi mwenu na itawagharimu ninyi wenyewe na vizazi vyenu. Majuto ni mjukuu.
 
hawa ndugu zetu polisi wataendelea kuuwawa haiwezekani magaidi uwaite majambazi,hivi toka lini majambazi wakaa maporini tena vijijini tujuavyo majambazi hukaa mjini sikuzote na matukio yao ni ya kuiba bank,magari na uporaji

lakini kitendo cha kuendelea kuficha mambo ndio maana na wao wana-take advantage ya kufanya lolote
 
Wito kwa jeshi la polisi kuweni werevu sana kwenye jambo hili , Tafadhali sana msiwanyanyase wakazi wa eneo husika kwa jambo wasilohusika nalo , tafadhali sana .

Nimemsikia na kumuona Nsato Marijani akijiapiza , sikupenda style yake , wananchi wasikomolewe.
 
Umenena.zHakuna haja ya kumung'unya maneno.Mara ooh hatuwezi sema ni magaidi mara ooh, Igp tafadhari usifunike maneno.Hawa ni magaidi.Unapoingia uwanjani siyo unapambana na majambazi.Narudia tena.Hawa ni magaidi.Ingia uwanjani kupambana na magaidi.Mungu tunaomba majaaliwa.Tupe ulinzi wako.
 
Dah! Polisi Marijani ametoa vitisho vya kufa mtu
"acha maneno leta muziki"----Darasa
 
Wito kwa jeshi la polisi kuweni werevu sana kwenye jambo hili , Tafadhali sana msiwanyanyase wakazi wa eneo husika kwa jambo wasilohusika nalo , tafadhali sana .

Nimemsikia na kumuona Nsato Marijani akijiapiza , sikupenda style yake , wananchi wasikomolewe.
Angalizo zuri sana hilo mkuu,wakikaa vibaya wanaongeza uhasama na wananchi na zoezi la kuwapata wahusika litakua gumu sana mwishowe watakufa wasio husika ili tu kwenye vyombo vya habari ionekane kazi imefanyika.
 
Kusema ukweli imani ya polisi wetu kwa raiya wao ni ndogo sana,

Na kutufanya sisi ni wakoseaji na tunastahili kukomolewa kwa vyovyote watakavyo wao,

mimi kusema la ukweli sina urafiki na polisi wala sitaki urafiki kwani wamejaa roho ngumu na mbaya kwetu sisi,,

Tutakutana motoni na hao watu ila sio kuwaonea huruma kwa wanayokutana nayo.
 
Back
Top Bottom