Game Theory
Platinum Member
- Sep 5, 2006
- 8,545
- 835
Wewe wewe brazameni... mbona hivyo jamani ndugu.... unanikumbusha mbali sana..
brazameni, kama unakumbukumbu na hayo yote, miye naomba kukuuliza kuhusu watu wawili tu; nawo ni Mwamba Ng'andwe na Cool James. Mwamba Ng'andwe alikuwa ni Mzambia alikuwa anatumia jina la Wizz Kidd, alikuwa anapiga beatbox kwa sanaa, na Cool James ninachokumbuka alikuwa anakaa Chuo Kikuu kule chini chini (makongo sijui kule)... Sasa je una habari hata kidogo kuhusu hawa jamaa?!
Nitashukuru sana ukinifahamisha.
SteveD.
Pia, Je unajua kuwa akina Cool Mo C, Fresh X, na KBC walikuwa members wa RAPPORT, way back kabla hata ya Kwanza Unit, kituo chao kilikuwa pale kwenye quarters karibu na Tazara Club, na chimbuko lake ni Tambaza Sec na member mwingine namkumbuka kwa jina la Kevin.....
Duuh, umenifanya ni travel down memory lane leo... ahsante.. usione tumekaa kimya ndugu yangu, wengine tulikuwemo humo kwenye misafara yao...lol
... pia hapo juu naona hujamtaja, Rob Mwingira -DRob (RIP)
SteveD.
Brazameni bwana kwa vituko, mbona wapo masela ambao pia ni ma-joni kisomo? wanajulikana kama "educated gangsters" ndio hao akina Y-thang na wengineo........ghorafa ya saba ilikuwa ni kijiwe poa, pia unakumbuka mambo ya pool side?
Dela soul siku hizi anajulikana kama "Balozi," hao watu wa roots wapo wengi.....sister 'ake nigga one mara ya mwisho alikuwa DC.....je wewe ulikuwa mshabiki wa PAZI au VIJANA??
Namjua Ally Mrisho, yule mluguru mshenzi sana, yaani bado kidogo tu na mie angekula pesa yangu. Kwenye hiyo Trip ya '95 ulikuwa na kina Tiff nini? Watoto flani hivi wa Kinondoni walikuwa "mazungu wa mbwimbwi", jamaa wamelikita hapo NYC.
Ndio mzee Malai wa Pazi(RIP) alivuta na kile kisukari. Kwahiyo utakuwa unamjua Yassini Wassira, jamaa alikuwa ndio Bigman wa Pazi......nakumbuka sana mambo ya Indoor na kina Zonga!!!.
Bills pale mie nilikuwa nanunua bia nje kwenye vibanda vya 'chinga halafu naimbuka nazo ndani ili kusave kidogodogo............mzee umenikumbusha mbali sana, mambo ya St. Albans na safari za mtoni!!.
Wengi watakuwa Dar Exit tu au "friji open na geti kali", kwahiyo misukosuko ya mjini hawaijui.
Mie mwenyewe baadae nilikuwa nabamiza sana bank statement "kajanja" pale salamander, sticker za bima na fax kinyago baada ya bomu la Osama.....yote hayo nikiwa mwanafunzi chuo. Ile ya Osama nayo ilileta neema maana watu kibao waliondoka kwenda kwa UK kwa gia ya kuchukua Visa ya US.
KBC
http://myspace.com/mrkbc
Picha ulizoziweka mwanzo ziko kwa KBC, na uhakika ukiwasiliana nae utapata majibu yako kuhusu KU. Kuna jamaa mwingine nadhani alikuwa KU yupo UK somewhere, nina muda sijawasiliana nae.
HBC - Prof. Jay yupo. Wengine sijui.
Ningependa kupata hizo video ulizozitaja mazee.
Sugu
http://www.myspace.com/mr2sugu
Halafu unakumbuka miaka ile IDDI JANGUA alivyokuwa akitesa kule coco beach full CHICAGO BULLS kuanzia CAP mpaka soksi na raba?
sasa unapajua NGAZI TANO? ni huu upande wa MKWEPU nyuma ya kwa Khery wa magazines ambaye naye pale si unajua tulikuwa tunajipatia ma RIGHT ON na WORD UP
Halafu unakumbuka miaka ile IDDI JANGUA alivyokuwa akitesa kule coco beach full CHICAGO BULLS kuanzia CAP mpaka soksi na raba?
Kuhusu Upanga miye namkumbuka jamaa mmoja alikuwa anajiita Cool, alikuwa mitaa ya katikati hivi nadhani walikuwa na garage ya magari, jamaa alikuwa anapenda Ragga music...Umezungumzia kuhusu UPANGA
Enzi za kina Puza (RIP) nakumbuka, akina Manyau na akina Tyson... kijiwe chao kilianzia pale kwenye fence ya Tambaza na magorofa ya upande wa Muhimbili, kijiwe kilianza kimchezo mchezo tu katika harakati za kuwa onea Azania baadae likawa soo kubwa dhidi ya walimu pale pale Tambaza...Ebwana unakumbuka enzi za PUZA WA TAMBAZA?
brazameni, wengi tu hapa wanafahamiana, na wengi tu ni watoto wa DAR, ila kama jinsi tulivyo binadamu, wengine wakimya wengine waongeaji sana... hivyo kuna wengine wanayajua haya yote unayo ongelea humu na wanafahamiana na wale unaowataja, ila ndiyo hivyo tena, hayo ni yao na ndugu, jamaa au rafiki zao... siyo ya ku share na kila mmoja hapa ukumbini!I wish QUICK MOVER ainie humu maana naye ni mmoja kati ya wachache wa JF ambao ni watoto wa DAR
Kabla ya Poolside, clouds disco lili hamia kwanza pahala fulani hivi opposite na Empire... kisha disco likawa lina hama hama na kati ya hapo na Twiga hotel (wakati huo), kabla hawajajigawa na kuanza kupiga Mayenu Tazara club...Ebwana kati ya vitu vilivyokuwa vikiniboa na POOLSIDE ni kile kiwinta cha saa tisa usiku ...kisha inabidi tukanyage miguu kwenda kule NDANI YA NYUMBA aka BILLS aka KWA CHALE MBOWE ambaye of course nadhani uanjua kama alimaliza almost shule nzima ya ZANAKI(lakini wale wazuri tuu) aka BILICANAS aka KWA KAKOBE
Nazungumzia hawa JF in house politicians wanna be ndio walikuwa Joni visomo na nahisi 99% yao walikwenda Jeshini kama si RUVU basi walikuwa MAKUTUPORA
najaribu kujiuliza hivi mwanaijiji na hawa vijana wengine humu ndali sijui walikuwa wapi enzi hizo
Heri wa Magazeti alikuwa mshkaji sana, pale kulikuwa na mafundi baiskeli na wachonga mihuli mbele ya duka la miwani....duh longtime yaani. Kwenye ngazi za kupanda Dar Chamber of Commerce, kulikuwa na fundi viatu mmoja mchaga.... namjua, naye kuna kipindi flani alikuwa anaingiza wakuja town kwa mzushi sana, kwani ile ilikuwa bosheni!!. Sisi tulikuwa na ofisi ya kizushi kule uwani ya mambo ya clearing and fowarding. Heri nasikia hayupo tena pale na salamander haipo tena!!!. Msofe(mpare)bank statement feki....alikuwa na ofisi yake kwenye basement jengo la opposite ya salamander kwa mtaa ule nadhani ni mansfield. Musa"fidodido" yupo NYC kesha kuwa gwiji, nilimwona mara ya mwisho Harlem mwaka '99. Hivi ulisha wahi kula ile mama ntilie pale palipokuwa magoti?? kwikwikwi, mlango gunia, lazima upige chabo (shoto,kulia)ili watu wasikuone ukiingia kula ugali wa kukata!!!. Unamjua Peter(PITAKULE), mchizi flani alikuwa ana-hang sana mitaa ile akitafuta safari............Ally Mrisho nasikia mwishowe alidhulumu watu, wakaamua kumtembezea "pira", lakini mwanga kichizi....yaani kesi zinakufa bila yeye kuchukuliwa hatua yeyote, jamaa walikuwa na plan ya kumfanyizia, lakini hata sijui iliishia wapi.
Kuna mshkaji mmoja nilikutana nae pale, alikuwa jamaa wa wale wachonga mihuri......jamaa alikufa mwaka jana. Yeye na mdogo wake walikufa maji Houston,TX......sijui kama unamjua?!!!.