Detective J
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 30,313
- 54,841
Umesahau kundi moja ambalo huwa mnalifumbia macho. Lile kundi la wanaomkosoa kwa nia njema.. wanakosoa ili kujaribu kumfumbua rais macho. Na hawa idadi yao inaongezeka zaidi.
Sasa ww umecomment kisiasa sana, si kila anae kosoa ni mpinzan, ni team lowassa sijui membe.. sijui ana maslahi gani... wengine vyama hatuna wala hatuma interest.. lakin hatuachi kumkosoa ili atoke usingizini.
Sasa ww umecomment kisiasa sana, si kila anae kosoa ni mpinzan, ni team lowassa sijui membe.. sijui ana maslahi gani... wengine vyama hatuna wala hatuma interest.. lakin hatuachi kumkosoa ili atoke usingizini.
nimefanya kautafiti kadogo wanaompinga JPM wapo katika makundi kadhaa
Kwanza kuna wale walikuwa kwenye team Membe na team lowassa ndani ya CCM hawampendi JPM
Pili ni kundi la wafanyabiashara ambao kutokana na utawala kuwa dhaifu Tanzania waliitumia kama mtaji.........(Yaani unaweza ukaja Tanzania ukafanya lolote lile kwenye biashara)
Tatu ni kundi wa watumishi waliotumbuliwa na waliokatiwa mirija ya upigaji serikalini (Mfano kuondoa pesa za miradi ya serikali kwenye mabenki, kuhakikisha mapato yote ya serikali yanakusanywa kwa kutumia EFD machines, kufanyia kazi baadhi ya mapendekezo ya reports za CAG; kuzuia wana siasa kukopa kwenye benki kuu nakadharika
Pia Magufuli anachukiwa na watu kutoka nje pia nao wanatokana na sababu zifuatazo
kwanza kwa kuzuia tuu usafirishaji wa mchanga wa makinikia share za ACACIA zimeshuka kwenye london stock exchange.......unadhani watampigia makofi kumpongeza
Pili kwa kuweka ukuta mererani na kudhibiti utoroshwaji wa Tanzanite kuna viwanda India vimefungwa maana havina malighafi ya Tanzanite
Tatu kwa kuwabomoa walanguzi wa korosho/ kuzuia fedha za export levy ambazo zilikuwa zinaishia kwa wanasiasa wachache/ kubana kangomba na kuzuia raw materials ya korosho kwenda nje kuna watu wengi walikuwa wakifaidia na sasa mirija imekatwa
Mkuu haya ni baadhi tuu.....ila kwa wenye akili nadhani 2020 ni Magufuli tuu.........Maana walizoea kula vya bure