Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,350
- 11,222
Ikiwa miezi mitatau imetimia tangu vita vianze kati ya Israel na Palestina na bila mshindi kupatikana, wafuatiliaji wa vita hivyo wana nafasi ya kuchagua wa kupewa nishani baada ya kumalizika kwa vita vyenyewe.
Kwa mtazamo wangu nishani ya mwanzo itawaendea Hamas kwa kuchukua maamuzi magumu na ya kimkakati kupambana na jeshi kubwa na linalotumia silaha za kisasa zaidi duniani, jeshi la IDF.
Nishani ya pili itawaendea kitua cha televisheni cha Aljazeera kwa kuviripoti vita hivi kwa karibu zaidi na kwa gharama kubwa. Pongezi halisi zitaelekezwa kwenye maamuzi yao ya kuonesha matukio uwazi mkubwa kiasi kwamba kama kungekuwa na watu waliobakiwa na ubinadamu basi matukio ya kuuliwa watu namna hii kusingeachwa kukaendelea tangu siku za mwanzo za vita.
Kwenye kituo hicho ingependekezwa itolewe nishani maalumu kwa mwandishi wao anayeitwa Wael Dahdouh, ambaye alikuwa ni msimamizi mkuu wa matangazo ya kituo hicho kwa Gaza.
Mwandishi huyo aliitikia wito wa kuhamisha watu kutoka kaskazini ya Gaza kuwapeleka maeneo mengine yaliyotajwa yangekuwa salama. Siku chache familia yake yote ilipigwa kombora na kufariki hapo hapo,kuanzia mke na watoto wote.
Wael alipopata taarifa hiyo alishtuka kidogo lakini baada ya hapo akaenda kushuhudia maiti za watu wake na kwa ushujaa mkubwa yeye mwenyewe akaongoza sala ya jeneza ya mke na watoto wake huku akiwa amevaa jaketi la uandishi wa habari.
Cha kushangaza baada ya mazishi hayo ya mke na watoto wake,Wael akarudi kuripoti matukio mengine ya vita ya kuuliwa na kubomolewa majumba maeneo mengine.
Maamuzi ya kituo cha Aljazeera kumpumzisha kidogo ndio yalimuondoa Wael hewani kabla ya kurudia tena kazi yake.
Nishani ya tatu itawaendea wapiganji wa Hizbullah na Houth kwa pamoja kwa kuwaunga mkono Hamas mpaka mwisho bila kuogopa wala kurudi nyuma.
Idadi ya nishani hizo na watu zinazowaendea inaendelea mpaka 10 lakini mimi naishia hapo kwa sasa.