Hatujui kesho yetu

Haipaswi kumdharau Binadamu yeyote, awe fukara, mlemavu, Tajiri n.k

Tuheshimiane tu.
 
Kabisa mkuu.
Me mwez wa 7 nilipanga nitoke home nikapange ilikuwa Arusha imefika mwez wa 7 nimeanza kukaa geto Tabora☺️
 
Lengo lake zuri sana nimelielewa la kutumotivate lakini mfano wake wa mchongo.....
Sio mfano Mzee .

It's really.. nimeona stars kwenye mabega..

Sasa mm sijui, mchakato wa kupata hiko cheo inachukua muda.

Ninachojua ukiwa na Elimu kubwa ndio unapata promotion ya vyeo

Na jamaa na meet, alikuwa kashamaliza chuo, miaka kadhaa nyuma

Ni big brother kabisa kwangu..
 
before alikuwa mlinzi wa getini .. now ni Afisa habari Wizara ya kilimo
Hawa ni wengi sana hata Sugu alikua Mlinzi wa getini baadhi ya wachungaji ukimtoa Mwmposa wakisimulia simulizi zao watakwambia waliwahi kua walinzi magetini
 
Kaka, mm ni bachelor Holder, ila kazi ninayo fanya ,acha tu

Ila naamini Kuna siku nitakuwa mkubwa
HAlafu balaa ni kwamba kuna wadau wanasoma comment yako wanaweza kukuvusha Ila sasa wanakuacha uendelee kuwa mtumwa, you're a slave you keep on obeying your master na unalipwa ujira kidogo Pole sana mtumwa.

Sasa kuna watumwa wengi sana wenye maelezo kama yako huku wakiwa wamebebeshwa vyeti vinaitwa degree wengi hujisemea Mimi ni degree holder Ila kazi ninayoifanya acha tu yaan nilijua nikisoma nitapata kujikomboa Ila nimebaki kuwa mtumwa.

Pole tena mtumwa wewe ni mtumwa umepigwa minyororo na hata ukipata decent job utumwa wako hautoishia hapo wewe ni mtumwa mpaka unaingia kaburini, pole sana mtumwa

Nitaandika shairi lako mtumwa...
Pole sana mtumwa
 
Don’t worry bro,,,the best issue ni kutokata tamaa kamwe regardless of what they say,,,coz no one can live your life on your behalf. Keep on moving little by little you will reach your destiny.
Mtumwa mmoja anamfariji mtumwa mwingine, nice and sweet

Pole sana mtumwa
 
Huku kitaa kuna jamaa alikuwa anaokota makopo ni kichaa kabisa amevurugika juzi juzi tulimuona yuko kwenye msafara wa kiongozi fulani kavaa kaunda suti😁
 
Huku kitaa kuna jamaa alikuwa anaokota makopo ni kichaa kabisa amevurugika juzi juzi tulimuona yuko kwenye msafara wa kiongozi fulani kavaa kaunda suti😁
Hiyo haipo siku hizi hawafanyi hivyo.
 
Et mtu umheshimu kisa ana mafanikio ko asipokuwa na mafanikio unayotaka basi hastahili heshima , mtoa mada ni ndezi Sana , na ndo chanzo cha kutengeneza machawa , hii nchi vijana wamekuwa machawa na walamba miguu ya watu
Tuende poke, kwa upwndo, kwa kujengana, kwa kuelewa kuwa kuna wengi wanajifunza mambo, wanajifunza maisha.

Kitu kimoja nilichojifunza JF ni kwamba, hapa kuna watu wa kila aina, kila rila, kila uzoefu.

Kwa hivyo, unaweza kukuta watu wawili tofauti sana wanajibizana, na wasipojua kupeana nafasi ya kujibizana vizuri, kitakachofuata ni matusi.

Mtoa mada ya msingi sijui umri wala elimu rasni yake, wala upeo wake, ika nimependa sana alivyoandika.

Kitu kikubwa anafundisha au kukumbusha jamii ni kuheshimiana, kutochukuliana poa tu.

Hili ni somo zuri sana ambalo wengi tunaweza kulitumia, hata mimi.

Kitu kingine anachotufundisha ni juwa maendeleo yanahitajika, yanatuheshimisha, ni jambo ambalo linatupasa wote tulilenge.

Hapo sina cha kumpinga. Yumkini ukiwa na rafiki ambaye hana maendeleo, halafu ukakutana naye baada ya miaka michache ana maendeleo, hayo maendeleo aliyoyapata ni kitu kizuri, ni kitu cha kupigiwa mfano, si kitu cha kubezwa. Hapo sijampinga hata tone. Mimi pia hupenda kujifunza kwa watu, sio tu walioendelea zaidi yangu, bali hata wale waliojiendel3za kutoka walipokuwa mara ya mwisho mpaka walipo sasa ambao hawajaendelea kama mimi labda. Kitu muhimu ni kujua wamepigaje hatua. Maana dunia inabadilika kila simu, na pengine hata mimi ninayeweza kujiona niko zaidi yao, nikawa sijajua kupiga hatua kwa haraka na ufanisi zaixi katika dunia ya leo, nikajifun,a kitu kutoka kwao. Hapo sina tatizo.

Kwa hivyo, kimsingi, mtoa mada namuelewa sana na mambo aliyoandika ni ya msingi sana.

Nilitaka kukumbushia tu point moja ya msingi kwamba, watu wote wanastahili heshima. Waliofanikiwa na wasiofanikiwa.

Kwa sababu, kwanza, si watu wote wanaostahili heshima wanafanikiwa.

Watu wengine huwa wanaacha mambo yanayoweza kuwapa heshima katika jamii fulani - hususan kupata pesa na positions za uongozi- kwa sababu zenye kuweza kuwapa heshima ya juu zaixi ya habari za pesa na uongozi.

Kwa hivyo, unapokutana na, kwa mfano, mtu ambaye alipata nafasi ya kuibia wananchi na kuwa tajiri mkubwa sana, lakini hakufanya hivyo, akijua kuwa cheo ni dhamana, akafanya kazi kwa uadikifu, akastaafu vizuri bila kupita njia za rushwa, kwa mtazamo fulani akawa masikini, huyu ni mtu wa kuheshimiwa, si mtu wa kubezwa kwa sababu hakuiba mali za umma kama jamii yetu ilivyotarajia.

Kwa hiyo, heshima ipimwe kwa mambo mengi yenye kina, kuzidi mafanikio ya juu juu tu ya nani ana kazi gani, ana hela ngapi.

Tuangalie mchango mkubwa zaidi kwa jamii.
 
Supported
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…