Hawa jamaa ni kina nani haswa?

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,563
2,037
Habarini za mchana wakuu,

Naomba kuleta mada hii ambayo nimeipitia ila sijapata nondo za kutosha maana bado nimepata mkanganyiko kidogo. Twende pamoja.

Inasemekana kuwa kuna hawa beings wanayo tabia ya kuja dunia kufanya vitu mbalimbali mfano: kuleta ujuzi wa kisayansi pamoja na ustaarabu baina ya jamii mbalimbali.

Kilichonifanya nikaleta uzi huu hapa ni mahusiano ya visa hivi ambavyo kama hapa nitaviita "myth" ili kutoleta mkanganyiko zaidi.

1. Huko Amerika Kusini kwa jamii ya Inca inaaminika kuwa kuwa beings ambao ni supernatural wanatokea mawinguni na wana rangi nyeupe mfano wa chaki. Kwa jamii hii ya Inca wamewapa jina la "Viracochas". Viumbe hawa wanaaminika kuwa waliwapatia elimu na ujuzi wa kujenga majengo makubwa kama vile Pyramids pamoja na ujuzi katika masuala ya utabiri.

2. Lakini tukienda Mesopotamia ambapo kwa sasa ni kama eneo La Iraq, kusini mwa Uturuki pamoja na sehemu chache za nchi ya Syria, kuna jamii zina imani ya hawa viumbe waliowapa majina ya "Ahura Mazda" wakiwa wana maana ya kwamba "roho zenye ujuzi wa mambo". Pia, wanaamini kuwa walikuwa wakisafiri kwa kutumia chombo kilichokaa mfano wa kisosi kinachotoa mwanga mkali sana.

3. Amerika ya kaskazini nayo ambapo hapa tunaangalia jamii ya Wahindi Wekundu ama Red Indians waliojulikana kama kabila la "Hopi", ambao nao wana imani ya kukutana na hawa beings na kuwapatia jina la "Bahana" wakiwa na maana ya "ndugu weupe" kutoka mawinguni. Hawa beings waliwapatia wanajamii hawa uwezo wa aina mbalimbali kama vile ujuzi wa kuwinda pamoja na ujuzi wa mambo ya kidunia.

4. Lakini pia India pia kuna jamii zinazoamini kuu ya hawa jamaa, ambapo wanawaita "Asura" kumaanisha miungu weupe wa upepo. Jamii mbalimbali ziliweza kupata ujuzi kutoka kwa hawa jamaa, lakini pia jamii ziliamini kuwa hawa jamaa wanaishi dunia yao ambayo imejaa na teknolojia ya kiwango cha juu sana kwa kuna ndege mfano wa visosi pia maisha yao yalikuwa ni mazuri sana kupita ya dunia ya kwako kipindi kile.

5. Mwisho, mnamo mwaka wa 1954, Rais wa 34 wa Marekani Bwana Dwight Eisenhower inadaiwa kuwa alikutana na hawa jamaa kwenye military base moja Marekani katika kikao cha siri. Taarifa hii ilivuja kutoka kwa Bwana Captain Major Robert O. Dean ambaye alikuwa ni mmoja katika ya viongozi wa juu wa jeshi kipindi hicho. Kwa maelezo yake anadai kuwa "viumbe wale walikuwa wakiongea kwa mtindo wa mentality zaidi kwani walikuwa hawafungui kinywa kabisa na kuwa walikuwa ni warefu mpaka kufika futi 9 na nusu.

Mimi nimejaribu kuchakata ubongo kwenye kuunganisha dots, nimeshindwa. Naombeni wajuvi kidogo mnipe nondo zaidi.
Mshanajr Malcom Lumumba na wengine Please nisaidie kwa hili.

Nitashukuru sana kwa hilo.
Ninawasilisha uzi.

Sent using Infinix hot 4
 
Hapa nimefanya kusummarize ila vyanzo vya habari vipo vingi sana

Sent using Infinix hot 4
 
Back
Top Bottom