... tupo tu tumeuchuna, si unajua tena siku zenye ma breaking news kama leo... noma tupu..
...sasa nyie masela, nani anamkumbuka jamaa mmoja hivi pale Tambaza alikuwa anaitwa Meja, jamaa alikuwa mnoko huyoo usiombee, alikuwa prefect wa maswala ya misosi....mbona tulikuwa tunakoma siye mafreshers pale, jamaa kwa vile alivyo lazima tu alienda kupapa kazi jeshini, niaminini mimi... mdude ule ulikuwa nuksi, fullstop!
...lakini pia wakati wa mgao wa misosi pale Tambaza, kuna jamaa mmoja alijitokeza, tulikuwa tunamwita Chua (chuwa), jamaa naye alikuwa nuksi kichizi kwenye maswala ya misosi, yeye wala hakuwa prefect, lakini connection zake kule jikoni na ukiwa kundi moja naye lazima muibuke na sinia kama 3 hivi za wali na nyama, hali wengine wakiangulia vibakuli tuu... jamaa alikuwa hana mchezo, siku nyingine kukiwa msosi hautoshi wanafunzi halafu unamkuta amefanikiwa kupata walau plate moja, jamaaa alikuwa anatemea mpunga wote na mate, ili mtu asimsogelee... lakini kuna machizi vile vile nakumbuka hilo halikuwa sooo kwao, walikuwa bado wanautwanga wali ule pamoja na kutemewa mate...nomaaaaaa... halafu chizi yule siku amekuruhusu kula msosi wake, ukishiba na kutaka kuondoka anakuambia 'lete mikono hiyo', kama hujaelewa unaweza anza shangaa shangaa, kumbe jamaa walikuwa wanamaanisha kuleta mikono hiyo 'na kulambwa', ili mradi tu usiondoke na punje hata moja... daaaah, kweli siku hizo nazimiss kichizi masela wangu..