DOKEZO Kwa mara nyingine tena Kituo cha Daladala Mwisho Mbezi Luis hakuna mwanga, taa zimezima usiku

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
Kama kawaida Kituo cha Mbezi Luis maarufu kwa jina la Mbezi Mwisho, leo tena Agosti 11, 2023 hakuna mwanga, giza limetawala na kusababisha usumbufu mkubwa wa watumiaji.

Hii sio mara ya kwanza wala ya pili kwa hali hii kutolea katika Kituo hiki kilichopo karibu na Stendi Kuu ya Mabasi ya Magufuli hapa Dar es Salaam, ajabu ni kuwa sehemu nyingine zinazozunguka Kituo hiki Kuna umeme.

Jamii Forums tusaidieni kipaza sauti hiki Kituo kina changamoto gani kwani mbona ni hapa tu mara kwa mara, nimeshuhudia abiria wengi wakiwemo Wanafunzi wanavyopata ugumu kupigania magari kukiwa na giza.

Mazingira kama haya yanatengeneza nafasi nzuri kwa vibaka na wahalifu wengine kufanya yao.

IMG_20230811_190423_176.jpg

IMG_20230811_190415_157.jpg

IMG_20230811_190503_491.jpg
 
Hebu fatilieni vizuri uongozi wa kituo, huenda wananufaika na hali hiyo.

I mean huenda wameandaa vijana wao ambapo kila wanapozima taa vijana hao hufanya kazi ya kupiga ndole abiria waliopo kituoni hapo, na baadae kuletewa, kugawana au kupozwa na wapiga ndole hao.
 
Ngoja nisogee apo chapa najua nakavzia kadada nakapora simu nikila chocho sionekani na giza hilo dah kesho weekend inaisha vyeMa
 
Nchi hiii safar ni ndefu saanaa!Hata nyegeza mara nyingi hakunaga umeme

Kazi ipo sana
 
Back
Top Bottom