Have I ever posted here? Here I come... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Have I ever posted here? Here I come...

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Mphamvu, May 5, 2012.

 1. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Sina hakika na nilichokiandika au la, kwa kuwa mambo yamekuwa mengi.
  Haya, ngoja niweke post yangu.
  Karibuni nyumbani kwetu wali umekuwa adimu, kisa bei. Sasa na Ugali nao unaelekea kubaya, kilo ya unga buku' sh. mbili, namaanisha 1200/=... Bahati mbaya ugali hauna malighafi mbadala, lazima unga uhusike.
  Jumamosi njema!
  [​IMG]
   
 2. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  We msukuma?
  Asante...lete mboga tuushambulie
   
 3. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Ni namna gani unajionesha jinsi ulivyokua mchoyo! Unapotukaribisha hom ugali mtupu! hauna mboga/kitoweo! Tuleje ?
  Au wageni ndo tuje na mboga zetu?
  We huna dhati ya kutukaribisha , mi siji !
  Basi hata kachumbari ?
   
 4. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  mboga kisoda ugali mlima ndivyo mitz tulivyozoea..
   
 5. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Afadhali hapo kwangu kwetu unga 1500KGMchele 2500KG Sukari 2500 kgImebidi tubadilishe bajetiChai tunakunywa saa sita na ..chakula cha mchana saa 11 jioni hiyo ndo mpaka kesho..Wali tunakula kwa week mala moja jpili..
   
 6. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Pole dada.
  Hiyo huku uswahilini tunaita pasi ndefu, wakati wewe unafikiria kuanza huo utaratibu, wenzako tulishauanza muda mrefu sana, na tulishajizoelea.
   
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  May 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Sio kaka, mimi ni suriama.
  Kuhusu mboga mpango mzima kujitegemea, hauna hata kipande cha papa au nguru hapo?
   
 8. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #8
  May 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160

  FirstLady1 kuna dalili zote za masikini kuendelea kuwa masikini hata zaidi.
  Pole kwa ugumu wa maisha,mtanzania wa kawaida amepoteza matumaini.Ukiona kwako kuna joto basi kuna kwingine panaungua kabisa.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #9
  May 5, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Ukiwa na njaa kutoka moyoni wala huhitaji kubembelezwa na mboga, unashuka tu wenyewe.
  Umenifurahisha mkuu, ugali mkubwa ndio ubora wa chakula huku kwetu.
   
 10. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #10
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280

  Jamani bado nawaza hili baraza Jipya la mawaziri
  Njaa inaniuma mie .
  Hii hali inakuwa ngumu kwangu kuizoea .
  watoto wanauliza mama mbona siku hizi wali tunakula mala moja moja na hatushibi mama
  Roho inauma jamani
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ambitious
  Mie sasa nawaza kuwekeza kwenye kilimo
  Maisha yanazidi kuwa magumu kila siku.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #12
  May 5, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  FL , hii mitoto yetu sie wazazi ndiyo tunailea vibaya! Utaniuliza whaay? Siku mambo yamekaa vibaya pakipikwa ugali usiku mitoto inazira !
  mitoto imenuna! Kosa tunaanza kuwabembeleza!
  "ni leo tu wanangu kuleni , haturudii tena kupika ugali usiku".
  Unategemea nini hapo FirstLady ?
  Miaka ya utoto wetu ilikua hom gaga likipikwa usiku No objection zaidi ya kula, wala hatukuuona ugali wa usiku ni kituko! Kuna siku nimewakuta wanangu wanamcheka mama yao, nilipowauliza kiwachekeshacho wakanijibu,
  "eti mama anapika ugali usiku! "
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. Ambitious

  Ambitious JF-Expert Member

  #13
  May 5, 2012
  Joined: Dec 26, 2011
  Messages: 2,125
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160

  FirstLady1,Hilo wazo zuri tu haya mambo ya kuzunguka kutwa maghorofani huku bati la nyumba yako lavuja ni utumwa.
  Ukiweka mikakati mizuri kilimo kinalipa kinachotakiwa ni kujitoa kikweli na uvumilivu.
  Usione watanzania tu wagumu kushaurika huu si wakati wa kutafuta kazi za mjini na kuishia kununua Blackberry na LCD TV na mtu akaona maisha ameyaweza.
  We dont need to think outside the box anymore.We have to tear it into tiny little pieces.Today not tomorrow.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #14
  May 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  dah, huo ugali mgumu wa kisukuma unatia hamasa kula kwa maziwa ya mgando.
  Afu unapigwa la manyani sio kila mtu kwenye sahani yake.
  Na mboga iwe mashishanga au chubu au mkarango lol
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  May 5, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,230
  Trophy Points: 280
  ama kweli mwili haujengwi kwa matofali......
   
 16. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #16
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Judgement naona hii mambo ya watoto iko pote ..Sasa leo umpe mtoto mchana ugali ,usiku ugali atakuelewa huyo?
   
 17. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #17
  May 5, 2012
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,582
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  Ambitious
  Inabidi sasa tupange mipango inayopangika na kufanyika ..la sivyo tunakoelekea siko
  Mie nilidhani nitapangwa kwenye baraza la mawaziri angalau nikajenge kijiji changu ..mheshimiwa hakuniona
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #18
  May 5, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Teh mi nakuja na mlenda wa dodoma
   
 19. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #19
  May 5, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 160
  heri wa hapa kwangu wanakula ugali bila kunung'unika, iwe mchana au usiku.

  Sasa kibinti kimevaa pedo na dred kichwani kitakula ugali?
  Mtoto wa kiume ana kiduku au afro kichwani ugali upite wapi?
   
 20. simplemind

  simplemind JF-Expert Member

  #20
  May 5, 2012
  Joined: Apr 10, 2009
  Messages: 11,813
  Likes Received: 2,586
  Trophy Points: 280
  Msukuma kwa Ugali sijaona, nimeshuhudia ugali unasongwa alfajiri for breakfast pale shy mjini.
   
Loading...