Hawa wako wapi sasa?

Hawa wako wapi sasa?

Duuh humu jf kuna mabronz na masistery wangu kibao shikamooni wakubwa japo nilikua mdogo ila kuna vitu nimekubuka vingi sn.
 
Topic hii ilianza vizuri lakini wameharibu walioanza kuingiza mambo ya shule, hapa tunaongelea Ma Mcs wa OldSkul wa Bongo,
Je nani anajua kwamba kulikuwa na Beef kati ya Salehe Jabir a.k.a Cool S na Adili Kumbuka The late Nigger One ( R.I.P) walishakutana fainali mara mbili Lang'ata kwenye mashindano ya Yo Rap Bonanza mara moja akshinda Nigger One mara ya pili Cool S hope so na nilikuwa nina tape ya mashindano hayo but so sorry kuna mtu alinizima
nigger One alikuwa anachana kiingereza sana na kishwahili kidogo nadhani hapa IST ilikuwa inachangia na alikuwa anamanda salehe kwa kuimba kiswahili na Salehe alikuwa mbaya kwenye kiswahili lakini alikuwa anacopy au anabadilisha nyimbo za wanamuziki wa nje kutoka kiingereza kuwa kiswahili. mfano nyimbo ya vanilla Ice, Black Box mfano ni mistari hiyo hapo chini;

....'Ice ice Baby nipo nipo na maprino invasion kitu kimenikaa moyoni na sasa naamua kukitoa mdomoni, werastop yoo I dont know kusema mengi naona choo, nipo kwenye steji nayakata madebe dance ngoma hii ya ajabu........ cassete ya Salehe jabir ninayo mpaka leo huwa naisikiliza na kucheka sana.

hizo verse kama ulikuwa hajazishika ilikuwa ngumu kuchukua totoz kwani ndio ulikuwa ujanja nakumbuka kuna mchizi primary madem walikuwa wanamfuata na kmwomba awashushie hiyo mistari yaani ilikuwa soooo.

Kitu kingine wadau wa Old Skul kulikuwa kuna dada mmoja tu ndio alikuwa anashika kipaza kitambo hicho naye alikuwa anaitwa Tass alikuwa anasoma IST huyu alikuwa anashiriki Yo Rap Bonanza alikuwa anakaa mitaa ya Obay.


All in all kulikuwa na wakali wengine kibao kama wakina Mc Cux, Dj Cux, fresh XE, ...... HiPhop was hot those days sio sasa wabana pua wengi

Mkuu zi upload youtube maana hata mimi sikumbuki tape yangu ilivyo japo ninazo nyingi sana na siwezi sikiliza zote oi

https://www.reverbnation.com/ngomanagwa/song/15363709-saleh-jabir-opp
 
Ebwana unakumbuka enzi za PUZA WA TAMBAZA?

what about mamabo ya DON BOSCO tournament?

Hapo kwenye red, dahhh Don Bosco Zanaki na Tambaza


enzi za aaah msela mimi nampenda msela ingawa hana hela msela aaaaah msela
mmmmmh mselaaa.

We jamaa ni mwana Tambaza nini!umenikumbusha mbali sana,Puza alifariki 1991 akiwa form 2,Miaka hiyo ndio miaka ambayo Kwanza unit ilianza,Tambaza alikuwepo member wa KU,aliyekuwa anaitwa Y Thang nakumbuka verse yake.Nikifa hakuna matanga juu weka panga,Y nasema Hi natoa rai, za kimasai...Enzi hizo Ras Kalikawe (R.I.P)anaishi jirani na Tambaza sec,baadae wakaja Diplomats,wakina Saigon.Kweli miaka inakimbia
 
Cha ajabu hawa jamaa wote waliotajwa wengi walishafika marekani..lakini kwa sasa ni ngumu kwa nyandu toz au stamina kwenda ata burundi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom