Mindi
JF-Expert Member
- Apr 5, 2008
- 3,523
- 4,998
Rais Magufuli amezuia wapinzani wasiseme wala kukohoa. kazuia bunge live. alimwagiza Ndugai awashughulikie wabunge wa upinzani ndani ya Bunge na yeye atawashughulikia nje ya Bunge. Alipoona haitoshi kuzuia mikutano ya nje, sasa anadhibiti hata mikutano ya ndani.
Kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM, alihakikisha anapata ushindi wa asilimia mia moja. Sikumbuki katika enzi zake kama Nyerere au waliomfuatia, aliwahi kupata asilimia hizo. Tunajua kwamba kama angetaka, Nyerere angeweza KUJIPA kura asilimia 100, kama alivyofanya Magufuli.
Kwenye chaguzi za marudio ngazi za udiwani na ubunge, Magufuli alihakikisha CCM inashinda asilimia 100. mkuu wa mkoa ambaye mkoa wake alipita diwani mmoja wa CHADEMA, aliomba radhi kwa Magufuli. Zilifanyika figisu za kila aina. kama uchaguzi utaachwa ufanyike, basi atatangazwa mgombea wa CCM ameshinda, hata kama ameshindwa. mara nyingi figisu zilikuwa kwenye kuchukua na kurejesha fomu, kama ilivyokuwa jimbo la Korogwe, uchaguzi wa marudio.
Sasa hivi kuna magazeti mapya lukuki, baada ya kuona Uhuru na Daily News hayatoshi kuimba mapambio. kuna channel za TV mbalimblai: TBC, Channel Ten ambazo daima huimba mapambio ya mafanikio ya JPM, lakini sasa hata TV zingine tuseme zinapewa tenda kumtangaza JPM. na kwa kuwa siku zote nyimbo ni hizo hizo, hii tathmini ya miaka 4 ya kuimba mapambio ni kama inachosha tu maana yale yale yanarudiwa kila siku.
JPM anajitangaza mafanikio yake na wengi wanaimba sifa zake. lakini hiyo yote haitoshi. bado JPM amejipanga kupora uchaguzi wa Serikali za mitaa. Yaani mafanikio ya Magufuli hayatoshi kuwafanya watanzania wachague CCM, mpaka kuwe na wizi na uporaji wa kiwango hiki?
Aliwaita watendaji wa ngazi za chini kule Ikulu. hatujui walichoongea, ila matokeo tunayaona. Watu sijui wamekula bangi? yaani vituko vinavyofanyika nchi nzima ni aibu tupu. haijawahi kutokea hii. CCM ni wezi wa kura inajulikana tokea enzi na enzi. lakini siyo kwa kiwango hiki. kwamba wameagizwa toka juu, unaweza kuona pale Waziri Jafo anatoa amri vituo visifungwe, lakini hali ndio inakuwa mbaya zaidi. anasema watu wasienguliwe, waachwe wakataliwe kwenye kura, ndio kwanza figisu zinaongezeka. Tatizo hasa ni nini?
Tatizo ni maradhi ya JPM: anataka daima kusifiwa, daima aonekane kwamba yeye ndiyo yeye. kama ni uchaguzi anashinda asilimia 100, kwa gharama yoyote ile. matokeo yake analiingiza taifa zima katika maradhi. gharama ya matibabu ya kuliponya taifa inazidi kuongezeka. siku Magufuli akiondoka madarakani, sijui tutakuwa wagonjwa kiasi gani kama taifa. wengi wanaamini miradi anayoianzisha magufuli ndio fidia ya figisu zake. Binadamu anahitaji sana uhuru wake, hata kama unamfuga kama kuku na kumlisha vizuri.
lakini hata chama chake ndio kabisaaa kinakufa kama chama cha siasa. CCM