Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 10,886
- 2,766
Ukweli ni kwamba tangu nizaliwe hadi sasa naelekea utu uzima wenyewe sijawahi ona haya machungwa. Nachojua machungwa aidha yawe matamu au machachu, ila hayakosi maji. Sasa haya sijui ya wapi. Na ni mwaka jana na huu tu ndio nimeanza kuyaona.
Chungwa kwanza kubwa, halafu gumu, kuonyesha kabisa lina walakini. Nanunua machungwa matano na yote nakatakata na kuyatupa. Naambulia hapo vimajimaji kiasi, na nyama ya chungwa iliyobakia ni ngumu, mbichi na isiyo na maji. Yanatoka wapi? Kwa nini yanakuwa hivyo? Au nayo yanapepewa kama ndizi?
Yani tunapigwa kila kona. Tikiti, ndizi, sasa machungwa, mbogamboga. Kwa nini haya machungwa wasiyaache hadi msimu wake?