Haya maamuzi ni kujenga au kubomoa?

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,111
115,906
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?

Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..

je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?

Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?

walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....

kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?

kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?

na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?
 
Kuhusu Elimu ni swala gumu kidogo lkn hili la kufunga Biashara siyo gumu kwani kwa kawaida ukiona mtu kafungiwa Biashara yake ujue hiyo ni hatua ya mwisho kabisa kuchukuliwa na Serikali, kuna watu wanadaiwa kwa zaidi ya miaka 10 na siku zote wamekuwa wakionywa na kuandikiwa barua lkn bado hawajali sasa ulitegemea nini kifanyike tena zaidi ya hapo?
Sidhani kama kuna duka la mtu au biashara iliyofungiwa kwa sababu ya tu ameshindwa kulipa kodi ya mwezi/mwaka 1 tu na kwamba hilo lilikuwa ni onyo la kwanza, sidhani kama kuna kitu kama hicho, mara nyingi ni ukaidi wa muda mrefu!
 
Kuna tatizo kubwa tatizo tunafikiri unapomfungia mtu office ndio njia ya kutatua tatizo wakati huyo mtu alikuwa amewaajiri wananchi waliompigia kura Rais akawa hapo alipo ,alafu leo hii Ajira ya yule mtu inakufa yeye moja kwa moja anaanza kuilaumu Serikali.
Tungetengeneza kwanza sheria ya kuwadhibiti kuanzia sasa kodi ilipwe ndani ya mwaka mmoja.
Kwa sababu tulifanya uzembe uko nyuma hata kuna wakandarasi nasika hawajawai kulipa kodi kuanzia miaka 5 iliyopita.
 
Siku zote kujali ajira za watu inapaswa kuwa kipaumbele
sio tu kufilisi tu ili mradi sheria zifuatwe
 
Kuhusu Elimu ni swala gumu kidogo lkn hili la kufunga Biashara siyo gumu kwani kwa kawaida ukiona mtu kafungiwa Biashara yake ujue hiyo ni hatua ya mwisho kabisa kuchukuliwa na Serikali, kuna watu wanadaiwa kwa zaidi ya miaka 10 na siku zote wamkuwa wakionywa na kuandikiwa barua lkn bado hawajali sasa ulitegemea nini kifanyike tena zaidi ya hapo?
Sidhani kama kuna duka la mtu au biashara iliyofungiwa kwa sababu ya tu ameshindwa kulipa kodi ya mwezi/mwaka 1 tu na kwamba hilo lilikuwa ni onyo la kwanza, sidhani kama kuna kitu kama hicho, mara nyingi ni ukaidi wa muda mrefu!

Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....
 
Crime haina expire date, sometimes muhusika anaweza kuwa ame move on but ikigundulika lazima awajibike, huenda aliziba nafasi ya mtu mwingine ambaye kwa kukosa stahili yake haku recover hadi leo.
 
Ujanja ujanja huu walioutumia kupata hivyo vyeti ndio unaolifilisi hili taifa!Tena ni hatari kwa Prof. kuwa na vyeti feki maana kuna uwezekano mkubwa kwamba hata tafiti zake nyingi alifeki ili afike hapo! Tuite spedi spedi, tuache kutetea upuuzi!
 
Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....

Ndiyo maana nimesema hili la Elimu ni swala gumu, kwa maana hapa unaongelea udanganyifu, hivyo basi kama umedanganya umefanya kosa ina maana unapaswa kuadhibiwa na haijalishi wewe ni nani au una wadhifa gani!

Nitakupa mfano, kuna Waziri wa Ulinzi wa nchi moja barani Ulaya aliondolewa kwenye wadhifa wake kwa sababu walikuja kugundua kwamba kwenye PhD thesis yake alinakiri kazi ya watu wengine, hali iliyopelekea Chuo Kikuu alichosomea kumvua Shahada yake ya PhD ingawaje ni miaka mingi ilipita na yeye alikuwa tayari amefikia ngazi ya Uwaziri na baada ya hapo Serikali ya nchi yake nayo ikamvua Uwaziri kwa sababu ya udanganyifu alioufanya zaidi ya miaka 10 iliyopita!

Ni kama vile kwa mfano Raisi wa USA Obama (sijui kama mfano unaendana), kuna wanaosema kwamba hajazaliwa USA na kwamba aligushi cheti cha kuzaliwa, sasa Je kama ingekuwa tuseme wanaosema hivyo wako sahihi na ikathibitishwa kabisa kwamba ni kweli hakuzaliwa USA na kwamba aligushi cheti cha kuzaliwa unafikiri nini kingetokea? Unafikiri Obama angeachwa aendelee na Uraisi wake kwa sababu ni miaka mingi iliyopita au wangemu impeach?
 
hiyo mimi naifananisha na mtu aliyejenga mabondeni alafu tanesco wakamuekea umeme, idara ya maji ikamuekea maji na akafungua duka,watu wa biashara wakampa liseni lakini kosa likawa la mjengaji nyumba hao wengine waliopeleka uduma sehemu isiyohusika hawaangaliwi. kichekesho kikubwa. ndio maana nilisema miaka hii mitano itakuwa ya kusikia na kuona mambo mengi ya ajabu. sawa na kujenga daraja la salenda unaacha la wami
 
Crime haina expire date, sometimes muhusika anaweza kuwa ame move on but ikigundulika lazima awajibike, huenda aliziba nafasi ya mtu mwingine ambaye kwa kukosa stahili yake haku recover hadi leo.

Uhalifu wa mtu mmoja mmoja ndo unaweza sema hivyo
ikiwa ni widespread......lazima mkae chini kuona mnazuia vipi damages kwa jamii
 
Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....
Mkuu hili zoezi la vyeti 'contradictions' zitajitokeza. Inawezekana huyu mwenye cheti fake aliendelea na vyeti fake mpaka elimu ya juu zaidi au ilikuwa ni juhudi yake kufikia elimu ya juu. Mimi nadhani idara husika ilipashwa kuaangalia hili jambo. Utendaji wa kazi uzingatiwe kuliko kuangalia vyeti peke yake. Ni wazo langu. Ila kuna watu wana Masters PHD unajiuliza aliipata vipi kwani akifungua mdomo kuzungumza utaweka mikono kichwani ukijiuliza aliwezaje kusoma kufikia kiwango hiki!!!???
 
Ndiyo maana nimesema hili la Elimu ni swala gumu, kwa maana hapa unaongelea udanganyifu, hivyo basi kama umedanganya umefanya kosa ina maana unapaswa kuadhibiwa na haijalishi wewe ni nani au una wadhifa gani!

Nitakupa mifano, kuna Waziri wa Ulinzi wa nchi moja barani Ulaya aliondolewa kwenye wadhifa wake kwa sababu walikuja kugundua kwamba kwenye PhD thesis yake alinakiri kazi ya watu wengine, hali iliyopelekea Chuo Kikuu alichosomea kumvua Shahada yake ya PhD ingawaje ni miaka mingi ilipita na yeye alikuwa tayari amefikia ngazi ya Uwaziri na baada ya hapo Serikali ya nchi yake nayo ikamvua Uwaziri kwa sababu ya udanganyifu alioufanya zaidi ya miaka 10 iliyopita!

Ni kama vile kwa mfano Raisi wa USA Obama (sijui kama mfano unaendana), kuna wanaosema kwamba hajazaliwa USA na kwamba aligushi cheti cha kuzaliwa, sasa Je kama ingekuwa tuseme wanaosema hivyo wako sahihi unafikiri nini kingetokea? Unafikiri Obama angeachwa aendelee na Uraisi wake kwa sababu ni miaka mingi iliyopita au wangemu impeach?

Mifanoo ya mtu mmoja mmoja sidhani kama ina apply
nikupe tu mfano halisi
wafanyakazi wa bandari 1500 ambao wengi wanafanya kazi tu za mikono wamekamatwa na vyeti bandia vya form four
je wote wafukuzwe? mtu pengine ni kuli tu
anashiriki kubeba mizigo.....cheti halisi cha form four kinasaidia nini?

Madaktari tuseme wa Muhimbili labda robo yake wagundulike vyeti vya form four ni bandia
wafukuzwe wote?
 
Mkuu hili zoezi la vyeti 'contradictions' zitajitokeza. Inawezekana huyu mwenye cheti fake aliendelea na vyeti fake mpaka elimu ya juu zaidi au ilikuwa ni juhudi yake kufikia elimu ya juu. Mimi nadhani idara husika ilipashwa kuaangalia hili jambo. Utendaji wa kazi uzingatiwe kuliko kuangalia vyeti peke yake. Ni wazo langu. Ila kuna watu wana Masters PHD unajiuliza aliipata vipi kwani akifungua mdomo kuzungumza utaweka mikono kichwani ukijiuliza aliwezaje kusoma kufikia kiwango hiki!!!???

Halafu hilo zoezi ni kwa wanyonge
kina Muhongo na Mwigulu na Kigwangwala wametajwa mno humu kwa utata wa vyeti

Kigwangala cheti chake ni Andrea Kigwangala...huku anajiita Hamisi....
 
Kuna tatizo kubwa tatizo tunafikiri unapomfungia mtu office ndio njia ya kutatua tatizo wakati huyo mtu alikuwa amewaajiri wananchi waliompigia kura Rais akawa hapo alipo ,alafu leo hii Ajira ya yule mtu inakufa yeye moja kwa moja anaanza kuilaumu Serikali.
Tungetengeneza kwanza sheria ya kuwadhibiti kuanzia sasa kodi ilipwe ndani ya mwaka mmoja.
Kwa sababu tulifanya uzembe uko nyuma hata kuna wakandarasi nasika hawajawai kulipa kodi kuanzia miaka 5 iliyopita.
Sheria za kodi zipo lakini zilikuwa hazitekelezwi kikamailifu. Kwa sababu hizo watu walikuwa wanakwepa kulipa kodi au kutolipa kabisa. Serikali ya awamu ya tano haijatunga sheria mpya bali imeamua kufuatilia utekelezaji wa sheria zilizopo. Katika hatua hiyo imegundua wafanyakazi biashara ambao wanatozwa kodi hata miaka 10. Kisheria wana makosa na hatua zinazochukuliwa ni sahihi. Suluhu ni kulipa kodi bila kuingiza siasa
 
Mifanoo ya mtu mmoja mmoja sidhani kama ina apply
nikupe tu mfano halisi
wafanyakazi wa bandari 1500 ambao wengi wanafanya kazi tu za mikono wamekamatwa na vyeti bandia vya form four
je wote wafukuzwe? mtu pengine ni kuli tu
anashiriki kubeba mizigo.....cheti halisi cha form four kinasaidia nini?

Madaktari tuseme wa Muhimbili labda robo yake wagundulike vyeti vya form four ni bandia
wafukuzwe wote?

Ukiniuliza mimi ndiyo wafukuzwe, kwa maana wamedanganya, kwa maana nyingine ni kwamba hawakupaswa kuwepo hapo au kazi wanayoifanya hawakupaswa kuifanya na ilipaswa wapewe watu wengine wenye sifa!
Ni sawa tu na mwizi ambaye amejipatia mali kiudanganyifu!

Haya mambo siyo rahisi hivi kama unavyodhania, ukishaanza kutoa special treatment kwa uhalifu wa aina fulani kwamba huu unasameheka na huu hausameheki kama nchi hauwezi kwenda mahali, aliyedaganya amedanganya na hamna kusema sijui hivi au vile ni kwamba amedanganya na kama imethibitishwa hivyo hatua stahiki dhidi yake zichukuliwe, na haijalishi kama ni mtu mmoja, 5 au shirika zima, kwa maoni yangu!
 
kwanini leo kikwete,mkapa wapumzike kwa amani wakati walishiriki kuunda taifa la namna hii??ndomana nasema mh ni mnafiki
 
Hapa tumeongea kila MTU na maonn yske ingekua ya vyama mmmm na HIV ndo tunatakiwa kujadili maada
 
Back
Top Bottom