Hatupendi ila tutafanyaje

Hatupendi ila tutafanyaje

Sio kama tunapenda kuwavizia usiku ili tuwakabe kwa nia ya kuwaibia.....HATUPENDI ILA TUTAFANYAJE

Sio kama tunapenda kushinda kutwa nzima kwenye betting station tukihesabu odds.... HATUPENDI ILA TUTAFANYAJE

Sio kama dada zetu wanapenda kuuza miili yao kwa kufanya sehemu zao za Siri kama chanzo Cha mtaji....HAWAPENDI ILA WATAFANYAJE

Sio kama tunafurahia kuitwa majobless,kula kunya nyumbani kwa wazazi,shemeji au shangazi.... HATUPENDI ILA TUTAFANYAJE

Sio kama tunapenda kufanya kazi za viwandani kwa siku nzima unatoka na buku 4,kubeba zege kuokota makopo,kupiga debe.... HATUPENDI ILA TUTAFANYAJE

Na sio kama tunapenda kuuza bangi mtaani au kusafirisha madawa ya kulevya ilhali najua kuwa Kuna kukamatwa na kupewa adhabu Kali.... HATUPENDI ILA TUTAFANYAJE

Najua unaweza sema nirudi shambani ,vipi naweza kupata Mali ya shambani bila mtaji???unadhani nakataa kwnda VETA ,nikimaliza nitautumiaje huo ujuzi bila mtaji...au unataka niwe nyoka wa kijiwe wakati umri ushaenda?????

Tunaishi inavyobidi tuishi
Hatupendi uandike haya yote ila tunafanyaje
 
Maumivu ya ukosefu wa ajira ni makali sana, nimetumia takribani miaka sita kupambana mimi mwenyewe binafsi mpaka kufikia leo hii angalao naanza kuona mwanga, kwaiyo ni hali ambayo naijua vizuri. Again, maumivu ni makali sana, especialy ukiwa mwanaume.

TUnafahamu kabisa wanasiasa hawana maarifa ya kukabiliana na ili tatizo kwaiyo ni vyema watumie busara kukaa kimya tu kuliko kuchokonoa nyongo za vijana
🗣️Umeongea point mkuu 😔😔
 
Back
Top Bottom