Hawa watu sasa wamekubali kuwa Corona imeisha?

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
7,339
2,000
Corona ipo ya kutosha hususani hapo Dsm wagonjwa wanafia majumbani Hosptal ndogo ndogo na hata wakifa ndugu hawasemi ni corona huficha siri kwa hofu ya kutengwa na jamii
Hivi huo ugonjwa ungekuwa upo wa kutosha kwa maana umeenea sana hivi kweli kungekuwa na kuogopa kutengwa na jamii?
Maana kama huo ugonjwa upo na watu wana uguwa sana sasa iweje tena iwe siri na kuogopa kutengwa wakati jamii yenyewe inasumbuka na huo ugonjwa,sasa huyo mwenye kumtenga mwenzei ni nani?
 

Aladeen04

JF-Expert Member
Sep 6, 2016
1,199
2,000
Kwa mujibu wa mbunge mstaafu wa Chatto jana, ni rasmi kuwa Tanzania Corona sasa hivi ni historia.

Hata hivyo inafahamika kuwa juzi imemwondoa mfanyakazi mmoja wa idara ya afya tokea jimbo hilo hilo.

Kushoto au kulia, ajuaye ni mzee baba peke wengine hawa mavuvuzela tu.
Tuendelee kuchukua tahadhari.
 

double R

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
2,248
2,000
Nakubaliana na hoja nafikiri serikali nyingi wanaogopa kubadilisha direction lakini kwa makadirio ya awali sasa watu mamilioni wangekuwa wamefariki kwa COVID-19 duniani badala yake vifo havijafikia milioni. Na hakuna nchi yenye uwezo wa kusema ili contain kabisa.
 

boma2000

JF-Expert Member
Oct 18, 2009
3,288
1,500
Toka mwanzo na mpaka sasa, msimamo wangu kuhusu hii Corona ni sawasawa na ule wa Rais Magufuli.

Si ajabu pia, kuwa, msimamo wangu waweza kuwa ni mkali zaidi kushinda hata huo wa Rais Magufuli.

Yaani, COVID-19 si hatari kama tulivyoaminishwa. Tumelishwa matango pori.

Jana nilimwona Bernard Membe akienda kuchukua fomu za kugombea urais.

Alipofika hapo ofisini, akasalimiana na mtu kwa kushikana mikono. Sikuona watu wakiwa wamevaa upuuzi wa barakoa. Sikuona watu wakiwa wamekaa mbalimbali.

Wakina mama waliokuwepo walikuwa wakiimba. Inasemekana katika kuimba, vichembe chembe vya mate huwa vinaruka na hivyo kuwezesha kiurahisi maambukizi ya magonjwa mbalimbali.

Kipindi Corona inabamba, hawa watu wa kambi ya upinzani ndo walikuwa mstari wa mbele kumnanga Rais Magufuli kuhusu msimamo wake wa hivyo virusi.

Sasa hebu tazama video hii! Imekuwaje? Hao wapinzani sasa wamekubali kuwa Corona si hatari kivile?

Mpende au umchukie, kiukweli Magufuli kwa misimamo yake lazima umheshimu tu.


Kumbe ameombwa na Zitto na Sharif agombee Urais siyo mahaba yake. Chama mufilisi
 

Nguruvi3

Platinum Member
Jun 21, 2010
13,860
2,000
Safi!

Unakihusisha kifo cha Mkapa na COVID-19?
Mkuu huu uzi ulikuwa na swali la kufikirisha sana. Ilikuwa ngumu kusema lolote kwangu.
Niliona Wapinzani na CCM wakiwa na harakati kama zile za mkutano mkuu wa Chama Dodoma.

Nilijiuliza sanahivi hawa south Africa wametofautiana nini na sisi?
Hakuna cha Barakoa (mask) au social distancing . Wazee na Vijana kuserebuka tu kwenda mbele

Nilikuwa naufuatilia sana huu uzi ingawa watu walifanya mzaha, mimi niliufuatilia sana
 

Nyani Ngabu

Platinum Member
May 15, 2006
86,884
2,000
Mkuu huu uzi ulikuwa na swali la kufikirisha sana. Ilikuwa ngumu kusema lolote kwangu.
Niliona Wapinzani na CCM wakiwa na harakati kama zile za mkutano mkuu wa Chama Dodoma.

Nilijiuliza sanahivi hawa south Africa wametofautiana nini na sisi?
Hakuna cha Barakoa (mask) au social distancing . Wazee na Vijana kuserebuka tu kwenda mbele

Nilikuwa naufuatilia sana huu uzi ingawa watu walifanya mzaha, mimi niliufuatilia sana
Well, tataona namna ambavyo mazishi yake yatakuwa.

Hapa Rais mstaafu Kikwete akimzungumzia marehemu Rais mstaafu Mkapa.

Sioni barakao wala social distancing.


Tundu Lissu naye anarudi wiki ijayo. Tutaona atavyopokelewa...
 

Tz mbongo

JF-Expert Member
Mar 12, 2015
7,339
2,000
Unajua kuna vitu vinafurahisha maana kwa jinsi corona tulivyokuwa tunaisikia kwa nchi za wenzetu huko ni ajabu kwamba hapa tunabishana kuwa et corona bado ipo nchini au haipo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom