Haya mahesabu ya Wazungu dhidi ya Urusi ni hatari

mtarimbo

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
423
1,019
Hawa jamaa leo wanataka kufanya jambo la kihistoria yaani kumwingiza Ukraine kwenye umoja wa Ulaya kama V.I.P membership wiki hii, kumbuka kuwa membership huchukua had miaka 5, hivyo Ukraine anapita directly bila mlolongo.

Kwa nini wanafanya hivi? Nia kubwa ni kutaka kuingia kumchapa mrussi direct, hili liko wazi kabisa, Mrusi anatafutwa akae kwenye Target.

Tuombe sana Mungu moyo wa Putin ashushe ghadhab dhid ya Ukraine maana itakua vita ya kihistoria.

Kumbuka Mkuu wa Majeshi wa Uingereza alitangaza majuzi kuwa ni wakati wa Ulaya kujiandaa kwa vita.

Mungu atusaidie tu maana tunawategemea sana Urusi na Ukraine kwa chakula na nishati.
 

Aleyn

JF-Expert Member
Nov 12, 2011
14,784
23,369
Hivi unadhani nchi gani ya EU Iko tayari kurisk kuwa kwenye vita na Urusi?
Hilo jambo haliwezi kutokea na litapingwa na member states wengi!
Tofauti ya Ulaya na mabara mengine ni kuwa, wao wanaongozwa na taasisi/systems. Uwe mbunge, uwe rais au uwe nani ni lazima ufate kile kilichopangwa.

Hakuna wa kuja kuzuia hili, kama kwa sasa ajenda ni kupambana na putin, basi kiongozi yoyote lazima aendane na ajenda hiyo.
 

4by94

JF-Expert Member
Oct 1, 2019
2,636
1,633
Hapo ni Mmarekan na Muingereza ndo wanaoratibu hayo mambo! Mtu kama Mfaransa sidhan kama ana nia hakufanya hayo mambo.
Soma historia kijana, Wakubwa wa Ulaya huwa hawaikubali Urusi tangu enz na enz km Tz tusivyokubalika East Africa sabab ya kutotaka kucopy with others, Urusi ndo taifa pekee balani Ulaya lenye akili za Ki Asia (udikteta na utawala wa mabavu usiojali nin wananch wanataka, nguvu ya dola ipo mikononi mwa mtu mmoja, ona UK juz walikuwa wana mchallange Boris ila Bunge la Urusi halina kauli dhidi ya Putin, hiki ndo Mabeberu hawakitaki)
 

Bukyanagandi

JF-Expert Member
Jun 24, 2009
9,267
9,044
Hivi unadhani nchi gani ya EU Iko tayari kurisk kuwa kwenye vita na Urusi?
Hilo jambo haliwezi kutokea na litapingwa na member states wengi!
Mkuu, si nchi za EU tu ambazo haziwezi ku-risk kuingia vitani na Urusi, hata Amerika haina ubavu wa kuingia vitani moja kwa moja na Urusi - they know military capabilities of them Russians should they decide to unleash their formidable weapons/missiles which western nations have no capabilities of intercepting them!!
 

Bome-e

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
14,872
18,368
Tofauti ya Ulaya na mabara mengine ni kuwa, wao wanaongozwa na taasisi/systems. Uwe mbunge, uwe rais au uwe nani ni lazima ufate kile kilichopangwa.

Hakuna wa kuja kuzuia hili, kama kwa sasa ajenda ni kupambana na putin, basi kiongozi yoyote lazima aendane na ajenda hiyo.
Sio kweli,kila nchi Ina haki ya kuwa na msimamo wake!Ndio maana unaona Turkey huko NATO anavyowatoa kamasi juu ya kupiga kura ya hapana Kwa Fins na Sweden kujiunga NATO!

Mfano Kwa upande wa NATO, moja ya kanuni za kujiunga ni kuwa hutakiwi kuwa vitani. Sijui kuhusu EU,ila hata Ukraine akiwa mwanachama leo, hatakuwa na haki ya kulindwa kijeshi na EU members!
 

mathewa

JF-Expert Member
Sep 5, 2012
744
1,097
Mkuu, nani kakuambia kuwa ulaya wana jeshi la pamoja?
Huyo ukraine hata hakuingia EU hakuna watakachofanya katika vita inayoendelea

EU wameshikiwa akili zao na Marekani. Ndo maana Marekani hawezi kuruhusu ulaya kuwa na jeshi lao. Ni hatari kwa usalama wa Marekani.

Wao wataendelea kuburuzwa ndani ya NATO tu.

Labda angejiunga na NATO ndo ingekuwa na madhara katika operation hii.

Hata hivyo kilichofanyika sio kupewa VIP membership, yeye amepewa hadhi ya kugombea kuwa mwanachama, atapitia mchakato wote wa kuwa mwanachama wa EU. ambao utachukua muda mrefu.

Ni kama mwenzake Uturuki ambaye mpaka leo bado hajaidhinishwa kuwa mwanachama
 

Mhandisi Mzalendo

JF-Expert Member
Aug 23, 2010
5,357
7,032
Hawa jamaa leo wanataka kufanya jambo la kihistoria yaani kumwingiza Ukraine kwenye umoja wa ulaya kama V.I.P membership, kumbuka kuwa membership huchukua had miaka 5, hivyo Ukraine anapita directly bila mlolongo...
Mleta mada tofautisha kati ya EU na NATO...

EU haina jeshi la pamoja hapo ni masuala ya kiuchumi na kijamii. Member wa EU wanajitegemea kila mmoja na jeshi lake.

NATO ndio wana jeshi ambalo ni baadhi ya nchi za ulaya pamoja na marekani.

So hakuna kitisho kwa usalama wa Russia kwa Ukraine kujiunga EU.

Na kumbuka kwenye EU mmoja wa superpower alishajitoa. Muingereza.

Nakushauri FUTA huu uzi.
 

Champagnee

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
8,608
17,709
Mkuu Ulaya wakiamua wameamua maana hawana namna, wako hatarin mruss akimalizana na Ukraine ulaya itakua haina ushawishi wowote na si ulaya tuu hata Marekani.

Mzee kama EU wamechoka kuishi au wameichoka dunia bhs wajidanganye kuingia vitani na Russia nahis watoto wetu kwenye history watakua wanafundishwa kulikua na bara linaitwa ulaya”

Hakuna nchi Ulaya inayoweza pigana na Russia direct hata US mwenyewe hana huo ubavu. Mnajua wengi mmedanganywa na propaganda za west kuhusu majeshi yao ila kiuhalisia ni kawaida sana.

Wengi wenu humu mmeanza kuijua Russia wakati wa kipindi hiki cha mgogoro na Ukraine.

VITA PEKEE EU WANAYOWEZA NI VIKWAZO.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

24 Reactions
Reply
Top Bottom