Haya sasa ni Maradhi ya Rais Magufuli

Haya sasa ni Maradhi ya Rais Magufuli

Rais Magufuli amezuia wapinzani wasiseme wala kukohoa. kazuia bunge live. alimwagiza Ndugai awashughulikie wabunge wa upinzani ndani ya Bunge na yeye atawashughulikia nje ya Bunge. Alipoona haitoshi kuzuia mikutano ya nje, sasa anadhibiti hata mikutano ya ndani.

Kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM, alihakikisha anapata ushindi wa asilimia mia moja. Sikumbuki katika enzi zake kama Nyerere au waliomfuatia, aliwahi kupata asilimia hizo. Tunajua kwamba kama angetaka, Nyerere angeweza KUJIPA kura asilimia 100, kama alivyofanya Magufuli.

Kwenye chaguzi za marudio ngazi za udiwani na ubunge, Magufuli alihakikisha CCM inashinda asilimia 100. mkuu wa mkoa ambaye mkoa wake alipita diwani mmoja wa CHADEMA, aliomba radhi kwa Magufuli. Zilifanyika figisu za kila aina. kama uchaguzi utaachwa ufanyike, basi atatangazwa mgombea wa CCM ameshinda, hata kama ameshindwa. mara nyingi figisu zilikuwa kwenye kuchukua na kurejesha fomu, kama ilivyokuwa jimbo la Korogwe, uchaguzi wa marudio.

Sasa hivi kuna magazeti mapya lukuki, baada ya kuona Uhuru na Daily News hayatoshi kuimba mapambio. kuna channel za TV mbalimblai: TBC, Channel Ten ambazo daima huimba mapambio ya mafanikio ya JPM, lakini sasa hata TV zingine tuseme zinapewa tenda kumtangaza JPM. na kwa kuwa siku zote nyimbo ni hizo hizo, hii tathmini ya miaka 4 ya kuimba mapambio ni kama inachosha tu maana yale yale yanarudiwa kila siku.

JPM anajitangaza mafanikio yake na wengi wanaimba sifa zake. lakini hiyo yote haitoshi. bado JPM amejipanga kupora uchaguzi wa Serikali za mitaa. Yaani mafanikio ya Magufuli hayatoshi kuwafanya watanzania wachague CCM, mpaka kuwe na wizi na uporaji wa kiwango hiki?

Aliwaita watendaji wa ngazi za chini kule Ikulu. hatujui walichoongea, ila matokeo tunayaona. Watu sijui wamekula bangi? yaani vituko vinavyofanyika nchi nzima ni aibu tupu. haijawahi kutokea hii. CCM ni wezi wa kura inajulikana tokea enzi na enzi. lakini siyo kwa kiwango hiki. kwamba wameagizwa toka juu, unaweza kuona pale Waziri Jafo anatoa amri vituo visifungwe, lakini hali ndio inakuwa mbaya zaidi. anasema watu wasienguliwe, waachwe wakataliwe kwenye kura, ndio kwanza figisu zinaongezeka. Tatizo hasa ni nini?

Tatizo ni maradhi ya JPM: anataka daima kusifiwa, daima aonekane kwamba yeye ndiyo yeye. kama ni uchaguzi anashinda asilimia 100, kwa gharama yoyote ile. matokeo yake analiingiza taifa zima katika maradhi. gharama ya matibabu ya kuliponya taifa inazidi kuongezeka. siku Magufuli akiondoka madarakani, sijui tutakuwa wagonjwa kiasi gani kama taifa. wengi wanaamini miradi anayoianzisha magufuli ndio fidia ya figisu zake. Binadamu anahitaji sana uhuru wake, hata kama unamfuga kama kuku na kumlisha vizuri.

lakini hata chama chake ndio kabisaaa kinakufa kama chama cha siasa. CCM
Watu wakija kugundua na kuamini kuwa huyu anastahili kuwa Mirembe kitandani taifa litakuwa limeishabomoka
 
kupata 100% kwenye uchaguzi ni jambo la kawaida sana. Kama kumbukumbu zako ziko sawa Lowasa 2015 alipitishwa kwa asilimia ngapi na mkutano mkuu Wa CHADEMA kuwa mgombea urais?

Magufuli ni kiongozi wetu sote ,wa Tanzania nzima. kila jambo linamhusu yeye ni habari, taarifa ama tukio la kitaifa. Kama hayo Magazeti na vituo vya runinga vinatutaarifu juu ya matukio na mafanikio ya Rais wetu kuna tatizo gani ? Kama huitaki TBC au nipashe kuna tanzaniadaima kasome hilo

Rais Magufuli licha ya kwamba ni mkuu Wa nchi na serikali pia ni mwenyekiti Wa CCM taifa hivyo atahahakisha CCM inashinda kwa 100% ndani ya siasa kwa kuwa ataulizwa sababu za kushindwa , hilo likumbuke. Kushinda kwa CCM kusihusishwe na mamlaka akiyonayo Rais kama amri jeshi bali kama mwenyekiti Wa CCM
Magufuli alisha jidefine vizuri sana na wala hakulazimishwa alisema yeye ni kichaa na kweli ni kichaa mwenyekiti wa chama kinachotawala atafanyaje mambo ya kijinga nakipumbavu namna hii
 
Mimi hapo niko kundi gani? Mbona watz wengi hawampendi jiwe
Wanaomchukia jpm ni hawa

1/ wenye vyeti feki

2/mafisadi

3/ wauza madawa ya kulevya

4/walishindwa kwenye uchaguzi 2015

5/makuwadi wa mafisadi na mabeberu

6/wanaofanya siasa za kuchumia tumbo

State agent
 
Wanaotaka wafie kwenye uwenyekiti wa chama, wakisema wanakubalika
kwa hiyo kwa akili yako ya kiroboto Magufuli anakubalika mbona ameshindwamiko yote hata ya kanda ya ziwa anakolingia hawatakihata kumsikia yaani wamemgomea mwenyekiti mshamba hata fomu hawakujishughulisha kuchua mwenyekiti uchwara anafoka foka tu lakini hopeless
 
Duu imenikumbusha utajiri wa madawa kweli jamaa kafanikiwa kuwa na pesa nyingi lakini AMANI hana kabisa
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu
Wote tunampenda isipokuwa hatuzipendi kazi za kiibilisi anazozifanya tunataka aongeze bidii katika yale mazuri anayoyafanya, ya bilisi amuachie ibilisi na wafuasi wake, hatutaki tuwe watumwa wa kupongeza kila kitu kama mazuzu wa lumumba.
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu

Kama ni hivyo figisu za nini kwenye uchaguzi wa serekali za mitaa
 
Usitusemee Watanzania wote,mm ni mtanzania na ninampenda, sema BAADHI YA WATANZANIA ndio hawampendi FULL STOP
Watanzania hatumpendi fullstop. Orodhesha list utakayo lakini habari ndio hiyo.
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu
Wanaomchukia jpm ni hawa

1/ wenye vyeti feki
2/mafisadi
3/ wauza madawa ya kulevya
4/walishindwa kwenye uchaguzi 2015
5/makuwadi wa mafisadi na mabeberu
6/wanaofanya siasa za kuchumia tumbo
State agent

The terrible twins wako kazini hapa. Nami naongezea "Wanaomchukia JPM ni wale wapenda DEMOKRASIA na UTAWALA bora wa vyama vingi"
 
Sometimes ni busara sana kuficha upumbavu kwenye mijadala ya ishu sensitive kama hii.
Kama Serikali ya awamu hii imefanya mengi mazuri kama yanavyoandikwa na kusifiwa (yapo ndio), kwa nini wanaogopa kukosolewa ama kuacha uchaguzi uwe huru bila figisu? Kwa ninj wamewakata mpaka wana ccm ambao wanakubalika ktk jamii?
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli,hao wachache wanajiangaisha tu
 
Rais Magufuli amezuia wapinzani wasiseme wala kukohoa. kazuia bunge live. alimwagiza Ndugai awashughulikie wabunge wa upinzani ndani ya Bunge na yeye atawashughulikia nje ya Bunge. Alipoona haitoshi kuzuia mikutano ya nje, sasa anadhibiti hata mikutano ya ndani.

Kwenye uchaguzi wa Mwenyekiti wa CCM, alihakikisha anapata ushindi wa asilimia mia moja. Sikumbuki katika enzi zake kama Nyerere au waliomfuatia, aliwahi kupata asilimia hizo. Tunajua kwamba kama angetaka, Nyerere angeweza KUJIPA kura asilimia 100, kama alivyofanya Magufuli.

Kwenye chaguzi za marudio ngazi za udiwani na ubunge, Magufuli alihakikisha CCM inashinda asilimia 100. mkuu wa mkoa ambaye mkoa wake alipita diwani mmoja wa CHADEMA, aliomba radhi kwa Magufuli. Zilifanyika figisu za kila aina. kama uchaguzi utaachwa ufanyike, basi atatangazwa mgombea wa CCM ameshinda, hata kama ameshindwa. mara nyingi figisu zilikuwa kwenye kuchukua na kurejesha fomu, kama ilivyokuwa jimbo la Korogwe, uchaguzi wa marudio.

Sasa hivi kuna magazeti mapya lukuki, baada ya kuona Uhuru na Daily News hayatoshi kuimba mapambio. kuna channel za TV mbalimblai: TBC, Channel Ten ambazo daima huimba mapambio ya mafanikio ya JPM, lakini sasa hata TV zingine tuseme zinapewa tenda kumtangaza JPM. na kwa kuwa siku zote nyimbo ni hizo hizo, hii tathmini ya miaka 4 ya kuimba mapambio ni kama inachosha tu maana yale yale yanarudiwa kila siku.

JPM anajitangaza mafanikio yake na wengi wanaimba sifa zake. lakini hiyo yote haitoshi. bado JPM amejipanga kupora uchaguzi wa Serikali za mitaa. Yaani mafanikio ya Magufuli hayatoshi kuwafanya watanzania wachague CCM, mpaka kuwe na wizi na uporaji wa kiwango hiki?

Aliwaita watendaji wa ngazi za chini kule Ikulu. hatujui walichoongea, ila matokeo tunayaona. Watu sijui wamekula bangi? yaani vituko vinavyofanyika nchi nzima ni aibu tupu. haijawahi kutokea hii. CCM ni wezi wa kura inajulikana tokea enzi na enzi. lakini siyo kwa kiwango hiki. kwamba wameagizwa toka juu, unaweza kuona pale Waziri Jafo anatoa amri vituo visifungwe, lakini hali ndio inakuwa mbaya zaidi. anasema watu wasienguliwe, waachwe wakataliwe kwenye kura, ndio kwanza figisu zinaongezeka. Tatizo hasa ni nini?

Tatizo ni maradhi ya JPM: anataka daima kusifiwa, daima aonekane kwamba yeye ndiyo yeye. kama ni uchaguzi anashinda asilimia 100, kwa gharama yoyote ile. matokeo yake analiingiza taifa zima katika maradhi. gharama ya matibabu ya kuliponya taifa inazidi kuongezeka. siku Magufuli akiondoka madarakani, sijui tutakuwa wagonjwa kiasi gani kama taifa. wengi wanaamini miradi anayoianzisha magufuli ndio fidia ya figisu zake. Binadamu anahitaji sana uhuru wake, hata kama unamfuga kama kuku na kumlisha vizuri.

lakini hata chama chake ndio kabisaaa kinakufa kama chama cha siasa. CCM
Hahahahaha jomba naona hizi ndotp za alinacha ndizo unazoziota Sasa...Kuna tatizo gani kwa wananchi kuelewa au kujua Nini Magufuli anafanya na serikali yake...ni muhimu Sana wanachi wakajua ili msije kuwaongopea wakati wa kampeni
 
Back
Top Bottom