Hawa wako wapi sasa?

Game Theory

JF-Expert Member
Sep 5, 2006
8,545
833
Mtanisamehe lakini najua wengi wenu humu JF mlikuwa Joni visomi na najua pia kuwa ambao hawakusoma mlikuwa mabaharia,na of course wengi wenu mnatokea mikoani na Dar mekuja miaka 1- iliyopita... lakini vile vile nilitaka kuwafahamisha kuwa early 80's kulikuwepo hili kundi la KU na sie wengine tulikuwepo siku ile ya jumamosi walipokuja CINE CLUB kurekodi video yao ya MSELA



ku1.jpg

176069136.img.jpg

176069062.img.jpg



Masela hawa wako wapi sasa...!!

Kwa wale tuliokuwa tukifwatilia kwa karibu muziki huu wa kizazi kipya wakati unaanza kuchipua,tutaungana mkono kuwa vijana walitokea mbali kiana na bila shaka katika harakati zao za kuukuza muziki huu walikutana vizingiti vingi na vya kila aina,mfano naweza kumtolea rafiki yangu Robert ambaye ilifikia wakati wazazi wake wakawa wanaingia na Radio zao chumbani ilimradi tu kumnyima bwana mdogo haki zake za msingi tena za kikatiba za kusikiliza muziki aliokuwa akiuf*gilia eti kwa maelezo kuwa muziki huo ni wa kihuni na usiokuwa na maadili hata kidogo.


Hapa kushoto ni KU Crew,katikati ni Terry kutoka HBC na kulia ni Mr II.Enzi hizooooo


Lakini kadri miaka ilivyokuwa ikizidi kusonga na wasanii kuendelea kuwa wabishi na kuachia mipini mipya tena kwa hela ya ngama waliyokuwa wakiidunduliza kwa taaabu kubwa, huku wakiwa hawapati maslahi yoyote ya maana zaidi ya ujiko tu...hatimaye wasanii walianza kuongezeka taratibuu jambo lililokuwa likiwachanganya zaidi wazazi wengi waliohisi vijana wamechanganyikwa.


Left ni Saigon na katikati ni Dola Soul kutoka the Diplomatz,kulia kwao ni Mr Paul...enzi hizoooooo


Yote hayo yalichangiwa na wengi tu kuanzia waandishi,vituo vya radio, mapromoter na kadhalika.....Jambo kubwa la kujiuliza wengi wa waanzilishi wa vita hiyo kubwa ya kuupigania muziki huu hawajulikani walipo.

Na leo hii itakuwa si vibaya hata kidogo tukiweza kuwakumbuka kwa pamoja wachache tu ambao mchango wao hata kama ni mdogo lakini umeweza kuifikisha Bongo Flava hapa tulipo na kuweza kuufanya muziki huu uwe kioo cha muziki wa vijana kwa Afrika Mashariki na Kati.


Hapa kushoto ni Caz T kutoka (BANTU POUND GANGSTER),katikati ni Bonny Harmony kutoka(AFRO REIGN),na kulia ni Rashid Ziada (KR) kutoka GWM ambaye pia ni mwasisi wa kundi la Wanaumeela TMK.


Kati ya tutakao wakumbuka wengine wanaendelea na muziki na wengine hatuko nao duniani kwa sasa, wengine hatujui walipo na wanafanya nini! tunajua wengi wangependa kujua wako wapi maselaaaa?



JE UNAWAKUMBUKA MASELA HAWA ?

Saleh Jabir
Adili a.k.a. Nigga One (R.I.P)
Afro Reign
K. U Crew
Bantu Pound
4 Kreuz Flava
Hard Blasters
Weusi Wagumu Asilia3
Sos B (ameongezwa na tony-serena znz)
Rhymson (KU Crew)
E-Attack
Fresh X
Kool Mooccc
Columba Mwingira - mawingu Band
OJ - Mawingu Band
Sindila
De-Plow-Matz
II Proud
G.W.M.


WATANGAZAJI WA RADIO (RADIO 1)
Master t
Mike mhagama


MAPROMOTER
Kim Magomelo (Kim & the Boyz)


STUDIOS
Container la Master J
Don bosco Studios
Sound Crafters


Je unazikumbuka video hizi za kwanza kwanzaaaaaa ?
1.Oyaa Msela oyaaaaa (Mawingu Band)
2.Usiige mambo ya mjini (Hard Blasters)
3.Kukurukakara zako (Sos B)



KUMBI
Kilimanjaro pool side
FM Club (zamani Lang'ata Social Hall)
Silent Inn club (umeongezwa na Frank Suura)
 
Wewe wewe brazameni... mbona hivyo jamani ndugu.... unanikumbusha mbali sana..

brazameni, kama unakumbukumbu na hayo yote, miye naomba kukuuliza kuhusu watu wawili tu; nawo ni Mwamba Ng'andwe na Cool James. Mwamba Ng'andwe alikuwa ni Mzambia alikuwa anatumia jina la Wizz Kidd, alikuwa anapiga beatbox kwa sanaa, na Cool James ninachokumbuka alikuwa anakaa Chuo Kikuu kule chini chini (makongo sijui kule)... Sasa je una habari hata kidogo kuhusu hawa jamaa?!

Nitashukuru sana ukinifahamisha.


SteveD.
 
Pia, Je unajua kuwa akina Cool Mo C, Fresh X, na KBC walikuwa members wa RAPPORT, way back kabla hata ya Kwanza Unit, kituo chao kilikuwa pale kwenye quarters karibu na Tazara Club, na chimbuko lake ni Tambaza Sec na member mwingine namkumbuka kwa jina la Kevin.....

Duuh, umenifanya ni travel down memory lane leo... ahsante.. usione tumekaa kimya ndugu yangu, wengine tulikuwemo humo kwenye misafara yao...lol


... pia hapo juu naona hujamtaja, Rob Mwingira -DRob (RIP)



SteveD.
 
Kuhusu studio!
Soundcrafters ipo na inaendeshwa na akina Bizzman na wenzake na inafanya vizuri sana katika kutayarisha muziki!
Master J anaendelea kuwaandalia vijana muziki,katika studio yake ya MJ, ingawa sasa amekuwa na malalamiko kwamba vijana wanampelekea kazi nyingi sana kiasi kwamba amekuwa bize sana, na vijana hao wanataka kazi zao kwa haraka iwezekanavyo ili "Watoke", bila kujali kwamba inatakiwa ziandaliwe kwa ubora unaokidhi soko!
 
watoto wa Mjini utawajua tuu...thread imetazamwa na watu kibwena lakini wote wameingia mitini for simple reason walikuwa bado wako countryside wanawinda ndezi au walikuwa wako UD wanaandamana...na ni bora maana waatu tutajuana na tunaweza tukacheza santuri moja wale joni visomo wakija noma wataaanza na mamabo ohhh tunabaguliwa ohhh tulipanda meli ohh sijui nini yaani tabu tupu

Ebwana Rhymson nakumbuka alipata demu wa kijamaica ambaye ni mcanada na aliondoka naye lakini mara ya mwisho nilionyeshwa picha yake sikuamini jamaa naona ana kwenda kama YAAA'DI BWOY...au kuliko maana kawa mzee wa ROOTS

Ebwana hivi kati yenu nani alikuwa nakwenda GHRORFA ya SABA?
 
Wewe wewe brazameni... mbona hivyo jamani ndugu.... unanikumbusha mbali sana..

brazameni, kama unakumbukumbu na hayo yote, miye naomba kukuuliza kuhusu watu wawili tu; nawo ni Mwamba Ng'andwe na Cool James. Mwamba Ng'andwe alikuwa ni Mzambia alikuwa anatumia jina la Wizz Kidd, alikuwa anapiga beatbox kwa sanaa, na Cool James ninachokumbuka alikuwa anakaa Chuo Kikuu kule chini chini (makongo sijui kule)... Sasa je una habari hata kidogo kuhusu hawa jamaa?!

Nitashukuru sana ukinifahamisha.


SteveD.


sasa STEVE D i can out your misery to rest kuhusu yule kijana wa kizambia

Alikuwa anakaa mikocheni B na nadhani Quick moveratakuwa anamjua ...jina lake ndio alikuwa anaitwa MWAMBA na alikuwa IST na ADILI KUMBUKA ambaye alifariki kwenye ajali ya gari...sijui kama ile sanamu ya Adili bado ipo pale IST lakini ndio hivyo...MWAMBA na alidi wote walikuwa wnaishi Mikocheni B adili alikuwa akikaa kule karibu na shule ya Ushindi na of course dada yake marehemu alikuwa anaitwa MANDIA niliwahi kumtokea lakini ahhh nikaishia njiani unajua tena nilikuwa bado sijaqualify kama full player enzi hizo

MWAMBA alikuwa anjiita DJ WHIZZ

halau huwezi kuamini wiki mbili zilizopita nilikuwa na SALEH JABIR kwenye Hitma London na jamaa kaoa, ana makidi wawili, hajabadilika sana sema kawa menene tuuu halafu amekuwa mtu wa ma ICT
 
Pia, Je unajua kuwa akina Cool Mo C, Fresh X, na KBC walikuwa members wa RAPPORT, way back kabla hata ya Kwanza Unit, kituo chao kilikuwa pale kwenye quarters karibu na Tazara Club, na chimbuko lake ni Tambaza Sec na member mwingine namkumbuka kwa jina la Kevin.....

Duuh, umenifanya ni travel down memory lane leo... ahsante.. usione tumekaa kimya ndugu yangu, wengine tulikuwemo humo kwenye misafara yao...lol


... pia hapo juu naona hujamtaja, Rob Mwingira -DRob (RIP)



SteveD.

Halafu unakumbuka miaka ile IDDI JANGUA alivyokuwa akitesa kule coco beach full CHICAGO BULLS kuanzia CAP mpaka soksi na raba?


Umezungumzia kuhusu UPANGA hivi kile kijiwe cha AHRLEM bado kipo pale au jamaa walikihamisha?

Hivi unahabari kama ARISTOTO naye yuko bongo na makid wake

Ebwana unakumbuka enzi za PUZA WA TAMBAZA?

what about mamabo ya DON BOSCO tournament?

how about mambo ya FOOD EVENING kule SHALIMAR town na watoto wa FORODHANI?

unamkumbuka SINGITIRA? ROZI MLEKWA je?

I wish QUICK MOVER ainie humu maana naye ni mmoja kati ya wachache wa JF ambao ni watoto wa DAR
 
Brazameni bwana kwa vituko, mbona wapo masela ambao pia ni ma-joni kisomo? wanajulikana kama "educated gangsters" ndio hao akina Y-thang na wengineo........ghorafa ya saba ilikuwa ni kijiwe poa, pia unakumbuka mambo ya pool side?

Ebwana kati ya vitu vilivyokuwa vikiniboa na POOLSIDE ni kile kiwinta cha saa tisa usiku ...kisha inabidi tukanyage miguu kwenda kule NDANI YA NYUMBA aka BILLS aka KWA CHALE MBOWE ambaye of course nadhani uanjua kama alimaliza almost shule nzima ya ZANAKI(lakini wale wazuri tuu) aka BILICANAS aka KWA KAKOBE


Nazungumzia hawa JF in house politicians wanna be ndio walikuwa Joni visomo na nahisi 99% yao walikwenda Jeshini kama si RUVU basi walikuwa MAKUTUPORA
 
Dela soul siku hizi anajulikana kama "Balozi," hao watu wa roots wapo wengi.....sister 'ake nigga one mara ya mwisho alikuwa DC.....je wewe ulikuwa mshabiki wa PAZI au VIJANA??

ebwana mimi nilikuwa VIJANA for simple reason, nilikuwa nanyemelea zile bank statement za marehemu MZEE MALAI ambaye nadhani unajua alikuwa hana hiyana kuzitoa na of course DULA alikuwa bwa mdogo wetu kwa hiyo ahhh we acha tuu...


halafu talk about haya mamabo ya bank statement umenikumbusha zile safari za SCOUT za pale ST ALBANS ...pale nilipata visa yangu ya kwanza kupitia lile kanisa kwenda states in 1995 ..kulikuwa na kijana mmoja pale alikuwa anaitwa ALLY MRISHO

watoto wa mjini mtamjua tuu huyu maana alikuwa pesa za watu vile vile
 
Namjua Ally Mrisho, yule mluguru mshenzi sana, yaani bado kidogo tu na mie angekula pesa yangu. Kwenye hiyo Trip ya '95 ulikuwa na kina Tiff nini? Watoto flani hivi wa Kinondoni walikuwa "mazungu wa mbwimbwi", jamaa wamelikita hapo NYC.
Ndio mzee Malai wa Pazi(RIP) alivuta na kile kisukari. Kwahiyo utakuwa unamjua Yassini Wassira, jamaa alikuwa ndio Bigman wa Pazi......nakumbuka sana mambo ya Indoor na kina Zonga!!!.
Bills pale mie nilikuwa nanunua bia nje kwenye vibanda vya 'chinga halafu naimbuka nazo ndani ili kusave kidogodogo............mzee umenikumbusha mbali sana, mambo ya St. Albans na safari za mtoni!!.

sAFARI YA 1995 haikuwa inajualikana sana kwani walitakiwa watu watatu tuu kwa sababu kulikuwa na makanisa yamechimwa moto na hao ma KKK kule SOUTH CAROLINA sasa mwaliko ukaja pale kwa yule pari ambaye of course akampa ally..ally naye akamua kutengeneza pesa mle...ebwana safari ilikuwa tamu kinoma ile maana ilikuwa haina ngongolo wala nini lakini maana kufika unyamwezini watu tukapokelewa na hao watu wa makanisa..ete

of course kama kawaida yetu wabongo pale tukatia HASARA kisawa sawa kwani watu wlikuwa wanapiga simu bongo DIRECT kisha of course watu wakaingia miktini

Mind you ile safari ilikuwa kipindi MV BUKOBA ilipotoa watu kafara na MKAPA ndio kachua nchi...nchi ilikuwa na UKAPA ile mbaya yaani hata kupata hizo passport ilikuwa mbinde ile kinoma maana ikienda pale immigration unakutana na akina SABU ambaye jana yke jioni mlikuwa pamoja mpirani kesha kupa mi ahadi kede kede mara ana kutupa kwa ABASI ambaye naye atakutupa kwa yule jamaa wa KIPEMBA ahhh na si kwamba huyo ALLY AMEIR watu walikuwa hawamjui ila ndio ya nini kuua mbu kwa gobole?

Hao watoto wa Ilala nawakumbuka ni wale wapemba na zile zilikuwa safari za 1996/7 za Holland halafu kipindi hicho CUF nao wakawafungulia milango wabongo kwenda kujilipua Holland yaani si mchezo ST ALBAN palikuwa bize ile kinoma

Ebwana ALLY MRISHO alimlia pesa mchizi wangu ndipo hapo tukaanza safari za kwenda kwao kule KIGAMBONI yaani noma tupu

maana nchi jua kali watoto wa kishua walikuwa wanzidi kuacha nchi na sie tuliobugi step kurudi tena bongo ilikuwa noma tupu maana si mshike mshike huop...lakini hicho ndicho kitu pekee cha kuwashukuru CUF maana bila zile kadi zao watu sijui wangeingiaje CANADA au huko MASKENDINAVIA au kwa BI MKUBWA

ebwan nilikuuliza maswali kwenye first page naona kimyaaa

najaribu kujiuliza hivi mwanaijiji na hawa vijana wengine humu ndali sijui walikuwa wapi enzi hizo
 
Wengi watakuwa Dar Exit tu au "friji open na geti kali", kwahiyo misukosuko ya mjini hawaijui.
Mie mwenyewe baadae nilikuwa nabamiza sana bank statement "kajanja" pale salamander, sticker za bima na fax kinyago baada ya bomu la Osama.....yote hayo nikiwa mwanafunzi chuo. Ile ya Osama nayo ilileta neema maana watu kibao waliondoka kwenda kwa UK kwa gia ya kuchukua Visa ya US.

mindhali umeleta habari za salamander basi poa

sasa unapajua NGAZI TANO? ni huu upande wa MKWEPU nyuma ya kwa Khery wa magazines ambaye naye pale si unajua tulikuwa tunajipatia ma RIGHT ON na WORD UP ( najuaOLE na wenzie watakuwa wanajiuliza sie tunazungumzia nini hapa( sasa pale NGAZI TANO kulikuwa na travel agency hiyo ukitaka VISA ya INDIA basi unaata na Ticket kwa hiyo watu wa midude wote walikuwa wanachukua ticket zao za kwenda shamba ...labda mpaka bombaya kisha machizi wanaingia zao PUK au wanajitwinga ndani ya PASHAWAR na kule si unajua kama unaroo ya paka basi unaweza kuingia na mzigo nyuma ya punda mpaka Iran ambako mzigo ulikuwa unanunulika kwa bei nzuri kinoma

Anywa back to salamander ebwana unamjua CARL LWEIS? nasikia naye yuko NY na MUSA yule mtoto wa Kipemba na wote wanakwenda kama FREAKY TAH maana si midreadlocks hiyo...

Hivi unamkumbuka LUGANO alikuwa nauza Juisi pale salamander? je unaikumbuka ile video library pale ilikuwa inatwa TAKE 5?

Lazima utakuwa na wewe ulishawahi kukutana na akina MWAKITWANGE, JESSE,SAIDI (nasikia yuko UJERUMANI alipatatoto la kijerumani) na bila kumsahau ndugu yetu bwana JOFREY na mwenzie DULA..japo dula aliamua kutukimbia na kwenda kijiwe cha WAUZA VIWANJA na MAGARI MNAZI MMOJA...kule nako noma ile mbaya maana kwanza hakuna kuitana kula wlala nini ...nazungumzia kijiwe cha Mnazi mmoja, pili kama una bahati basi umapate TALL ambaye mnapa cut yake ya laki moja na nyie mkipatalaki tatu poa, au ukiuza gari basi umpate NDAMA na enzi hizo mali asli walikuwa na yule JUMA NGIDA au juma NYAMIELA basi ahhh ndama alikuwa haaci kutupa shavu


ebwan uliwahi kuonana na MSOFE?
 
sasa unapajua NGAZI TANO? ni huu upande wa MKWEPU nyuma ya kwa Khery wa magazines ambaye naye pale si unajua tulikuwa tunajipatia ma RIGHT ON na WORD UP

..eeh bwana bro kheri siku hizi biashara inadorora kidogo,haonekani sana pale,jamaa zake ndo wamejaa!
 
Halafu unakumbuka miaka ile IDDI JANGUA alivyokuwa akitesa kule coco beach full CHICAGO BULLS kuanzia CAP mpaka soksi na raba?

Nakumbuka sana hiyo, hayo yalianza tokea baada ya safari yake mamtoni.
Lakini pia kuna wakati ulitokea ugonvi mkubwa baina ya kundi la kina Idd na Adili (RIP), ugonvi huo ulianzia huko Coco beach na kuwa bonge la beef btn IST na vijana kadhaa toka Shaban Roberts waliokuwa upande wa Idd...


Umezungumzia kuhusu UPANGA
Kuhusu Upanga miye namkumbuka jamaa mmoja alikuwa anajiita Cool, alikuwa mitaa ya katikati hivi nadhani walikuwa na garage ya magari, jamaa alikuwa anapenda Ragga music...


Ebwana unakumbuka enzi za PUZA WA TAMBAZA?
Enzi za kina Puza (RIP) nakumbuka, akina Manyau na akina Tyson... kijiwe chao kilianzia pale kwenye fence ya Tambaza na magorofa ya upande wa Muhimbili, kijiwe kilianza kimchezo mchezo tu katika harakati za kuwa onea Azania baadae likawa soo kubwa dhidi ya walimu pale pale Tambaza...

I wish QUICK MOVER ainie humu maana naye ni mmoja kati ya wachache wa JF ambao ni watoto wa DAR
brazameni, wengi tu hapa wanafahamiana, na wengi tu ni watoto wa DAR, ila kama jinsi tulivyo binadamu, wengine wakimya wengine waongeaji sana... hivyo kuna wengine wanayajua haya yote unayo ongelea humu na wanafahamiana na wale unaowataja, ila ndiyo hivyo tena, hayo ni yao na ndugu, jamaa au rafiki zao... siyo ya ku share na kila mmoja hapa ukumbini!

Baadae,

SteveD.
 
Ebwana kati ya vitu vilivyokuwa vikiniboa na POOLSIDE ni kile kiwinta cha saa tisa usiku ...kisha inabidi tukanyage miguu kwenda kule NDANI YA NYUMBA aka BILLS aka KWA CHALE MBOWE ambaye of course nadhani uanjua kama alimaliza almost shule nzima ya ZANAKI(lakini wale wazuri tuu) aka BILICANAS aka KWA KAKOBE
Kabla ya Poolside, clouds disco lili hamia kwanza pahala fulani hivi opposite na Empire... kisha disco likawa lina hama hama na kati ya hapo na Twiga hotel (wakati huo), kabla hawajajigawa na kuanza kupiga Mayenu Tazara club...

Nazungumzia hawa JF in house politicians wanna be ndio walikuwa Joni visomo na nahisi 99% yao walikwenda Jeshini kama si RUVU basi walikuwa MAKUTUPORA

he he he, umeniacha naumwa mbavu hapa brazameni... duuuh, eti jeshini Ruvu au Makutupora... miye nilikimbia hilo..niliepuka!!

SteveD.
 
najaribu kujiuliza hivi mwanaijiji na hawa vijana wengine humu ndali sijui walikuwa wapi enzi hizo

Again, watu wasikuzuge kuongelea siasa hapa ukawaona siyo watu wa mjini.... ni progression tu watu wanafanya katika maisha yao, hivyo unaweza kukuta Mkjj ni mtoto wa mjini kupita... wewe mchokoze akutolee data zako.... he he.

SteveD.
 
Heri wa Magazeti alikuwa mshkaji sana, pale kulikuwa na mafundi baiskeli na wachonga mihuli mbele ya duka la miwani....duh longtime yaani. Kwenye ngazi za kupanda Dar Chamber of Commerce, kulikuwa na fundi viatu mmoja mchaga.... namjua, naye kuna kipindi flani alikuwa anaingiza wakuja town kwa mzushi sana, kwani ile ilikuwa bosheni!!. Sisi tulikuwa na ofisi ya kizushi kule uwani ya mambo ya clearing and fowarding. Heri nasikia hayupo tena pale na salamander haipo tena!!!. Msofe(mpare)bank statement feki....alikuwa na ofisi yake kwenye basement jengo la opposite ya salamander kwa mtaa ule nadhani ni mansfield. Musa"fidodido" yupo NYC kesha kuwa gwiji, nilimwona mara ya mwisho Harlem mwaka '99. Hivi ulisha wahi kula ile mama ntilie pale palipokuwa magoti?? kwikwikwi, mlango gunia, lazima upige chabo (shoto,kulia)ili watu wasikuone ukiingia kula ugali wa kukata!!!. Unamjua Peter(PITAKULE), mchizi flani alikuwa ana-hang sana mitaa ile akitafuta safari............Ally Mrisho nasikia mwishowe alidhulumu watu, wakaamua kumtembezea "pira", lakini mwanga kichizi....yaani kesi zinakufa bila yeye kuchukuliwa hatua yeyote, jamaa walikuwa na plan ya kumfanyizia, lakini hata sijui iliishia wapi.

ahhh kama unazungumzia Chamber of commerce kulikuwa na jamaa mmoja mzungu alikuwa na mkewe black american na irasta hivi wanashuka sana pale kwa hery kuchukua magazines yule mama alikuwa ni ESSENCE halafu lile zungu lilikuwa jitu la NEWSWEEK

kana kama hiyo haitoshi kama unasema ni kule nyuma ya Chamber of commerce ndio kulikuwa na mdosi ana ofis ya uwongo na kweli na vile vile kulikuwa na mzee mmoja alikuwa nafanya kazi posta na simu kaaanzisha kampuni yake ya kufunga mitambo ya simu ya PABX na fundi wake kubwa alikuwa anaitwa RAMA ambaye alikuwa anakaa morocco ...of course rama boy baadae akaanzisha kampuni yake baada ya kupata tenda mbili tatu hivi

na khery mwenyewe huyu hapa: biashara lianza kuwa mbaya baada ya ALLIANCE kufa na matokeo yake akina FILEMONI CHACHA na DEO nao ikabidi waangalie ustaarabu mwingine. last time nilikutana na FILEMONI pale chooni au jina lingine CLUB AFRIQUE, canningtown na yuko hapo morogoro ya UK (reading) nakumbuka ilikuwa kama miaka 4 hivi iliyopita
Picha kwa niaba ya MJENGWA BLOG

heri0111.JPG


MUSSA FIDO DIDO ndiye alikyekuwa mjajanja wake CARL LEWIS alipokwenda NY, sasa enzi zile Mussa kaanza na
Zaidi ya yote hayo, ebwana basi nyie mtakuwa mlikuwa na pesa maana sie kama si pale fery ya hapa karibu na maboti ya zenji basi ilikuwa KWA MAMA PAUL kule karibu na ovean road hospital au tueme INTERNETAIONAL HOUSE jirani na holiday inn

sasa kama hiyo haitoshi kulikuwa na wale mabinti wanatembea jioni wakiuza ndizi kwenye sini wale walikuwa washikaji ile kinoma ..story ndefu kidogo maana walikuwa wanasoma kwa masawe sasa nadhani unanielewa hapo kuhusu age range zao..inshort walikuwa ni watoto wa USWAZI sasa kwenda kwa mama apul ilibidi mnanunua ndizi zenu kabisa kabla ya kwenda kule

siku mamabo yakijipa basi saa kumi nayie mnaenda kujipatia chai pale mtaa wa CHAGGA opposite na CHEFS PRIDE na JK enzi hizo bado yuko forein hivyo wapambe wake walikuwa akina Maharagwe na kanali Ibrahim

na of course mambo yakiwa mazuri zaidi basi mnaingia zenu CHIEFS PRIDE ijumaa after noon pale mnaagiza wale kuku wa kuzunguka


mambo yakiwa medium basi hamna noma mnaingia pale BUTIHAMA RESTAURANT magomeni mnaagiza plau nyama au NYEUPE MOJA na kisha unajichagulia samaki waliokaangwa pale kwenye sinia...na unaagiza na mindi huku ushajichukulia ndizi zako toka kwa yule bibi pale nje

ukishashiba huyooo unaenda kwa bitebo kukata nyewe pale oppposite na Lango la jiji huku mnacheki premier league kama ni jumamosi na ukitaka kupiga simu za ulaya na USA basi unaenda hapo kwa BABU MTAMA MCHUNGU na kama babu hapati line basi tunaenda zetu MUHIMBILI kule karubu na wamisela tunaitia hasara serikali kisawa sawa kwa misimu ya uchee ya America

Habo sijakupa ratiba ya Usiku jumamosi
 
Kuna mshkaji mmoja nilikutana nae pale, alikuwa jamaa wa wale wachonga mihuri......jamaa alikufa mwaka jana. Yeye na mdogo wake walikufa maji Houston,TX......sijui kama unamjua?!!!.

ebwana naikumbuka hiyo ya jama kufa maji TX noma tupu unaambiwa mwenyewe nimechinga sana mihuri kwa wale vijana wa kichaga pale mbele

duh noma


ebwansi unajua opposite pale akina IPPY MALECELA,KINJE, NA ALBERT MARWA (nasikia kasilimu) walikuwa na ofisi opposite na kile kiji saluni alichoanzia maisha RITA MLAKI na enzi hizo yule binti yake NAMBUA likuwa bomba ile kinoma sema si unajua keshachoka na kuzeeka? yaani market ya watoto wazuri imekuwa saturated ile kinoma unambiwa
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom