Hawa watu sasa wamekubali kuwa Corona imeisha?

Ungetuwekea tujisomee/tusikie wenyewe aliyosema huyo Daktari.

Kwa hivi ulivyofanya hapa ni kutulisha matango tu na kumfanya huyo Daktari aonekane kama juha fulani kwa kusema maneno kama hayo.

Daktari tulikua tunaongea nae ana kwa ana, pia kuna post inayofuata nimeeleza maswali niliyomuuliza.
 
Unamaanisha nje na nchi ulizozitaja hakuna nyingine iliyoweka lockdown....

Straighten hoja yako usaidiwe majibu?
Hawa mataga wanataka kuwaaminisha watu kuwa Tz pekee ndio hakukuwa na lockdown in all African countries...
 
Daktari tulikua tunaongea nae ana kwa ana, pia kuna post inayofuata nimeeleza maswali niliyomuuliza.
Kwa hiyo unataka nasi tumuelewe kama ulivyomwelewa wewe, bila ya uthibitisho wowote?

Hata jina hana, hata machapisho yanayoweza kuonyesha mwelekeo wake huna? Tukubali tu kuwa Daktari alisema hayo uliyoyaandika?
 
Kweli. Ninawafahamu angalau watu 11 walioipata na kupona baada ya kujidunga mixer za tangawizi, kitunguu swaumu, kitunguu maji, pilipili kichaa na limao. Hii kitu imetuspare waafrica. Wazungu hata flu tu huwaua sana
Kujidunga mixer?
 
Kwa hiyo unataka nasi tumuelewe kama ulivyomwelewa wewe, bila ya uthibitisho wowote?

Hata jina hana, hata machapisho yanayoweza kuonyesha mwelekeo wake huna? Tukubali tu kuwa Daktari alisema hayo uliyoyaandika?
Siyo lazima ukubali alichokisema/ andika.

Unaweza ukakikataa.
 
We vipi
Corona kutokuwepo sasa haimaanishi kipindi kile haikuwepo..
Halafu acheni kufanya kama Afrika nzima Magufuli peke ake hakuweka lockdown..
Nitajie nchi nyingine zaidi ya Kenya,Uganda,Rwanda,South Africa na Nigeria zilizokuwa na lockdown.
Burundi mpaka kesho hata kipimo cha joto la corona hawakuweka na kazi ziliendelea kama kawaida!
 
Mashirika ya Ndege ya kimataifa bado yanaitenga Tanzania ni Ndege chache za kimataifa zinakuja hapo Dsm, nyinyi mnasema corona haipo lakini ofisi za Balozi wana taarifa za kwenye jamii kote wanajua corona ipo kwa wingi.
Hizo balozi zinapata wapi hizo taarifa? Kama sio hisia zao tuu.
 
Kwa hiyo unataka nasi tumuelewe kama ulivyomwelewa wewe, bila ya uthibitisho wowote?

Hata jina hana, hata machapisho yanayoweza kuonyesha mwelekeo wake huna? Tukubali tu kuwa Daktari alisema hayo uliyoyaandika?

Kwani umelazimishwa kuamini nilikiandika?
Jambo moja nalishangaa, nidanganye kwa maslahi ya nani?

Nimeshakwambia hii ni kwamujib wa mazungumzo yetu tena akiwa na mwenzake ambae sio daktari ila ni mwangalizi wa mashirika ya kimataifa.

Huyu Daktari namuongelea hapa anawakilisha WHO na sio mtanzania. Huo ulikua ni mtazamo wake binafsi kuhusu JPM alivyopambana na Covid 19.
 
Jana Russia iliondoa raia wake nchini, us,uk nk wameishaondoa watu wao. Sisi tuendelee kuimba na kumtukuza huyo yesu mpya ila ukweli bado ugonjwa upo na watu wanakufa sana ila haitangazwi. Maisha ni mali yako binafsi unaweza kuwachezea kamali kama utaona inafaa

wewe unasena watu wanakufa. mbona wewe ujafa. watoto wako wako shule hawajafa. mama yako yuko hajafa. mjomba. baba yako.
; shangazi, mke wako, jirani wote hajafa na corona. alafu unasema watu wanakufa.
 
wewe unasena watu wanakufa. mbona wewe ujafa. watoto wako wako shule hawajafa. mama yako yuko hajafa. mjomba. baba yako.
; shangazi, mke wako, jirani wote hajafa na corona. alafu unasema watu wanakufa.
Unazidi kuthibitisha ile tafiti ya twaweza kuwa ccm inawekwa madarakani na wajinga walio wengi sana nchini
 
Kwani Korona nchini haipo?

Kama Haipo mbona serikali inasema tuendelee kuchukua tahadhari?

Sasa ACT kutochukua tahadhari ni kwa sababu ya Magufuli?

Naona contradiction kwenye huu uzi.

Hoja yako ingekuwa na mashiko kama Magufuli angetangaza Korona nchini imeisha halafu wapinzani wakawa wanapinga kisha wakawa hawachukui tahadhari kuonyesha kuwa wanakiamini wanachokisema, hapo tungewaita wanafiki

Lakini sasa hivi Taifa zima linajua Korona ipo lakini hatuchukui tahadhari ya kutosha, Mimi nasema ni UZEMBE ZAIDI KULIKO UNAFIKI
 
Watu laki 6 wamekufa duniani mpaka sasa, maambukizi yanaongezeka. Tumpongeze mtoa mada Kwa msimamo aliokuwa nao tangu mwanzoni.
IMG_20200719_090306.jpg
 
Licha ya msimamo wa s
wanasiasa (aliwemo JPM) kuhusu COVID-19, mwongozo wa serikali na wizara ya afya haujabadlika!
 
Hawa mataga wanataka kuwaaminisha watu kuwa Tz pekee ndio hakukuwa na lockdown in all African countries...
Twambie wewe hizo nchi nyingine,hizo nyege ni za wapinzani mbona tumewazoea tu hamna jema nyie. Nasikia Konyagi tena imewatoa knockout!
 
Sina uhakika sana, ila ngoja niulize.

Je, nchini Tanzania watu wanakufa kama nzi waliopuliziwa dawa ya kuua wadudu?

Maana kwa hivi sasa sioni tahadhari zozote zile zilizopendekezwa zikichukuliwa na watu nchini Tanzania....
Tell me something... ina maana hii ni "blesseing" kwa Tanzania tu au duniani kote watu hivi sasa hawafi kwa corona?!

Kwamba, "je, Tanzania watu wanakufa kama nzi waliopuliziwa dawa ya kuua wadudu?" Ina maana kuna nchi ambako watu wanakufa kama nzi waliopulizwa dawa ya wadudu, au ulikuwa unajaribu kusema nini hasa?!
 
Toka mwanzo na mpaka sasa, msimamo wangu kuhusu hii Corona ni sawasawa na ule wa Rais Magufuli.

Si ajabu pia, kuwa, msimamo wangu waweza kuwa ni mkali zaidi kushinda hata huo wa Rais Magufuli.

Yaani, COVID-19 si hatari kama tulivyoaminishwa. Tumelishwa matango pori.

Jana nilimwona Bernard Membe akienda kuchukua fomu za kugombea urais.

Alipofika hapo ofisini, akasalimiana na mtu kwa kushikana mikono. Sikuona watu wakiwa wamevaa upuuzi wa barakoa. Sikuona watu wakiwa wamekaa mbalimbali.

Wakina mama waliokuwepo walikuwa wakiimba. Inasemekana katika kuimba, vichembe chembe vya mate huwa vinaruka na hivyo kuwezesha kiurahisi maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Kipindi Corona inabamba, hawa watu wa kambi ya upinzani ndo walikuwa mstari wa mbele kumnanga Rais Magufuli kuhusu msimamo wake wa hivyo virusi.

Sasa hebu tazama video hii! Imekuwaje? Hao wapinzani sasa wamekubali kuwa Corona si hatari kivile?

Mpende au umchukie, kiukweli Magufuli kwa misimamo yake lazima umheshimu tu.


Marekani wamekufa laki na zaidi.

Kukataa kukubali uwepo wa tatizo sio jawabubla tatizo.Ni sawa na kunywa pombe ili usahau matatizo yako.

Kilichotakiwa kufanywa ni kupima wote wenye matatizo na kufatilia hatima yao.
 
Huu ushauri uliutoa wakati wa Mkutano mkuu wa CCM Dodoma? Au CCM wana kinga ya kutopata Corona!!!
 
We vipi
Corona kutokuwepo sasa haimaanishi kipindi kile haikuwepo..
Halafu acheni kufanya kama Afrika nzima Magufuli peke ake hakuweka lockdown..
Nitajie nchi nyingine zaidi ya Kenya, Uganda, Rwanda, South Africa na Nigeria zilizokuwa na lockdown.
Tatizo sio hilo tatizo mlikejeli mkasaidiwa na kenya kuona jpm kakosea
 
Kuna magonjwa mengi tu tunayo miaka nenda miaka rudi na yamepoteza sana ndugu zetu ila maisha yanaendelea,sasa kwenye corona tulitegemea tungeona tofauti kwa kuwepo hali isiyo ya kawaida kwenye wingi wa watu kuumwa na hadi vifo. Na hali hiyo ingetufanya tusiendelee kuishi maisha yetu yaleyale ya siku zote kabla ya corona.
 
Back
Top Bottom