Haya ndio mambo ya Simiyu.

Kiba

JF-Expert Member
Mar 23, 2012
459
62
Ukifika katika mkoa wa Simiyu utapokelewa kwenye magari kwa sauti nzuri za watoto wakukukaribisha ununue aidha karanga au mahindi yakuchemsha.

Katika mikoa ya kanda ya ziwa wasukuma endapo mtu ni mganga na anataka kwenda kuanzisha maisha mapya sehemu nyingine mtu huyo huenda tu na pale mizimu yake itamtuma ajenge basi mara moja huanza kujenga pasipo kujua kiwanja ni cha nani.

Nilifanikiwa kufika katika kijiji cha Itongo ktk wilaya ya Busega na kukuta mkutano wa kijiji.

Mkutano huo ulikua na ajenda mbili ya kwanza uchawi umezidi kijijini hapo na ya pili ametokea mganga toka Bariadi na majini yake yamemtuma kuishi hapo hivyo viongozi wanaomba wanakijiji wachange feda ili kumjengea nyumba mganga huyo.


Sasa wandugu je haya yanatokea katika vijiji vingine.
 
Back
Top Bottom