Hatujafanya utafiti: Synovate | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatujafanya utafiti: Synovate

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by QUALITY, Oct 11, 2010.

 1. QUALITY

  QUALITY JF-Expert Member

  #1
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 854
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  HATUJAFANYA UTAFITI: SYNOVET
  Kwa wale wenzangu ambao mnafuatilia vyombo vya habari, haijapita wiki mbili tangu kampuni ya Synovet ilipotamka wazi kuwa hawajafanya utafiti kuhusu wagombea wa Urais. Ndani ya juma moja, wametoa matokeo. Mbona wanajikanganya? Unaweza kufanya utafiti nchi nzima, kufanya uchambuzi wa makini na kuchapisha taarifa ndani ya juma moja? Je hii inawezekana?
   
 2. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #2
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Hata me nimeshindwa kuelewa!
   
 3. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #3
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "In politics, a lie unanswered becomes truth within 24 hours." good kwamba umewaumbua mapema
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Oct 11, 2010
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Njia ya Mwongo siku zote ni fupi
   
 5. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #5
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  hivi ccm ina nguvu za fedha kiasi gani hadiwananunua kila wanachotaka?
   
 6. mwizalubi

  mwizalubi Member

  #6
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 62
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Ukisikia SIHASA ndio hiyo, wananchi wakishaambiwa Kikwete atashinda nao kisaikolojia wanakuwa wameshamchagua, na mwisho wa siku utasikia ameshinda kwa asilimia 81.

  Tusikate tamaa zimebaki siku ishirini kwa wale wote wanaopenda mabadiliko waende wakapige kura kuchagua upinzani ili Bunge liwe na changamoto,

  Upinzani Oyeeeeeeeeeeeeeeee,.... twendeni tukapige kura mwimize na mwenzio mwambie aache kulalamika kichinichini
   
 7. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #7
  Oct 11, 2010
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Kweli. Walamba makalio ya Mafisadi wako Wengi.
   
 8. k

  kilua New Member

  #8
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utaelewa tu.
   
 9. M

  MWANALUGALI JF-Expert Member

  #9
  Oct 11, 2010
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 601
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  CCM wanaweweseka sasa, CHADEMA wamewakamata pabaya!!! Kaza buti Dk wa ukweli tutayaona mengi tu. Hawa synovate wanachakachua utaqfiti wao wenyewe mpaka wanakosea wenyewe kwa kusema kuwa hawajafanya utafiti halafu kesho yake wanakuja na kutusomea utafiti uliofanywa na Makamba akisaidiana na Hizza!
  Mungu ibariki Tanzania.
   
 10. Endeleaaa

  Endeleaaa JF-Expert Member

  #10
  Oct 11, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 1,223
  Likes Received: 314
  Trophy Points: 180
  Hebu soma hiyo atiko ya mwananchi ya september 30 2010. Synovate wanakana hawakufanya utafiti wa anaekubalika katika kinyang'anyiro cha urais. hapo hapo serikali iliagiza matokeo ya tafiti zisizokidhi kama hizo za REDET na Synovate zizibitiwe maana hazijafikia kiwango. Sasa inakuwaje hao hao Synovate wanaruhusiwa kutangaza matokeo kwa public ambayo walikana kuyafanyia utafiti? wakati huo huo report yao inaonesha walifanya utafiti kati ya september 14 na 16?

  Lazima Synovate iwaombe radhi Watanzania kwa kuwadanganya kuwa hawajafanya utafiti wa mgombea urais anaekubalika zaidi wakati wanajua ukweli ni kuwa walifanya huo utafiti. Na kama hawakuufanya kama walivyoripotiwa september 30 2010. lazima waombe radhi watanzania kwa kuwapa taarifa ya uongo. Juu ya yote watulipe watanzania kwa kuzisumbua akili zetu.

  Here are the articles: penye hilite nyekundu ni jinsi synovate walivyojikanyaga, na hilite blue ni jinsi serikali ilivyo na inavyojikanyaga kwa kuruhusu tafiti kutangazwa hovyo.

  From Synovate report document

  MATOKEO YA KURA YA MAONI 10-10-2010
  Utangulizi
  Haya ni matokeo ya kura za maoni ambazo zilifanywa na kampuni ya Synovate
  Tanzania. Hi mojawapo ya mfulilizo wa kura za maoni ambazo Synovate wamekuwa
  wakifanya na kutangaza baada ya kila robo mwaka. Utafiti huu ulifanyika mwezi wa
  Septemba kati ya tarehe 5th and 16th 2010. Tulitembelea Mikoa yote ya Tanzania bara.
  Katika kazi yetu tulichagua kwa nasibu wilaya 63 kuwakilisha maoni ya Watanzania.
  Tuliwatumia wahoji 75 kukusanya data katika utafiti huu.

  gazeti la mwananchi waliripoti:

  Thursday, 30 September 2010 19:26
  0diggsdigg
  James Magai
  KUKIWA na tuhuma za kuzuiwa kutangaza matokeo ya tafiti za kisiasa, serikali imesema inajipanga kuweka mkakati wa kuhakikisha Chama cha Wanatakwimu (TAST) kinadhibiti matokeo ya tafiti zinazofanywa na taasisi zisizo za kiserikali au watu binafsi ili kuhakikisha kuwa ni sahihi.

  Katika siku za karibuni matokeo ya tafiti zilizofanywa na taasisi binafsi kuhusu hali ya kisiasa zilipingwa na baadhi ya wanasiasa ambao baadhi wanadai vigezo vilivyotumiki havikidhi utashi wa kisayansi kutokana na kuhusisha watu wachache na hivyo kutoa picha tofauti na hali halisi.

  Pia Chadema ilidai hivi karibuni kuwa taasisi ya Synovate ilitishwa na chama tawala na kuamua kutotoa matokeo ya utafiti wake kuhusu mgombea wa urais anayekubalika zaidi kwa sasa. Synovate imekana kufanya utafiti kama huo. Jana, mkurugenzi mkuu wa Idara ya Takwimu ya Taifa(NBS), Dk Albina Chuwa alitangaza mkakati wa kudhiti taarifa za matokeo ya tafiti zinazohusu umma wakati akizungumza na wandishi wa habari kwenye mkutano wa TAST jijini Dar es Salaam. Dk Chuwa alikuwa akiunga mkono kauli ya mgeni rasmi katika mkutano huo, Omar Mzee, ambaye ni Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi aliyezungumzia udhaifu wa takwimu ambazo zimekuwa zikitolewa katika tafiti nyingi zinazofanywa na taasisi zisizo za kiserikali.

  Alisema mkutano huo wa jana wa chama hicho ambacho alisema kilikuwa kimeanza kulegalega ni chachu ya kuboresha matumizi ya takwimu katika tafiti. "Kufufuliwa kwa chama hiki kutaboresha matumizi ya takwimu katika tafiti. Sasa tutahakikisha kuwa maadili ya matumizi ya takwimu katika tafiti yanafuatwa," alisdema. Tutahakikisha kuwa takwimu za tafiti kwa ajili ya matumizi ya umma zinathibitishwa na ili kujiridhisha kama ziko sahihi," alisisitiza Chuwa. Akifungua mkutano huo, Naibu Waziri Mzee alikiagiza chama hicho kusimamia na kuhakikisha kuwa takwimu zinazotolewa katika tafiti mbalimbali ni sahihi na zinakidhi maadili ya matumizi ya takwimu.

  Naibu waziri huyo, ambaye pia kitaaluma ni mtakwimu, alisema tafiti nyingi zinazofanyika nchini zinafanyika kiholela pasipo mpangilio, jambo ambalo halikidhi matwakwa ya tafiti. Alisema leo hii kuna tafiti ambazo zinafanyika kwa kuhusisha watu 10 lakini zinajumuisha watu 200,000 kama vile ndio msimamo wao wote, jambo ambalo si sahihi. "Kwa nini tunaacha tafiti hizi zisizo na mpangilio. Tusiayaache haya.

  Sisi ndio tunapaswa kuwaelekeza nini cha kufanya ili kuhakikisha kuwa takwimu zinazotolewa ni sahihi. Huwezi kutumia sampuli ya watu 10 kwa matokeo ya wilaya nzima," alisema naibu waziri huyo. Kutokana na tatizo hilo, Mzee alisema kila mtu anaweza kufanya utafiti kwa matumizi yake binafsi, lakini tafiti zinazofanywa kwa ajili ya matumizi ya taifa lazima takwimu zake ziwe zimepitiwa na kuthibitishwa na Idara ya Takwimu ya Taifa.


  Pia Mzee alikitaka chama hicho kuziunganisha sekta za umma na sekta binafsi katika matumizi ya takwimu kwa kuwa ndio watumiaj wakubwa wa takwimu. "Ninyi ni wazalishaji na private sector (sekta binafsi) ni consumer (watumiaji). Sasa mnakutana vipi... mnakutana? Je, ipo forum (jukwaa) ya kuwakutanisha," alihoji. "Bila kuwa na forum ni matatizo. Angalieni namna ya kukutana nao ili nao wawaeleze maoni yao. Muandae vikao vya mara kwa mara na watumiaji ili nao watuambie maoni yao vinginevyo tutazalisha tu bila watumiaji."
   
 11. K

  Kihega JF-Expert Member

  #11
  Oct 12, 2010
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 1,338
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Synovate walichofanya ni kuhesabu wingi wa mabango yanayomnadi JK ktk jiji la Dar na kwingineko then wakafanya uchakachuaji uliokubuhu.Hakuna zaidi ya hilo,si mnakumbuka JK moja ya ahadi zake ni kutoa ajira kwa waganga njaa wa aina ya Synovate?:A S 13::A S 13:
   
 12. YeshuaHaMelech

  YeshuaHaMelech JF-Expert Member

  #12
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 2,624
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  I can't believe the law of contradiction is not known to such wasomi :A S 13:
   
 13. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #13
  Oct 12, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,211
  Likes Received: 313
  Trophy Points: 180
  Mwandishi mmoja wa habari atusaidie kuwauliza Synovate mbona walisema hawajafanya utafiti na sasa wanatangaza matokeo ya utafiti kisha atuandikie kwenye gazeti.
   
 14. bullet

  bullet JF-Expert Member

  #14
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 959
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 45
  Inasemekana ukitaka kuwa mwongo mzuri basi uwe na kumbukumbu nzuri. Synovate hata kwa uongo si wazuri sana maana kama wanasahau kile walichokisema chini ya wiki tatu zilizopita, hata utafiti wao hauwezi kuwa na maana! Tatizo wanafikiri kila mtu ni msahaurifu.
   
 15. W

  We know next JF-Expert Member

  #15
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hayo ni matokeo ya kuwa na Serikali au uongozi ambao hakuna uwajibikaji, matokeo yake ndiyo hayo, kila kitu ubabaishaji tu, inachefua Tanzania kwa kweli.
   
 16. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #16
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kama unaamini kuwa Synovate haijafanya utafiti basi at least ama kwa Kiswahili tunasema kwa uchache kubalini kuwa mgombea wenu Slaa na Mwenyekiti wenu wa Bills Club walikuwa wanadanganya pale walipowatangazia kuwa Synovate imefanya utafiti kuonyesha Slaa anaongoza huo utafiti. Lakini hili ni gumu kufanya kwani kufanya hivyo ni sawa na kujitia dole.
   
 17. Job K

  Job K JF-Expert Member

  #17
  Oct 12, 2010
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 6,824
  Likes Received: 2,765
  Trophy Points: 280
  Usitulazimishe kukubali upupu jamaa yangu! Wao wenyewe ndo walijikanganya kuwatangazia wa-TZ kuwa hawajafanya utafiti halafu baada ya muda mfupi wanatoa takwimu za JK kuongoza ataongoza wapi bwana hata vijijini wameshastukia deal? Ni afadhali hata wangesubiri wakatoa matokeo yao wiki ya mwisho ya Oktoba tungewaelewa!! Hivi na huyu meneja wao mbona kama M-Kenya vile? Asituletee mambo ya huko kwao hapa bwana!!
   
 18. Kudadeki

  Kudadeki JF-Expert Member

  #18
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 859
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mbona unajipiga chenga mwenyewe. Sasa unaamini kuwa Synovate hawakufanya utafiti kwanini ulimuamini Slaa na yule Mzee wa Billicanas Club kuwa Synovate wamefanya utafiti na Slaa anaongoza kwenye utafiti huo? Acha kuruka viunzi!:tonguez:
   
 19. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #19
  Oct 12, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Semeni kwa staili yoyote mimi lazima nikapige kura, na slaa ndo chaguo langu.
   
 20. S

  SUWI JF-Expert Member

  #20
  Oct 12, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haahahha! Una hasira ( :decision:kujitia dole?) sio kosa lako ni kosa la hao mafisadi wakiongozwa na Kikwete waliosababisha CCM ikose mwelekeo na kupoteza maana kwa WATANZANIA na matokeo yake wameamu kukipiga chini. Pole sanaaaaa...
   
Loading...