Haya hapa makosa ya habari ya kaburi la Balalli iliyoripotiwa na gazeti la Mwananchi Julai 12, 2014

Nyie pigeni kelele tu. Mwandishi kavuta si chini ya 10 ml. Na watu wenye akili nyepesi bado wanaamini hili gazeti
 
Kama nitakua na kumbukumbu vizuri, gazeti la mwananchi (hiyo mwaka 2007) ndio lilikua gazeti la kwanza ku-report kua Balali anaumwa na ameondoka kimya kimya to USA, gazeti lililofuata siku ya pili, liliripoti tena kua limemuuliza waziri wa Fedha (alikua bi Zakia Megji) nae alionesha kutokujua kama Balali alikua anaumwa na kaondoka nchini, tukumbuke ki protocal huyu mama alikua ndio boss wa Balali. Gazeti lilioripoti kua Balali kafariki dunia lilikua Tanzania Daima, nadhani aliyethibitisha alikua huyu mhariri mkuu wa gazeti hili kwasasa, by that time alikua anapiga shule kule Uingereza. Kama serikali inataka kuficha kitu (yawezekana kweli jamaa alikufa ua hakufa sina uhakika) nadhani wangetumia magazeti mengine, mwananchi kuamadhani Semtawa wameisha onesha kua wananunulika, refer to zzk Saga! Naville Maena ninahakika ni member humu kwa jina la bandia kama tufanyavyo sisi pia, ningepanda aje athibitishe cause mleta uzi hu (shukurani za pekee kwake kwa uchambuzi alioufanya) ametengeneza habari ambayo ukweli ni ngumu sana kumpinga, kaweka ushahidi uliokwenda shule hasa
 
Meena alitakiwa kueleza nini hasa lengo la yeye au waliomtuma kutuletea hiyo habari.
 
Story hii ya gazeti la Mwananchi, na Mtanzania zinatia shaka Ueledi wa vyombo hivi vya habari wa kuwalazimisha wasomaji au wananchi kijumla, kuamini kuwa KIFO CHA BALALI AMBACHO KWA MUJIBU WA STORY ZAO WENYEWE WANAAMINI KUWA KILIGUBIKWA NA UTATA MKUBWA ULIYOPO MPALA LEO PAMOJA NA JUHUDI ZOTE ZILIZOFANYWA NA MAGAZETI HAYA KWA NIABA YA WALIYOWATUMA.

Kama kweli wao hawakutumwa na walifanya kazi hiyo kwa UTASHI wao ili kuwaelimisha wananchi kuhusu utata uliyopo wa kifo cha Balili, Basi, katika uchunguzi wao walipaswa kuongozwa au kuzingatia na masuala haya TETE yaliyoibua mashaka haya kwa Watanzania na siyo ndugu wala Familia ya Balali.

Kwanza .Dhiki wanayopata Watanzania katika mioyo ,ni Kwa nini kiongozi huyu aliekuwa muhimu katika tuhuma nzito ya Ufisadi,
(i.) Aondoke ghafla nchini, wakati fukuto uchunguzi wa Tuhuma hi ndiyo unaanza?
(ii.) Kama kweli alikuwa anaumwa uthibitisho wa vyeti vya Hospitali unapaswa kuwekwa na madaktari waliyokuwa wanamhudumia wanapaswa kupatikana na kueleza ukweli.

Hii ni muhimu kwa sababu Ufisadi wa EPA ulikuwa una mhusu Balali katika kuthibitisha kilichotokea wakati wa matumizi ya fedha hizo.
Kwa hiyo maadamu Rais alimwachisha kazi kwa tuhuma hizi, kwa vyo vyote vile system ilikuwa inamwangalia kwa karibu sana nyendo zake. haiwezi kumchukulia Mtu muhimu kama huyu kwa usalama wa Taifa kama Chitembeja! Haiwezekani.

Suala la Pili huyu, alikuwa Rai wa nchi gani, Tanzania au Merikani? Utamaduni na taratibu za nchi yetu ni Raia wake akifia nje, Serikali, ndugu na jamaa hufanya kila linalowezekana Mwili kurejeshwa nchini, Mwandishi au chombo kilipaswa kije na maelezo ya Serikali, ndugu na jamaa na marafiki wa Karibu, sababu za msingi zilizokuwa nje ya uwezo wao zilizosababisha mwili wa Mtu huyu Muhimu kwa taifa hili usirudishwe nchini? Nini nini hicho?

Suala la tatu ambalo mwandishi wa Habari au vyombo hivi wanagejikita zaidi kuchunguza. Ni sababu zipi kuugua kwake, kufa kwake, na kuzikwa kwake kumegubwikwa na Utata na kiza kinene sana, hasa kuzikwa kwake amezikwa kama Osama,
Chunguzeni kwa nini serikali haikujihusisha kabisa na mtu huyu wakati wapo wastaafu wengi tu wa nafasi nyeti kama yake wanawajali katika kufiwa na kufa, why Balali ambaye hadi anaugua hadi kufa alikuwa hajafikishwa Polisi wala Mahakamani?
Kwa nini hata ndugu wa nje ya familia yake hasa wanaishi Marekeni hawakutakiwa kujua kuugua kwake, kufa kwake na kuzikwa kwake hakuwa na hata rafiki mmoja huko Merikani?

Suala la NNE Muhimu zaidi kwa nini uchungizi wa sauala hili tata namna hii ufanywe na vyombo vya habari na kutoa hicho kinachoitwa ukweli badala ya Serikali baada ya miaka yote hii ya Utata? Na kwa nini ni vyombo hivi viwili tu na wametoa habari hii kwa wakati mmoja na zote hazina tofauti kubwa?

Mwisho ninavitaka vyombo hivi kujibu masuala haya ya msingi kwangu kwa sababu story zao zinaweza kuchukuliwa kama watu wanaotumika kufukia dhana ya watu makini inadaiwa kuwa BALALI KAUWAWA ILI KUFICHA AUN KUHARIBU USHAHIDI WA UFISADI WA EPA.

Wanapswa wafahamu kuwa mara zote wezi wakubwa majambazi wanaofanya kazi kwa makini siyo vibaka au panya Road wakitekeleza wizi au ujambazi wao kazi ya kwanza ni kuwauwa waliyowasaidia katika mpango wao wa wizi huo ni muhimu sana kwao na hapa ndiyo kilichoonekana Kumkuta Balali.

Pili Kama kweli kifo chake ni mpango basi watu waliyotekeleza mpango huo ni watu makini na wazoefu waliyojua walichokuwa wanakifanya, uchunguzi wake hauwezi kufanyika na akina Meena huku ni kukufuru kabisa, uchunguzi wa Kifo cha Balili unapaswa kufanywa na mashirika ya kimataifa ya upelelezi kama FBI siyo Mtanzania na Mwananchi hiki ni kichekesho.

Familia ya Balili haina cha kusema kwa sasa kwa sababu inaonyesha nayo ilifahamishwa au ilikuwa inajua kilichotokea.
Kwa hiyo kutegemea maelezo ya leo baada ya miaka yote hii nako kichekesho unataka kutuambia maiaka yote hii kama kifo chake kilikuwa cha hujuma waliyohujumu hawakujuwa kuwa alikuwa na familia yake ambao ndiyo wasemaji wakuu wa kuugua kwake kufa kwake na kuzikwa kwake? Na kama walijua waliwaacha hivi hivi?

Uandishi wa aina hii unaliondeshea gazeti sifa zake na kuonekana kituko mbele za wasomaji wao.
 
Walianza na Mwaisapile, juzi juzi hapa wakalikuza suala la ugonjwa wa Dengue, na sasa wanatuletea Balali.
Wanataka kututoa kwenye hoja ya Katiba Mpya ili turudi miaka Sita nyuma kwa kumjadili Balali.
Ova.
 
Inaonekana mwandishi alikurupushwa aiandike hii habari fasta fasta!

Ndo maana haina quality hata kidogo.Eti ilimchukuwa siku tatu kugunduwa kaburi.Ni kuligunduwa ama kulipata?Maana si alienda kulitafuta?

Halafu inaonyesha hakuwa na ushirikiano na ndugu za kina Balali ie mke wake bi Anna Muganda!

Wanaleta habari ambazo hazina uhakika na kujidai zina uhakika!

Thats why nikajiuliza, why now?
 
Hata mleta uzi walengwa wake ni watu kama wewe.

Kwa utata wa tukio zima ulivyo kulikuwa na haja gani muandishi mzima kufunga safari yote hiyo na kurudi na ushahidi hafifu kiasi hicho ?

Kama alifunga safari kwa nia njema na kukosa ushahidi unaoridhisha watanzania (kuondoa wewe na wenzako wachache) kulikuwa na sababu gani ya kuja na hiyo habari, si angekaa kimya tu...na hakuna ambaye angemuuliza.

Mkuu haumung'unyi maneeno
 
Iko hivi, mwandishi kaeleza kwamba hilo kaburi liko mstari wa mwisho kabisa; ndiyo maana hakuna makaburi mengine yanayoonekana beyond makaburi yalio mstari wa Ballali.

Unaweza kusema, sasa ni kwa nini asipige picha kutoka upande ule mwingine, ili makaburi mengine yaonekane .... jibu ni kwamba makaburi mengi huwa yanaandikwa upande mmoja tu, hivyo kwamba kama angepiga upande wa pili hakungekuwa na maelezo ya kwamba kaburi ni la Ballali.

Na sababu ya kutoliona hilo kaburi siku mbili za kwanza, ni kwa sababu ya ukubwa wa eneo lenyewe na wingi wa makaburi; halafu bear in mind kwamba haya makaburi hayazikwi kwa kujipanga kama bongo .... kwamba leo wanazika hapa; kesho wanaendelea pale etc ... to the extent unaweza kujua kaburi la marehemu liko wapi kama unajua lini alizikwa. Marekani ni tofauti; watu wananunua sehemu za maziko, na ndiko wanakozikwa .. so unaweza kukuta mtu kazikwa jana, na pembeni yake kuna kaburi la miaka 20 iliyopita!

Kwa hiyo ni vigumu sana kulitafuta na kulipata kaburi la mtu kwa kuzunguka tu pale makaburi, kwa kubahatisha! Wale jamaa wa makaburi wanakua na ramani ya makaburi yote .. so ukiwauliza wanakuelekeza vizuri!

I hope umeelewa sasa.

huna logic hapo mkuu! kifo ya balali ni usanii wa wakati ule labda afe sasa!
 
Mwandishi katuletea ushahidi japo wa picha,wale wenye ushahidi mwingine nao watuletee tuone huo uhai wake,acheni majungu

kwa akili yako iliyochoka una haki ya kusema huo ni ushahidi? structure kama hiyo inaweza kujengwa hata kule sangamwalugesha na tukaambiwa ni kaburi la dr balali!!!! use your head to think wisely!!!!
 
Mkuu maendeleo yapi unayozungumzia? Yaan mkuu wa kaya adanganye kisa alete story sebulen wakat wa chakula et kafa!! Sasa watt c wanamuulza, Bba kwa nn usimlete huku tukamzika? Anajib ooo unajua n siri,ooo cjui gharama... Halafu anatangaza hakuna matanga!!! Hv kweli ukiwa kwenye hyo kaya usiulize?

Haya maendeleo yakutokuhoji n yapi?
Yaan kwa akili za kawaida mtu asafr mpaka usa halafu aje na ushahidi picha la kabur!! Kweliii huyu ni mwandishi au ni mwandani? Au kapewa pesa ili ale akitumia mwanya wa gazet linaloaminika sana?

Ni maendeleo gan ya kutufanya cc watanzania kuwa kichwa cha mwendawazim? Watu wanaanzisha scandal ili kusahau ajenda mhim za nchi? Mfn mdogo n wa makamba et nae anataka kuwa rais! Duh jaman jaman tena ili kukoreza na RAIS nae anacoment ili wtz tusahau mambo ya mhim tujadili upuuzi,

Hatujakaa sawa huyu nae analeta uchunguzi wa kipuuz kweli et balal kafa na picha ya kabur, aseee jaman n lin mtaacha kuwa waongo?

Binafc namuamin sana tido ckutegemea angeruhusu upuuz huu uandikwe kwenye kazeti analoliongoza, nataman akanushe habar hii!

Mkuu ukisema maendeleo n pamoja na kuhoji mambo c kukaa kimya!

Ushaur kwa vyombo vya habar achen kuhamishwa na viongozi kwa story(scandal) za kuunda bakini njia KUU.
MziziMkavu kachemka mbaya! au na yeye ni mnufaika wa EPAGATE?
 
Last edited by a moderator:
Kutoka kurugenzi ya mawasiliano!

Ili kuleta maendeleo ya haraka na kusogeza huduma kwa wananchi tumeanzishwa wilaya mpya ya Balali katika mkoa mpya wa Balaa,na kwa mamlaka niliyopewa namtanganza ndugu Neville Meena kuwa mkuu mpya wa wilaya ya Balali.Kabla ya uteuzi ndugu Meena alikuwa mwandishi wa habari katika kampuni ya Mwananchi communication!Uteuzi huu unaanza mara moja
 
Aliyemwonesha kaburi kwa mujibu wa maelezo yake ni ndugu anayetoka Mafinga ila sasa
Pale aliposema alienda siku ya kwanza na ya pili hakuona kaburi na siku ya tatu aliomba msaada wanuongozi wa kaburi, je siku 2 za mwanzo aliongia hapo bila kujieleza anatafuta nini? Au ni mbwe mbwe za kutudanganya watanzania . Pia anavyosema kwamba sasa ndugu wa valali wanaweza kwenda kuliona je waliomzika ni nani? Ndugu wa karibu ndo waliomzika sasa nani katika hao ndugu hajui mzee wao kazikwa wapi? Meena anajipaka mavi ambayo baadaye itamfanya ajichukie kwa harufu jua likiwaka.
 
Halafu muulize kitu kimoja Kuwa 2008 hakuna marehemu wengine waliokufa wakazikwa karibu na balali ?

mkuu sina cha kumuuliza mwandishi kwani namuona kama pimbi tu kwa sasa! umewahi kusoma novel ya James Hadley Chase iitwayo THE COFFIN FROM HONG KONG? kama bado itafute, isome kisha ulinganishe na hii comedy ya kifo cha Dr Balali!
 
Mwananchi ni moja kati ya gazeti ninaloliamini lakini kwa habari hii naanza kufikiri upya!

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Mkuu niliyasema haya mwanzoni kabisa mwa scandal ya Mbasha's,baada ya kuiweka first page na kuiandika stori kiudaku udaku bila kuhoji maswali ya msingi,nikasema Mwananchi limepotoka na niliacha kununua Mwananchi tokea wakati huo
 
Mkuu umenena vema na ushahidi usio na shaka.

Kwenye web hakuna jina,

Kwanzia leo sitosoma tena gazeti la Mwananchi, linatumika ki propoganda zaid.

Kila siku eti mahojiano maalum, mara Ridhiwan mara Lowassa kumbe hawana lolote makanjanja tupu.

Wanaweka picha edited, na jina wanakosea coz Balali hata kwenye pesa hana double ll yaani siyo "Ballali" kama picha inavyoonyesha.

Wazushi wameshindwa..

Meena kafikiri watanzania wrote ni wapumbavu kiasi cha kutojua mambo ya mtandao the whole story is phoney
 
Back
Top Bottom