Haya maamuzi ni kujenga au kubomoa?

Haya maamuzi ni kujenga au kubomoa?

Mkuu The Boss, kwanza kwenye hili la vyeti feki, mimi naungana na serikali kuwa nia ni njema, ila utekelezaji inahitaji kiwango fulani cha busara ambayo very unfortunately busara hiyo haipo, utekelezaji ni wa kimakenika! .

Kuna vyeti fake, yaani vyeti bandia, na kuna kuna vyeti halisi ila majina ndio fake, au bandia.

Mfano sifa ya mtu kuwa mbunge ni angalau kuwa na elimu ya kidato cha 4. Ila ukitokea kuwa na elimu ya darasa la saba na unasifa za kuchaguliwa, unaweza kugombea. Kihiyo aliishia darasa la saba lakini akaghushi cheti na kudanganya amefika kidato cha nne, ilipobainika amefoji alifutwa ubunge. Lakini Prof. Maji Marefu ni darasa la saba na amejieleza yeye ni la saba na amechaguliwa hadi sasa ni Mbunge, hivyo kosa ni kughushi hii ni jinai! .

Dr. Hamisi Kigwangala alifeli darasa la saba, akachukua jina la mwanafunzi mwingine Said Bagaile na kusoma hadi kidato cha nne, ila alibadli jina na kutumia jina lake halisi la Hamisi Andrea Kigwangala. Aliyehudhuria masomo ni Hamisi Kigwangala na sio Said Bagaile, alipasi vizuri form IV, akapasi vizuri form VIP na sasa ni dakitari, japo mwanzo alighushi jina kuingia shule aliyesoma ni yeye na aliyehitimu ni yeye huyu hawezi kuachishwa au kufukuzwa.

Hivyo kama mtu alighushi cheti cha form IV lakini akaingia chuo, akasoma, akapata degree, mtu huyo hiyo degree yake ni halali na sio degree fake, hastahili kufukuzwa! .

Lakini kama kazi imetangazwa sifa ni cheti cha form IV au form VI au degree ya chuo kikuu, halafu akaja mtu hakusoma, hana elimu hiyo ila alileta cheti fake, then huyu ni wakufukuzwa bila huruma hata kama baadae alikuja kupata in service training na anaimudu vizuri kazi yake kwa sababu alipata kazi kwa self pretence.

NB. Kuna watu wana vyeti vya ukweli lakini kwenye delivery ni mabomu tuu hayawezi chochote, na kuna watu hawana elimu kabisa lakini wana deliver kuliko hao wenye elimu za ma vyeti! .

Serikali inapaswa ifanye tathmini yakinifu kabla haijafikia uamuzi wa kuwaachisha ikiwemo kuangalia the ability na the capacity to deliver! .

Mimi nilipata kazi ya wazungu fulani nikiwa na just a degree lakini nimeshindana na wenye masters na wenye Ph.D niliwaacha kwenye amplitude test za Delloite!, hivyo serikali yetu isigangamale na macheti tuu itaingia hasara ya macheti makubwa lakini performance na delivery zero! .
Pasco

Ndo maana naona zoezi zima halina maana
tukianza na kuulizana wenye 'capacity to deliver' mbona hata huko Ikulu watu tunaona 'hakuna kitu'
Phd inaleta maswali meengi

Na sio Kigwangala tu....Prof Muhongo je?Mwigulu Nchemba je?
 
Kati ya vitu naamini Magufuli hatagusa ni uraia feki...
cc Pasco.......kama ambavyo alishindwa kuvunja 'mbio za mwenge'
baada ya kujua 'umuhimu' wake
Ni kweli hili hataligusa kabisa na inawezekana kabisa Watanzania kamwe hawatakuja kuijua historia halisi ya kijana mmoja Banyamulenge aliyelelewa kwa Mzee Machalila pale Karagwe na kupewa jina la Kihaya la Katto! .

Pasco
 
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?

Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..

je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?

Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?

walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....

kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?

kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?

na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?
Hivi wewe kijana kwa nini huoni aibu?..hata huko US wagombea wanajisafisha kulipa kodo walizokwepa...wewe kukwepa kodi ni jinai na sio suala la kulaumu serikali, ndio maana mlipa kodi hutakiwa ''kufile return' na kujikadiria.
 
Ndo maana naona zoezi zima halina maana
tukianza na kuulizana wenye 'capacity to deliver' mbona hata huko Ikulu watu tunaona 'hakuna kitu'
Phd inaleta maswali meengi

Na sio Kigwangala tu....Prof Muhongo je?Mwigulu Nchemba je?
Mimi sina tatizo na wasomi walioiba tuu majina ya wengine ili kuingia sekondari, lakini darasani wamehudhuria masomo na wapefanya vizuri hadi kuwa madaktari, may PhD holders na ma Prof, bali natatizwa na wenye titles kubwa ila elimu zao ni fake
 
wanaosema(ga) nchi ngumu hii nimeamini.

ukichukua hatua ni kosa, ukiacha ni kosa pia

hatari sana
 
Kutafuta wenye vyeti feki is one good thing,hii ni kwa sababu tatizo lingeendelea kuwa sugu kama lingeendelea kufumbiwa macho,na pengine ndugu zako wangeshindwa kupata haki zao katika ajira kwa sababu ya watu kama hao,tatizo linakuja pale utaratibu wa kutimiza hilo unapokuwa duni na kuchanganywa na siasa na kuwafanya watumishi wengine kukosa stahiki yao kwa kigezo cha kutafuta wenye vyeti feki na wafanyakazi hewa.ufanisi ungehitajika katika process nzima ya kuwashughulikia watu hawa bila kuumiza upande mwingine ingekuwa vizuri zaidi
 
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?

Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..

je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?

Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?

walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....

kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?

kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?

na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?
Kuna la leo la CEO wa TTCL
 
Nilitegemea alipoingia madarakani angechora red line na kuweka misingi mipya.
Hapa namaanisha angesahau yaliyopita maana tukianza kufuatilia alie msafi kwa awamu iliyopita hakuna atakae salimika unless huyo mtu hakupata hiyo nafasi at all. Naamini hata yeye kuna mahali alicheza foul au ku take advantage.Huu ni muda wa ku move on as a nation na sio kufukua makaburi na kuwagawa wananchi
 
Mara nyingi wanaofukua makaburi huwa hawafanikiwi.......
makaburi ni mengi ya kufukua na mda hautoshi...
 
Sijui kama kuna neno la hivyo katika lugha ya Kiswahili.
Hiyo lugha yenu wala siijui sana , nyumbani kwangu wala haiongewi hata kidogo , hii natumia tu hapa Jf ili kurahisisha mawasiliano .
 
mimi kinachonishangaza ni kusimamisha ajira, alafu idara zinazohusika na kuajir, ukijumlisha idara za serikali amabzo zinamapungufu watu kukaimu na kuendelea kupiga pesa...
mfano pale secretaret, kuna watumish zaid ya 100, wanakula sarary bila kazi yyte kwa miez minne sasa.....

bado, maofisa wautumishi wanaosubil kuaproval, wametulia tu maofisin wanapigana picha...
 
Kati ya vitu naamini Magufuli hatagusa ni uraia feki...
cc Pasco.......kama ambavyo alishindwa kuvunja 'mbio za mwenge'
baada ya kujua 'umuhimu' wake
The Boss. Kuna jamaa mmoja namfahamu. Mtihani wa form four alifaulu vizuri sana na akachaguliwa kwenda A level. A level alimaliza na kufaulu kiasi. Ikaja sasa ngoma wakati wa kuingia chuo kikuu. Kila akipiga mahesabu hayakubali kwani kwenye cheti chake alikuwa na grade C, C na S (subsidiary) wakati chuo kikuu, wakati huo, walikuwa wanataka angalau grade C kwenye masomo yote ya combination. Jamaa ''akacheza'' na cheti kikasomeka ana C, C and C kwenye combi yake na akaingia chuo na kufaulu vizuri sana. Baaadae akasoma na masters na sasa hivi anafanya kazi vizuri tu. Je, huyu nae kweli tumpoteze kwa ajili ya ile S aliyoigeuza kuwa C? Hapana! Ndio maana naunga mkono hoja yako. Hili suala linahitaji busara zaidi badala ya kufanya kazi kama robot! Mimi wafoji vyeti wanaonikera ni wale wanaochukua cheti cha mtu na kuomba nacho kazi wakati wakijua hawakusomea ile taaluma. Au wanaochonga vyeti na kujifanya wamehitimu kumbe hawakuhitimu. Au wenye vyeti visivyotambulikana eg first degree au PHD kutoka hizi University magumashi kama aliyosoma Mrema na kina Nchimbi.
 
Kuhusu Elimu ni swala gumu kidogo lkn hili la kufunga Biashara siyo gumu kwani kwa kawaida ukiona mtu kafungiwa Biashara yake ujue hiyo ni hatua ya mwisho kabisa kuchukuliwa na Serikali, kuna watu wanadaiwa kwa zaidi ya miaka 10 na siku zote wamekuwa wakionywa na kuandikiwa barua lkn bado hawajali sasa ulitegemea nini kifanyike tena zaidi ya hapo?
Sidhani kama kuna duka la mtu au biashara iliyofungiwa kwa sababu ya tu ameshindwa kulipa kodi ya mwezi/mwaka 1 tu na kwamba hilo lilikuwa ni onyo la kwanza, sidhani kama kuna kitu kama hicho, mara nyingi ni ukaidi wa muda mrefu!
Nakupa like kwa kujibu kistaarabu, kumbe sometimes huwa ni swaga tu
 
The Boss. Kuna jamaa mmoja namfahamu. Mtihani wa form four alifaulu vizuri sana na akachaguliwa kwenda A level. A level alimaliza na kufaulu kiasi. Ikaja sasa ngoma wakati wa kuingia chuo kikuu. Kila akipiga mahesabu hayakubali kwani kwenye cheti chake alikuwa na grade C, C na S (subsidiary) wakati chuo kikuu, wakati huo, walikuwa wanataka angalau grade C kwenye masomo yote ya combination. Jamaa ''akacheza'' na cheti kikasomeka ana C, C and C kwenye combi yake na akaingia chuo na kufaulu vizuri sana. Baaadae akasoma na masters na sasa hivi anafanya kazi vizuri tu. Je, huyu nae kweli tumpoteze kwa ajili ya ile S aliyoigeuza kuwa C? Hapana! Ndio maana naunga mkono hoja yako. Hili suala linahitaji busara zaidi badala ya kufanya kazi kama robot! Mimi wafoji vyeti wanaonikera ni wale wanaochukua cheti cha mtu na kuomba nacho kazi wakati wakijua hawakusomea ile taaluma. Au wanaochonga vyeti na kujifanya wamehitimu kumbe hawakuhitimu. Au wenye vyeti visivyotambulikana eg first degree au PHD kutoka hizi University magumashi kama aliyosoma Mrema na kina Nchimbi.

Kuna jamaa alifeli form four
akachonga cheti akaenda DUCE akasoma akafaulu
akaanza kufundisha secondary....wakamdaka..wamemtimua....
 
Siku zote kujali ajira za watu inapaswa kuwa kipaumbele
sio tu kufilisi tu ili mradi sheria zifuatwe
Kwa sasa yuna janga kubwa la ukosefu wa ajira kwa vijana na wasomi wetu,sasa tukiendekeza hii tumbuatumbua tutatengeneza bomu kubwa sana ambalo likipasuka sijui tutakimbilia wapi,ugumu wa maisha kwa awamu hii naona hata matukio ya ujambazi na vibaka mitaani wameongezeka
 
Busara serikalii hiii ni kama kumpigia mbuzi gitaa
 
Kuna jamaa alifeli form four
akachonga cheti akaenda DUCE akasoma akafaulu
akaanza kufundisha secondary....wakamdaka..wamemtimua....
Kimsingi mtu kama huyu ni qualified na kumfukuza ni kumwonea tu. Kufeli mtihani kama wa form four inaweza kutokea hata kwa mtu mwenye uwezo mzuri. Watu kama hawa wangefumbiwa macho ila mkazo uwekwe kwa wanaoajiriwa sasa. Mimi bado nasisitiza kwenye vyeti feki wangecheza na groups za watu hawa:
1. Waliochukua vyeti vya watu wengine huku wao wenyewe hawana zile qualifications
2. Walionunua vyeti huku hawana qualification.
3. ''Waliohitimu'' shule na vyuo feki (nyingi zipo online). eg: Unakuta mtu anaitwa Dr Kikojozi kumbe phd yake kasoma online kwa nusu mwaka.
 
Sasa hizi busara ndo zinahitajika
lakini ni kama vile 'tunampigia mbuzi gitaa'
 
Back
Top Bottom