Haya ndio mambo Muhimu ili uwe muigizaji mzuri wa Filamu

Edwardo Ommy

Member
Feb 6, 2020
36
52
Ni swali ambalo mara nyingi naulizwa sana na watu wanaogiza au wenye matamanio ya kuigiza. Jibu langu huwa ni ndefu na linaloshirikisha sekta nyingi sana za filamu. Secta zenyewe ni kama uandishi(miswada na utunzi wa stori), uongozaji(directing), upigaji picha, utayarishaji(production) na muigizaji mwenyewe.

Ili wewe uweze kuigiza vizuri na ukavutia watazamaji sio kazi yako pekee tu,bali ni kazi ambayo inahitaji msaada kutoka kwa timu ya filamu na ngazi zake zote kama zilivyotajwa hapo juu. Labda tuone jinsi ambavyo ngazi hizi zinasaidia kukufanya uwe muigizaji mzuri.

1. UANDISHI.

PicsArt_1417781657437 Hii ni kazi ya mtunzi wa stori na mwandishi wa muswada wa filamu. Story lazima iwe ya kibunifu inayoeleweka,inapomfikia mwandishi wa muswada aiandike katika namna ambayo inatafsirika vizuri katika lugha ya sauti na picha. Wewe muandishi inapendeza ukaandika muswada unaotoa nafasi ya waigizaji kuonesha uwezo wao halisi, hapa ina maana huzuiwi kimawazo,lakini andika muswada ukifikiria utofauti wa kiuwezo wa watu/waigizaji, mfano unaweza kuandika mahojiano lakini ukilenga uwezo tofauti wa kukariri wa wasanii wako,hii ni kusema kuna mazungumzo ambayo utalenga msanii mwenye uwezo wa kukariri mistari mirefu zaidi wakati mistari ya wahusika wengine ikiwa labda mifupi/michache zaidi. Au unawez kuumba dialojia ya kitaalam huku ukilenga kuonesha uwezo wa muigizaji katika kuongea maneno na facts za kitaalam. Unaweza fanya hivyo hivyo huku ukiilenga tofauti za kiuwezo kwenye jamii.

2. TIMU YA UCHAGUZI WAIGIZAJI
Hii timu ni ya pili katika kung’arisha uzuri wa msanii, kwa lugha ngeni tunaweza kuiita ‘casting team’. Muswada unapochaguliwa, basi hii timu inakaa ili kuchagua waigizaji watakao faa kuzijaza nafasi zilizoumbwa na waandishi wa muswada na stori. Ni vyema msanii anayechaguliwa katika uhusika Fulani awe kweli mwenye uwezo wa kuicheza nafasi hiyo na sio uchaguzi ufanyike kutegemea sababu dhoofu, kazi ya kuvaa uhusika inakuwa rahisi na yakufaa pale ambapo muigizaji na ule uhusika unashabihiana,lengo ni kufanya acting to be seen rather natural,mfano ni vigumu kwa muigizaji mwenye hulka ya upole kucheza kama pasua kichwa,mbea na tabia zingine ambazo ama haziendani na muonekano wake au hulka yake. Nashuri uchanguzi wa kisaikolojia na kihulka kutumika katika upendekezaji wa waigizaji katika kuvaa uhusika stori flani.

3. UNGOZAJI WA FILAMU
Hii hasa ni kazi ya director, pia napenda kusema ni mtu mwenye kazi ngumu katika ufanikishaji wa filamu. Director anaesoma stori na muswada vyema, mapema na kuelewa kwa kutoa utata katika fikra za mwandishi kwa kuwasiliana nae anakua katika nafasi ya kutayarisha namna nyingi za ufanikisha wa scenes za filamu bila kulipoteza lengo la filamu husika. Pale scene inapokua ngumu kuchezeka basi anakua na namna tofauti za kurahisishia msanii na ujumbe lengwa kutolewa. Director elewa wasanii wako kiasi cha kujua mapungufu yao na uwezo wao itasaidia kumchezesha scene vizuri msaniii wako.

4. UPIGAJI PICHA
camera
Huwa napenda kusema,camera ni mojawapo ya msanii,japo sijajua bado niite ‘Actor’ au ‘Actress’!. Camera ina nafasi yake katika kuelezea stori sio kila kitu msanii,tuwape nafasi ya kupumzika kwenye kioo, kuna scene zingine napenda kuziita akward scenes. Mfano wa namna ambavyo kamera inaweza kutumika kueleza stori,mfano;

1.NJE. NYUMBA AISHA – USIKU
Tunaona bwana kikwesha akigonga mlango wa aisha, baada ya muda aisha anafungua na Bwana kikwesha anaingia kwa wasiwasi huku akiangalia nyumba kwa woga. Mlango unafungwa. Kisha tunaona nyumba nzima kwambali na tunaona kupitia dirishani taa moja moja zikizimwa hadi numba nzima kwa mbali tunaiona giza.
FADE TO BLACK:

camera shots

Kwenye mfano huu wa script story inaelezeka japo hakuna muigiza aliyeongea wala kutumia ujuzi mwingi wa kuigiza. Stori hapa inaeleweka mwanaume ameingia kwenye nyumba isiyo yake na kulala huko usiku mzima.
 
Jambo jema sana.

Ila bongo movie kigezo kikuu cha uigizaji lazima uwe na takle kwa wadada kwa wakaka lazima uwe shombe shombe au mlamba lips.

The rest bora liende.

#MaendeleoHayanaChama
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom