Hawa watu Mbezi Mwisho wanatumia kivuli cha Bahati Nasibu kuwaibia watu

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Ndugu zangu katika pitapita zangu nimefanikiwa kufika mitaa ya Mbezi Luis karibu na ilipo Stendi ya Mabasi ya Magufuli, nadhani ile ni Kata ya Mbezi, kuna mambo kadhaa yanaendelea yanayohusu utapeli kama ilivyo kawaida kunapokuwa na purukushani za watu Jijini Dar.

Karibu na Daraja la kuelekea Stendi ya Magufuli, kuna wizi unaendelea lakini wahusika wanajificha kwa kivuli cha Bahati Nasibu.

Wanaoibiwa asilimia kubwa ni kina mama, hao wezi wameweka maspika makubwa na kuna makorokoro mengi, wanachofanya unachagua namba ili upate vitu, waliozunguka ni wengi na ukishiriki michezo hiyo wanakuibia.

Nashauri viongozi wa maeneo hayo waangalie, wasiruhusu wizi huu uendelee, wanaoteseka kwa asilimia kubwa ni Wanawake wanaotoka nje ya Mji, kwa kuwa matapeli waliopo hapo wanawatumia Wanawake wenzao kuigiza kama vile nao wanashiriki kume ni michezo ya tu.

Ndio maana wenyeji wengi hawashiriki michezo hiyo kwa kuwa wanajua kinachoendelea ni utapeli, wanaopigwa wengi wao ni Wageni.

Hata kama wanapewa vibali na Serikali za Mtaa au Wilaya hao watu waangaliwe matendo na mtukio yao, wasitumie kivuli cha bahati nasibu kuzingua.
 
Acha wajinga waendelee kuwa mtaji wa watu wachache wenye akili.
Je wanalazimishwa kujihusisha na mambo hayo?

Binadamu mwenye akili finyu ni mtaji wa mwenye akili nyingi.
 
Nishawai leta vurugu hadi hawana hamu na mimi. Ilikua mwanza miaka fulani wakanichezea janja wakasepa na pesa. Nikapanda mlimani kurudi na wahuni. Wahuni walisomba kila kilichopo mbele
 
Waache wakaribishwe mjini mkuu inawezekana pia ni mpango WA serikali yetu pendwa maana kama sivyo mbona Kuna mashindano ya kuweka buku upate Mamilioni tena redioni na michezo mingine ikiitwa michongo pesa ila nyumbu Bado zipo
 
Dah! Watu wanaibiwa sana
Walikuwepo hapa karibu na stand ya malamba, mbezi luis ndo wakahamia hapo maguful darajan
Na hivi ninavyoandika hii mesej wamerud tena karibu na hii stand ya malamba
 
Ndugu zangu katika pitapita zangu nimefanikiwa kufika mitaa ya Mbezi Luis karibu na ilipo Stendi ya Mabasi ya Magufuli, nadhani ile ni Kata ya Mbezi, kuna mambo kadhaa yanaendelea yanayohusu utapeli kama ilivyo kawaida kunapokuwa na purukushani za watu Jijini Dar.

Karibu na Daraja la kuelekea Stendi ya Magufuli, kuna wizi unaendelea lakini wahusika wanajificha kwa kivuli cha Bahati Nasibu.

Wanaoibiwa asilimia kubwa ni kina mama, hao wezi wameweka maspika makubwa na kuna makorokoro mengi, wanachofanya unachagua namba ili upate vitu, waliozunguka ni wengi na ukishiriki michezo hiyo wanakuibia.

Nashauri viongozi wa maeneo hayo waangalie, wasiruhusu wizi huu uendelee, wanaoteseka kwa asilimia kubwa ni Wanawake wanaotoka nje ya Mji, kwa kuwa matapeli waliopo hapo wanawatumia Wanawake wenzao kuigiza kama vile nao wanashiriki kume ni michezo ya tu.

Ndio maana wenyeji wengi hawashiriki michezo hiyo kwa kuwa wanajua kinachoendelea ni utapeli, wanaopigwa wengi wao ni Wageni.

Hata kama wanapewa vibali na Serikali za Mtaa au Wilaya hao watu waangaliwe matendo na mtukio yao, wasitumie kivuli cha bahati nasibu kuzingua.
Huo utapeli upo tangu early 90s, kama kuna MTU anaibiwa Leo, huyo kaja mjini Jana,
Wandugu! Surely unafikiri kuna mtu, taasisi inanaanzisha michezo ya kubahatisha ili kutajirisha watu! Kama unawaza hivyo, wewe fika mirembe upimwe kichwa!
Michezo yote ya kubahatisha, inajitajirisha yenyewe! Wajinga ndio waliwao.
 
Hapo ndio unaambiwa karibu mjini. Hao jamaa ni kikundi kikubwa unawezs kusema ni wapita njia kama wewe kumbe wako kutapeli watu
 
Back
Top Bottom