KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
Nimekwambia Daktari alimsifia JPM kwa kuwa na msimamo thabiti wa kutokuyumba na kufuata mkumbo.
Akasema jambo la kwanza kutokuweka lockdown, pili, kutoa watu hofu kwamba huu ugonjwa huenda tukawa nao mda mrefu au ukaja mwingine hatari kuliko huu lazima tujifunze namna na kuishi nao.
Tahadhari zilichukuliwa, shule zikafungwa, maeneo ya mikusanyiko, uvaaji wa barakoa, vitakasa mikono.
Kingine alichofanya ni kutilia shaka vipimo na kuagiza uchunguzi wa maabara ufanyike. Kitu ambacho alionekana kituko licha ya nchi zingine nazo kukiri kuna shida kwenye vipimo vya Corona.
Tukafungua shule na vyuo huku shughuli za uchumi zikiendelea, kumbuka hayo yote yamefanyika tukiwa tunashutumiwa kuficha taarifa na kusitisha kupima maambukizi mapya.
Rudia tena kuelewa, alichosifia ni kusimamia maamuzi yako akaenda mbali kwa kwamba yeye hata kama mtu anasimamia jambo lisilosahihi anaheshim msimamo. Yeye ni mtu wa Eritrea.
Shida yake na JPM ilikua kwenye kutokutoa taarifa za maambukizi mapya.
Mkuu Monk,
Kwanza nikupongeze kwa kujadili bila kuonyesha mihemko. Naheshimu sana hali hiyo hata kama sikubaliani na unayoyaandika hapa.
Umechambua kwa utaratibu, nami nitakujibu kwa utaratibu huo huo:
1. "Daktari alimsifia JPM kwa kuwa na msimamo thabiti wa kutokuyumba na kufuata mkumbo."
Hili sikubaliani naye na wewe. Ugonjwa huu ni mpya, haukujulikana athari zake zingekuwa zipi. Tahadhari iliyotakiwa kuchukuliwa ni kufuata taratibu zilizopo zinazotumika kwenye magonjwa ya milipuko, huku taratibu zikiendelea kuuelewa ugonjwa ulivyo.
Kiongozi atakuwa na "msimamo thabiti" toka wapi na yeye kujiamria tu kufanya vyake ambavyo hata zile taratibu za kawaida za magonjwa mengine yeye anaona upuuzi?
Swala si "kufuata mkumbo" ni swala la kufuata Taratibu zinazoeleweka katika kupambana na magonjwa ya aina hii. Ugonjwa ulipoanzia, China, walishaonyesha njia na kudhibiti kuenea kwa ugonjwa haraka katika jamii.
Hapa hata wewe unataka kujisahaulisha tu kwamba wakti huo waChina walikuwa wakiletwa hapa kwa ndege kama watalii. Huo ndio msimamo thabiti?
2. "...kutokuweka 'lockdown', kutoa watu hofu-------; lazima tujifunze namna ya kuishi nao."
Elimu ya aina ya ugonjwa huu aliitoa wapi wakati anafanya maamuzi hayo? China walichukua hatua, wakaudhibiti ugonjwa usisambae. Yeye aliona mfano huo kuwa haufai kwa vigezo vipi.
Hadi hii leo, hakuna anayejua kwa nini ugonjwa unaumiza na kusababisha vifo vingi maeneo mengine zaidi ya mengine. Daktari, wewe, au JPM mnaweza kueleza sababu zinazofanya iwe hivyo?
Dunia hii ya leo, ambapo taarifa zinasambaa kwa haraka, mtu atatoaje watu hofu huku ugonjwa ukisambaa duniani kote? Unatoa hofu watu huku ugonjwa huujui kabisa, huna dawa..., unatoa hofu watu kwa kukazania waende makanisani na misikitini na kujifukizia? Kuna sayansi gani hapa inayotoa ushahidi wa uhakika kuwatoa watu hofu.
"Ujifunze kuishi nao" huku huelewi ugonjwa upo vipi na wala hufanyi lolote la mhimu kuudhibiti usienee zaidi kwenye jamii? Unauachia uenee, na madhara yake ya baadae huyajui. Unakubali tu 'ujifunze kuishi nao."
3. Kituko ni hiki "Shule zikafungwa" - Misikiti na makanisa yakafunguliwa?
4. Swala la vipimo ni aibu hata kuliweka hapa. Mtu aliyekwenda shule tena akasoma hadi Ph.D. na tena mwanasayansi. Kama hili nalo wewe mku 'Monk' unaona ni jambo la kujivunia lililofanywa na kiongozi wa nchi, basi sawa.
Hata kama vipimo vingekuwa na mashaka, ile njia iliyotumika ilionyesha ujinga wa hali ya juu sana kuwahi kutokea popote.
5. Huyo Daktari wako alisifia pia tulipositisha kufanya vipimo na kuficha taarifa za ugonjwa? Maana hata hili kwake litakuwa ni "kusimamia maamuzi na msimamo thabiti"? Huyo Daktari wako, umesema toka wapi, Eritrea, mwambie udaktari wake unaweza kuwa wa magumashi, na waajiri wake wakimtambua kuwa ni mtu wa aina hiyo, hata hiyo kazi ataipoteza.
6. Hapo mwisho, Daktari wako atakuwa anajichanganya (contradict) - kwa nini aone shida ya kutotoa takwimu kwa mtu ambaye anamsifia kuwa na msimamo, hafuati mkumbo wa wengine?
Mwisho: ninakuomba, ukiwasiliana tena na huyo Daktari wako, muulize kama COVID-19 imekwisha kabisa Tanzania kutokana na hatua zilizochukuliwa na JPM. Mpe mrejesho kwamba hapa corona haipo tena na hakuna watu waliopoteza maisha yao kutokana na gonjwa hilo.
Mwambie, tulicheza patapotea, tukabahatisha sana, sasa ni wakati wetu kujisifu kwa bahati yetu nzuri hiyo.. Sasa tunaweza kuuambia ulimwengu wote waje hapa kujifunza jinsi ya kushughulikia magonjwa ya aina hiyo pindi yakitokea tena huko mbeleni.