Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,227
- 113,583
Toka mwanzo na mpaka sasa, msimamo wangu kuhusu hii Corona ni sawasawa na ule wa Rais Magufuli.
Si ajabu pia, kuwa, msimamo wangu waweza kuwa ni mkali zaidi kushinda hata huo wa Rais Magufuli.
Yaani, COVID-19 si hatari kama tulivyoaminishwa. Tumelishwa matango pori.
Jana nilimwona Bernard Membe akienda kuchukua fomu za kugombea urais.
Alipofika hapo ofisini, akasalimiana na mtu kwa kushikana mikono. Sikuona watu wakiwa wamevaa upuuzi wa barakoa. Sikuona watu wakiwa wamekaa mbalimbali.
Wakina mama waliokuwepo walikuwa wakiimba. Inasemekana katika kuimba, vichembe chembe vya mate huwa vinaruka na hivyo kuwezesha kiurahisi maambukizi ya magonjwa mbalimbali.
Kipindi Corona inabamba, hawa watu wa kambi ya upinzani ndo walikuwa mstari wa mbele kumnanga Rais Magufuli kuhusu msimamo wake wa hivyo virusi.
Sasa hebu tazama video hii! Imekuwaje? Hao wapinzani sasa wamekubali kuwa Corona si hatari kivile?
Mpende au umchukie, kiukweli Magufuli kwa misimamo yake lazima umheshimu tu.