Haya maamuzi ni kujenga au kubomoa?

Haya maamuzi ni kujenga au kubomoa?

Ukiniuliza mimi ndiyo wafukuzwe, kwa maana wamedanganya, kwa maana nyingine ni kwamba hawakupaswa kuwepo hapo au kazi wanayoifanya hawakupaswa kuifanya na ilipaswa wapewe watu wengine wenye sifa!
Ni sawa tu na mwizi ambaye amejipatia mali kiudanganyifu!

Haya mambo siyo rahisi hivi kama unavyodhania, ukishaanza kutoa special treatment kwa uhalifu wa aina fulani kwamba huu unasameheka na huu hausameheki kama nchi hauwezi kwenda mahali, aliyedaganya amedanganya na hamna kusema sijui hivi au vile ni kwamba amedanganya na kama imethibitishwa hivyo hatua stahiki dhidi yake zichukuliwe, na haijalishi kama ni mtu mmoja, 5 au shirika zima, kwa maoni yangu!

Ndo maana tunatofautiana mitazamo
kwangu kama kampuni 20 zimedanganya kodi
na zina waajiriwa elfu 20 kuzifilisi na kuzifungia sio busara
unatafuta namna ingine walipe huku wanaendelea kuwepo

Same kwa waajiriwa.....kana una madaktari 200 wamedanganya ...lakini vyeti vya taaluma ni vyao
ni bora kuwaacha tu.....kuna sababu

shule za secondary zilikuwa chache sana
walifaulu hawakuchaguliwa na kadhalika na kadhalika...
 
Kama nilivyosema kwangu mimi ni swala la HAKI, kwa nini wengine wasome kwa tabu, wafaulu Mitihani halafu wengine waje kununua vyeti na kupata kazi? Hapo haki iko wapi? Mimi naamini ktk haki ndiyo maana nasema kama waligushi vyeti hata kama ni Muhimbili nzima ningewatoa kama mimi ndiyo ningekuwa muajiri wao!
 
Kwa hiyo unataka vyeti vya kughushi vihalalishwe?
Mkuu nadhani hujamuelewa The Boss

kwa leo hakuongea siasa ameongea ukweli tusiwe tunapinga kila hoja kwa vile tunajua si mlengo wetu.

ameongea ukweli kabisa
 
Mkuu
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?

Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..

je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?

Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?

walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....

kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?

kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?

na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?
mkuu nasikitika kwamba post yako yenye mantiki ni watu kumi tu wata ielewa! Mi wakwanza bado tisa
 
Mimi nawajua watu waliofukuzwa kazi kwa vyeti bandia vya kidato cha nne
huku wanavyo vya ukweli vya taaluma na wamefanya kazi kwenye taaluma hizo miaka....

Napata wasi wasi na thinking yako...ufoji vyeti vya form four na form six...halafu tuhalalishe cheti cha chuo??
Unakumbuka tamko la kisheria wakati unahakikiwa vyeti wakati wa kujiunga chuo???..wakati wowote chuo kikiridhika ulidanganya iwe kwenye mtihani au kuwasilisha vyeti... Kinafuta cheti cha chuo.
Napata mashaka na vyeti vyako.....popobawa kapita nini....
😀😀😀😀😀
 
Serekali ya CCM inatengeneza ajira kwa kuwafukuza waajiriwa,wakati huohuo serekali ya CCM inaimarisha kundi la vibaka mitaani kwa kuwaongezea nguvu kazi ya waajiriwa inaowafukuza.
 
Kama nilivyosema kwangu mimi ni swala la HAKI, kwa nini wengine wasome kwa tabu, wafaulu Mitihani halafu wengine waje kununua vyeti na kupata kazi? Hapo haki iko wapi? Mimi naamini ktk haki ndiyo maana nasema kama waligushi vyeti hata kama ni Muhimbili nzima ningewatoa kama mimi ndiyo ningekuwa muajiri wao!

Kula tano mkuu....
The end does not justify the means
 
Ndo maana tunatofautiana mitazamo
kwangu kama kampuni 20 zimedanganya kodi
na zina waajiriwa elfu 20 kuzifilisi na kuzifungia sio busara
unatafuta namna ingine walipe huku wanaendelea kuwepo

Same kwa waajiriwa.....kana una madaktari 200 wamedanganya ...lakini vyeti vya taaluma ni vyao
ni bora kuwaacha tu.....kuna sababu

shule za secondary zilikuwa chache sana
walifaulu hawakuchaguliwa na kadhalika na kadhalika...
Wakiifungia serikali inakosa PAYE ya hao watu 20 wataokosa kazi, kama mtu hajalipa kodi miaka 10 maana yake ni mapungufu ya pande mbili serikali na mlipa kodi hivyo kwa mazingira kama hayo inabidi wakae waangalie namna ya ku-handle hiyo changamoto maana mfanyabiashara ana hasara na serikali ina hasara zaidi maana inampoteza huyo mtu
 
Tukimaliza vyeti vya forma four tunakwenda kuangalia uraia feki,baadae wanaccm feki........ Utashangaa niaka mitano inamalizika tunakimbizana na maswala madogo madogo.
 
Kati ya vitu naamini Magufuli hatagusa ni uraia feki...
cc Pasco.......kama ambavyo alishindwa kuvunja 'mbio za mwenge'
baada ya kujua 'umuhimu' wake
 
Crime haina expire date, sometimes muhusika anaweza kuwa ame move on but ikigundulika lazima awajibike, huenda aliziba nafasi ya mtu mwingine ambaye kwa kukosa stahili yake haku recover hadi leo.
Professionals need to be honest people, how can you call yourself a Dr. with the responsibility of looking after a society while you are not a honest person?
 
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?

Sasa tuje na maamuzi ya kufunga biashara za wote wanao tuhumiwa kukwepa kodi..

je tukifunga hizo biashara na wanaotegemea hizo biashara kufilisiwa
ndo tumejenga?

Kwanini wasiwekewe utaratibu wa kuanza kulipa hata kidogo kidogo taratibu?

walioajiriwa kwenye biashara hizo je? hatuwajali?....

kama mtu hajalipa kodi miaka 10 je hatuoni ni uzembe pia wa serikali?

kufilisi na kufunga tu kila biashara wakati ukwepaji kodi ulikuwa kama ni utamaduni wa nchi nzima
kunasaidia nini?....si bora walazimishwe kulipa hata nusu ya kodi wanayodaiwa?

na biashara zao zibaki kuajiri na kuchangia uchumi?

Umesema kweli lakini hakuna atakayekusikiliza.
 
Halafu hilo zoezi ni kwa wanyonge
kina Muhongo na Mwigulu na Kigwangwala wametajwa mno humu kwa utata wa vyeti

Kigwangala cheti chake ni Andrea Kigwangala...huku anajiita Hamisi....
Hahahahhh nimecheka sana Andrea=Hamisi NHC naye mmh aka Kyandozzz
 
Kuna maamuzi mengi ya serikali hii ya awamu ya tano unajiuliza tu nani ni 'mastermind'?
na anajua hasa hasara ya maamuzi hayo au ili mradi 'sheria zifuatwe'?

La kwanza ni la vyeti feki.....binafsi nilifikiri walipaswa haswa kutazama vyeti bandia vya kitaaluma
ambavyo kama ni feki madhara yake yanajulikana...

lakini cha kushangaza wame concentrate sana na vyeti vya kidato cha nne...

Sasa unakuta mtu ana cheti bandia cha kidato cha nne lakini alitumia cheti hiko kusoma
taaluma akafaulu na kufanya kazi kwenye taaluma husika miaka hata 20

leo unakuja kumfukuza huyu mtu...hasara ni ya nani hasaa hapa?

mfano huyo mtu ni mwalimu au daktari.....je nani watakao athirika?

tuna walimu wa kutosha na madaktari wa kutosha?

Nimesikia tetesi kuna Professa wa Chuo kimoja maarufu kakamatwa na cheti cha form four
feki...proffesa huyu keshafundisha wanafunzi tele anakaribia kustaafu.....

Kama vyeti vya darasa la saba wamesema havina umuhimu..tujiulize na hivi vya form four
kuanza kuvichimba chimba leo kuna umuhimu gani iwapo wahusika wana vyeti vyao vya kweli vya taaluma zao? au ndo 'siasa za kukomeshana kila sekta' tu?

hivi hili zoezi ndo linajenga au linabomoa?
Mkuu The Boss, kwanza kwenye hili la vyeti feki, mimi naungana na serikali kuwa nia ni njema, ila utekelezaji inahitaji kiwango fulani cha busara ambayo very unfortunately busara hiyo haipo, utekelezaji ni wa kimakenika! .

Kuna vyeti fake, yaani vyeti bandia, na kuna kuna vyeti halisi ila majina ndio fake, au bandia.

Mfano sifa ya mtu kuwa mbunge ni angalau kuwa na elimu ya kidato cha 4. Ila ukitokea kuwa na elimu ya darasa la saba na unasifa za kuchaguliwa, unaweza kugombea. Kihiyo aliishia darasa la saba lakini akaghushi cheti na kudanganya amefika kidato cha nne, ilipobainika amefoji alifutwa ubunge. Lakini Prof. Maji Marefu ni darasa la saba na amejieleza yeye ni la saba na amechaguliwa hadi sasa ni Mbunge, hivyo kosa ni kughushi hii ni jinai! .

Dr. Hamisi Kigwangala alifeli darasa la saba, akachukua jina la mwanafunzi mwingine Said Bagaile na kusoma hadi kidato cha nne, ila alibadli jina na kutumia jina lake halisi la Hamisi Andrea Kigwangala. Aliyehudhuria masomo ni Hamisi Kigwangala na sio Said Bagaile, alipasi vizuri form IV, akapasi vizuri form VIP na sasa ni dakitari, japo mwanzo alighushi jina kuingia shule aliyesoma ni yeye na aliyehitimu ni yeye huyu hawezi kuachishwa au kufukuzwa.

Hivyo kama mtu alighushi cheti cha form IV lakini akaingia chuo, akasoma, akapata degree, mtu huyo hiyo degree yake ni halali na sio degree fake, hastahili kufukuzwa! .

Lakini kama kazi imetangazwa sifa ni cheti cha form IV au form VI au degree ya chuo kikuu, halafu akaja mtu hakusoma, hana elimu hiyo ila alileta cheti fake, then huyu ni wakufukuzwa bila huruma hata kama baadae alikuja kupata in service training na anaimudu vizuri kazi yake kwa sababu alipata kazi kwa self pretence.

NB. Kuna watu wana vyeti vya ukweli lakini kwenye delivery ni mabomu tuu hayawezi chochote, na kuna watu hawana elimu kabisa lakini wana deliver kuliko hao wenye elimu za ma vyeti! .

Serikali inapaswa ifanye tathmini yakinifu kabla haijafikia uamuzi wa kuwaachisha ikiwemo kuangalia the ability na the capacity to deliver! .

Mimi nilipata kazi ya wazungu fulani nikiwa na just a degree lakini nimeshindana na wenye masters na wenye Ph.D niliwaacha kwenye amplitude test za Delloite!, hivyo serikali yetu isigangamale na macheti tuu itaingia hasara ya macheti makubwa lakini performance na delivery zero! .
Pasco
 
kwanini leo kikwete,mkapa wapumzike kwa amani wakati walishiriki kuunda taifa la namna hii??ndomana nasema mh ni mnafiki
Mkapa na Kikwete wanapumuzika kwa amani kwa sababu ya mapungufu ya katiba ya sasa ambayo inawakingia kifua kutoshitakiwa. Kama katiba inayopendekezwa itatoa kipengele hicho na ikakubalika itekelezwe "retrospectively which is rare" kwa hiyo wataingia kwenye "mist net" yawahalifu wote dagaa na mapapa
 
Back
Top Bottom