OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 419
- 670
Utafiti uliofanywa kwa ushirikiano wa Sabancı University, Nukta Africa, Utah State University na University of Pennsylvania. Umebaini kuwa mbali na uwepo wa sheria kandamizi watanzania huendelea kutoa Mawazo yao kwa uhuru ndani ya JamiiForums.
Utafiti huu uliofanywa na Fatih Serkant Adiguzel, Nuzulack Dausen, Diego Romero na Erik Wibbels ulichunguza athari za Sheria ya Uhalifu wa Mtandao ya 2015 nchini Tanzania kwa tabia za mtandaoni za wananchi, ambapo waliangalia kwa kuzingatia mijadala inayoendela Jamii Forum. Watafiti walikusanya data kutoka kwenye mada za kisiasa kwenye Jamii Forums kuanzia mwaka 2006 hadi 2021, ambapo walipata jumla ya machapisho milioni 11.5. Walibainisha machapisho yanayohusiana na watendaji wa serikali kwa kutumia maneno muhimu. Uchambuzi wa hisia ulifanyika kwenye machapisho haya. Utafiti pia ulichunguza idadi ya akaunti mpya na zile zilizokuwa hazishiriki mijadala jukwaa.ni
Matokeo ya utafiti huu ni kuwa, Kiasi kikubwa cha machapisho ya kisiasa kiliongezeka kabla ya utekelezaji wa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao (Septemba-Novemba 2015). Kipindi hicho kiliambatana na uchaguzi, na sheria haikuonekana kuzuia mjadala wa kisiasa jukwaani.
Pia akaunti nyingi hazikuwa zinashiriki mijadala kabla na baada ya sheria kuanza kutumika kikamilifu mwezi wa Septemba, ikionyesha kwamba sheria ya ukandamizaji iliathiri tabia ya mtandaoni ya idadi kubwa ya wananchi waliokuwa na akaunti za awali.
Aidha kulikuwa na ongezeko za kufanya mijadala kwa watumiaji wapya muda mfupi kabla ya Sheria ya Uhalifu wa Mtandao kuanza kutumika kikamilifu, na idadi kubwa ya akaunti mpya ziliongezeka. Hata hivyo, ongezeko hili lilisimama mara tu sheria ilipoanza kutumika.
Uchambuzi wa hisia ulionyesha kuwa akaunti mpya na zile zilizokuwa hazifanyi mijadala zilikuwa na hisia sawa kuelekea watendaji wa serikali. Hii inaonyesha kwamba baadhi ya wananchi huenda walifungua akaunti mpya kwa mikakati huku wakiruhusu akaunti zao za awali kusimama ili kuepuka ukaguzi wa maudhui.
Watafiti hawa wamehitimisha kwa kuonesha kuwa Sheria ya Uhalifu wa Mtandao ya 2015 nchini Tanzania haikuzuia jumla ya machapisho ya kisiasa ya wananchi kwenye Jamii Forums. Ingawa baadhi ya akaunti zilisimama kwa muda lakini mijadala ya kisiasa dhidi ya watendaji wa serikali iliendelea.
Hii inaonesha wananchi wanaona wako salama ndani ya JamiiForums.
Hata hivyo, watu waliingia woga kidogo wiki moja baada ya sheria kufanya kazi, maelfu ya akaunti zilikuwa kimya na kulikuwa na ongezeko la akaunti mpya, japo si sawa na zile zilizokuwa kimya. Maana yake ni kuwa watu huweza kufungua akaunti mpya ili kuendelea na mijadala ikiwa tu anadhani akaunti yake ya awali inaweza kumletea sintofahamu.
Tafiti imebaini ni kweli sheria ilifanikiwa kuwanyamazisha baadhi ya wananchi na kuwazuia kushiriki kwenye majadiliano mtandaoni. Lakini kwa data za na matokeo ni kuwa watu wanaacha kutumika akaunti zao na kufungua mpya na kuendeleza moto.
Hii ndio Imani kubwa watu waliyonayo dhidi ya JamiiForums. Unaweza kuisoma tafiti hiyo hapa https://research.sabanciuniv.edu/id/eprint/48195/1/Jamii_Forum.pdf