Kama mfumo wa kupata watakaochaguliwa kuwa wabunge wa viti maalum utakuwa ni ule uliotangazwa na Kitila Kitumbo basi CHADEMA itakuwa imekosea sana.
Kwa maoni yangu viti maalum visitumike kama asante kwa watu bali kama ni mkakati wa kukiongezea chama mawanda yake na kukijengea umaarufu zaidi kwa jamii.
Kwa mfano kuna haja gani kwa mkoa wenye wabunge wengi wa CHADEMA kupewa tena wabunge wa vii maalum. Na kwenye tayari mbunge wa kuchaguliwa jee kuna haja ya kuteua tena mbunge wa kiti maalum ili afanye nini?
Ingekuwa bora kama CHADEMA ingechagua wabunge wa viti maalum (wanaofaa lakini) kutoka kwenye ile mikoa na majimbo ambayo hayana wabunge wa kuchaguliwa. lengo ni kutumia wabunge hao wa kuteuliwa kama changamoto kwa wabunge wa kuchaguliwa wa CCM (WATCH DOG).
Kilimanjaro ina haja gani tena ya kuwa na mbunge wa viti maalum kuliko Mtwara, au Mbeya mjini kuliko jimbo la Rungwe?
Mi nafikiri la muhimu kwanza ni kumpata mwenye moyo wa kukijenga chama kutegemea na uwezo wake wa kujenga hoja na kutoa muda wake kukisaidia chama. Huu ni wakati wa mapambano. Hata Jeshini huwezi kumweka kamanda legelege kwa sababu ati anatoka mkoa fulani. Ujasiri, umakini, na moyo wa kukitumikia chama wakati wa shida na wakkati wa raha ni muhimu zaidi.
Kama wapo wanaotoka mikoa ambayo haikupata wabunge ambao ni majasiri na wanajua kujenga hoja ni vizuri zaidi wakachukuliwa hao. Kama hawapo si vizuri ukamuokota mtu ukamwambia nenda bungeni wakati haoni kuna tatizo.