Hatuwezi kutatua tatizo la sukari bila kusahihisha makosa ya Hayati Magufuli kwenye sekta hii mwaka 2016

Waziri anasema wakulima wa miwa wa Kilombero na Mtibwa wanatupa wastani wa Tani 200 za miwa ambazo viwanda vinashindwa kununua. Hapa unaelewaje?

..naelewa kwamba viwanda vinatakiwa viongeze capacity.
 
mkuu naamini kuna mhuni mmoja ameshaanza kampeni za 2025, na anawavuruga ccm , anawafarakanisha wao kwa wao

ukweli ni kuwa huwezi kumtukana hayati magufuli bila kuwa umeitukana na ccm yenyewe kwa sababu yeye ndiye alikuwa mwenyekiti

sasa hawa wanaoleta mada kama hizi naamini wanajua wanachokifanya kabisa , mwisho wa siku hapo 2025 watakuwa wamemchafua sio JPM tu bali hata na chama kizima cha mapinduzi hivyo kujifagilia njia kwenye kampeni
 
Hicho kisamvu kwenye amani kinaliwa na BABA YAKO GAIDI huko SEGEREA! Yupo saaafi na amani ya MOYO! na Wafuasi wa gaidi wana amani ya moyo tozo haziwahusu! WAMELALA ndani na joto safi kabisa na MAJI YANAMWAGIKA! Shubaaaamit
Lakini tuna uhakika na kuwa kesho tutaamka!!hakuna kundi la interahamwe tena!!mmoja ndio huyo ameshachezea miaka 30, na mwingine ndio kwanza ana setiwa ajae kwenye rada!!MUNGU FUNDI
 
Kabisa mkuu.
 
MBona nyie watu wagumu kuelewa Waziri hazuii watu kuagiza sukari Bali anasimamia sheria iliyopo kwamba sukari anayetakiwa kuagiza in mzalishaji.
 
Wakati wa Kikwete kulikuwa na shida ya sukari acha uongo hadi mitaani ilijaa sukari nyeupe ya viwandani
Huyo mburula anaandika mambo ya kitoto nadhani kwa ajili ya wale wasiojua mambo ya nchi hii.

Japo niligundua anapoelekea ni kwa JPM ndipo nilipomdhalau, issue ya sukari haijawahi kupita salama au watz kuinjoi bei nzuri toka Mwl JKN aondoke.
 
Kama kufeli tunafeli na tunaendelea kufeli chini ya hawa ndugu zangu CCM
 
weka kumbukumbu zako sahihi, sukari 2011 ilifikia mpaka 8000 kwa kg!!, ukisema hatujawahi kuwa ana uhaba au mfumuko wa bei toka miaka ya 90 ntakushangaa!
Huu ni uwongo. Unless unaongelea Zimbabwe ila Tanzania, HAPANA.
 
MBona nyie watu wagumu kuelewa Waziri hazuii watu kuagiza sukari Bali anasimamia sheria iliyopo kwamba sukari anayetakiwa kuagiza in mzalishaji.
Ni sheria ya HOVYO mtu ambaye amepewa leseni ya kuzalisha sukari bado unamuongezea kuagiza sukari ikipungua. Mzalishaji anapata uvivu wa kuzalisha kwa kuwa kuagiza ni rahisi. Mwisho wa siku miwa Tani 100 inabakia haijanunuliwa kutoka kwa wakulima wa Kilombero
 

..kuna maelezo ya waziri amedai matarajio ya serikali ni deficit ya sukari kuisha mwaka huu.

..na kwa mwaka ujao kama bado deficit itakuwepo bodi ya sukari ndio watakaoagiza sukari.

..ngoja nitafute hiyo video clip nitaiweka hapa.
 
Umetoa maelezo mengi umeshindwa kutoa mstari mmoja tu wa suggestion ya tufanye nini?
 
Leo nimefurahi sana. Mtu kaleta ukweli wote

Jamaa alikuwa mbaya sana. Tushukuru mungu katuondolea. Imagine miaka mitano kaharibu nchi kwa kiasi hiki. Je isingekuwa covid kufika Leo tungekuwa hovyo sana
Kwa hiyo unataka kutuambia covid ndio nyota wa mchezo na mkombozi wetu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…