Funguka basi ndugu yetu, unataka elimu ya bure ya nani?
Kwanza acha kudanganywa na ghiliba za wanasiasa, hakuna elimu ya bure labda waitwe Wakongo au Wanigeria waje hapa ndio watakuwa wanasomeshwa bure. Mtanzania elewa kuwa hakuna elimu ya bure kama ni lazima wananchi walipe kodi ndipo elimu itolewe - hiyo wanayodai itakuwa ya bure.
Ijulikane kuwa ni wajibu wa serikali kukusanya kodi na hiyo kodi iwarudie wananchi kwa namna ya kupewa elimu, afya, miundo mbinu, maji n.k. Haijalishi tunalipa kodi kiasi gani lakini tunahitaji serikali itakayo kusanya kodi na tukaona manufaa ya kulipa kodi, wenzetu kama Sweden naambiwa wanlipa kodi asilimia sitin na tano ya mapato yao lakini hawalalamiki na wanfurahi kulipa kodi kwa sababu inawarudia na huduma wanazopata kutoka kwa serkali yao ni bora kabisa.
Lazima tubadilike na kuwaelewa wanasiasa wetu ati utasikia CCM au CHADEMA watatoa elimu bure, na tulivyo malofa tunapiga vigelegele. Ni lazima wananchi tufike mahali tuidai serikali huduma hizi kwa sababu tunalipa kodi. Na kodi tunayoiongelea hapa sio PAYE tu, mwananchi aelewe kuwa kila unaponunua dukani au sokoni na unapolipia huduma kama umeme, maji, matibabu kwenye hospitali za binafsi kuna kodi humo ikiwemo asilimia kumi na nane ya VAT - Zinduka mtanzania unaghilibiwa eti utapewa elimu ya bure, ni haki ya watoto wetu kupewa elimu na serikali kwani inakusanya kodi.
Wakati huu ni wa kuchagua serikali itakayotumia kodi zetu vizuri ili itoe huduma za jamii zilizo bora na pasipo kututaka eti tuchangie kwa kupangiwa kiwango. Hatukatai kuwa tunaweza kuchangia lakini si kwa kulazimishwa, tutachangia kwa hairi na baada ya kuona kweli serikali yetu imezidiwa na ni lazima tuone kweli imejitahidi nasi tutachangia - iwe ni nguvu zetu na si tulazimishwe kuwa michango ya pesa tu.
Naomba kuwasilisha kwa kuyanyumbulisha haya kwa upendo.