Mwl Mwakujonga
JF-Expert Member
- Jun 29, 2023
- 362
- 714
Ajira hakuna ila kazi zipo tele.
Je unacheti, au ujuzi au una afya njema au una ulemavu wowote?
Chochote ulichonacho ni fursa
Leo naongea na wewe ambae huko tu nyumbani au mtaani haujui uanzie wapi katika maisha aya.
Kuna habari niliiona katika mitandao ya kijamii, habari ya kina mama wa nyumbani ambao waliiona fursa wakati wengine wanaona ni changamoto wao waliona fursa
Wamama hao waliona vijana wengi ambao wanawatoto wadogo na kupatwa na changamoto za wadada wa kazi wanashindwa kutekeleza majukumu yao vizuri kutokana na kukosa watu wa kuwasaidia kulea watoto wao.
Wamama hao waliona hiyo ni fursa wakaanzisha biashara unaleta mtoto na wako unamwacha hadi jioni unawapa elfu mbili kwa siku watampa chakula watamtunza hadi utakaporudi kutoka kazini.
Wanandoa waliona changamoto ya wadada wakina mama waliona fursa ya kuanzisha daycare
Hata wewe hiko fursa bado tu ujapata kuitazama.
Umemalisha shule au ukusoma au kwa namna yoyote ile hauna shughuli ya kufanya ni kwamba haujaamua kumpa Mungu nafasi akuonyeshe fursa zinazokuzunguka
Kuna shuhuda nyingi ambazo nimeziona kwa macho yangu watu ambao walikuwa hawana chochote leo hii wanamaisha
Mfano kuns kaka ambaye anafanya biashara ya kuuza magari yeye mwenyewe anasema alikuwa mpiga picha tu lakini leo ni mfanyabiashara mkubwa tu wa magari
Kinachoniumiza ni kwmaba tuna vijana wengi lakini hawafanyi kazi, wako vijiweni au namakundi ambayo sio mazuri
Ni kweli ajira hakuna, kazi je ? Ajira zinaweza kukosekana lakini kazi ziko.
Hakuna mtu mkubwa ambaye alianzia juu, kila aliye na mafanikioa anahistoria yake
Changamoto tulizonazo tunatamani kuanzia juu, sio wote tutaweza kuanzi juu, wengine tutaanzia chini.
Leo hii unakutana na kijana anakuomba pesa ya kula na ni mzima tu hana shida yoyote ni aibu sana
Kuna wakina mama wanatunza familia kwa kazi ya kumwaga zege kwenye site za watu.
Unaweza kusema haha kaka mimi nimesoma chuo kikuu nikamwage zege?.
Sawa ni kweli umesoma sasa kama umesoma unashindwaje kutumia cheti chako kupata kipato
Wako vijana ambao hawakukaa kulalamika juu ya ajira kwa sababu hata ulilalamika hakuna ajira utafanyaje sasa kupa ajira? Wako vijana ambao hawakulalamika waliongia kazini mtaani leo hii sio kama walivyo jana
Nakumbuka miaka kadhaa kuna kaka mmoja alikuwa anafundisha tuition mitaa ya kwetu na kipindi hicho hakukuwa na shule nyingi za private miaka ikapita akafanikiwa kuansisha shule yake na shule yake ni miongoni mwashule bora mtaani kwetu kwa hiyo inawezekana
Mifano ni mingi shushuda ni nyingi, tunaweza kuandika shuhuda na shuhuda lakini kama hauataamua kuchukua atua na kupambana juu ya atima ya kesho yako utabakia hivyo hivyo.
Unakuta kijana anasimu ya bei kali lakini hana kazi ? Sasa hiyo simu yako inakusaidia nini?
Utaskia haha naafatilia michongo kwa wana sasa hiyo michongo mbona haijawai kufanikiwa ?
Waswahili wanausemi gari inayotembea ndiyo inashika mwendo, mafanikio ni atua.
Kuna watu wametumia simu zao vizuri unakutana na kijana kazi yake ni kupiga picha vitu madukani na kutafuta wataje, nawengine wanashuhudia kabla ya kumiliki maduka yao walikuwa wanapiga picha ya bidhaa za watu na kupost kwenye mitandao na leo hii wanamiliki ofisi zao.
Kuna kijana mmoja hata simjua hana kaa wapi nachojua nikiitaji kitu kutoka jijini najua nitamtumia fedha atakwenda dukani ataninunulia mzigo atanitimia nampa ya usumbufu maisha yanakwenda pia namuunganisha na watu wengine
Usitafute kisiingizio mara hoo mimi sikusoma wala wazazi wangu hawako, kama kweli waliosoma ndio wangefanikiwa basi tusingekuwa na matajiri ambao hawakwenda shule, lakini leo tuna matajiri wengi hawakwenda shule kabsa na wengine wameishia darasa la saba
Hacha kutafuta sababu za kutoakuanza hanza na ulichonacho, uwe umesoma au haujasoma we pambana na Mungu atakusaidia
Kuna mwingine anasema yeye ni yatima, utajiri au umaskini autegemeia unawazazi au hauna ila bidii na jitiada binafsi ndizo nguzo za mafanikio yako, simama na Mungu akusaidie.