Hatua sita za uumbaji

Hatua sita za uumbaji

Ww mshana kama mambo ya kichawi haugoogle ina maana wewe ni mchawi hadi unaujua uchawi vile?
Sasa huko gugo ndugu yangu kama yanapatikana si ningeshawekewa link za kuumbuliwa hapa? Kwa watu wako busy kutafuta hilo ujue
 
Biblia inasema kwa mungu miaka 1000 ni sawa siku moja na siku 1 ni sawa na miaka 1000.

Na kwanini ww mshana usiseme mungu aliuumba ulimwengu kwa miaka 6000 na miaka 1000 akapumnzika?
Swali lako la pili limajibiwa na la kwanza
 
Biblia inasema kwa mungu miaka 1000 ni sawa siku moja na siku 1 ni sawa na miaka 1000.

Na kwanini ww mshana usiseme mungu aliuumba ulimwengu kwa miaka 6000 na miaka 1000 akapumnzika?
Ngoja nisubiri jibu
 
Kaka, naomba unipe ufafanuzi na nijue kwa undani ni aina gani la tunda lililoongelewa mwanzo, ambalo liliwafanya adamu na eva kuanguka dhambini.
Kimsingi ni ngono lakini kuna mitazamo mingi sana ndio maana hata kanisa la leo dhambi ya kutubu rasmi ni kuzaa nje ya ndoa
 
Kimsingi ni ngono lakini kuna mitazamo mingi sana ndio maana hata kanisa la leo dhambi ya kutubu rasmi ni kuzaa nje ya ndoa
Lakini maandiko yanasema kuwa hawa aliporubuniwa na nyoka akala hilo tunda then akampelekea mumewe nae akala, hapa vipi hapa kama hilo tunda ni ngono?
 
Lakini maandiko yanasema kuwa hawa aliporubuniwa na nyoka akala hilo tunda then akampelekea mumewe nae akala, hapa vipi hapa kama hilo tunda ni ngono?
Alido kwanza na shetani(kubikiriwa?)kisha akampelekea mshikaji ndio maana inasemekana cain/kaini sio mtoto wa Adam
 
View attachment 362038Najua fika kwamba wengi watadhani ni ule uumbaji wa Kimungu uumbaji ule wa dunia na kila kilichopo
Hapa nazungumzia uumbaji wa uundaji japo kuna mfanano wa ajabu kwamba dunia iliumbwa kwa siku sita na ya saba ikawa mapumziko...lakini ukija kuangalia hiyo siku ya saba Aliyepumzika ni Mungu na si vile alivyoumba
Kimsimgi uumbaji hauna mwisho kazi ya kuumbwa inapokamilishwa na muumbaji, kilichoumbwa huanza safari ya kujiendeleza uumbaji...sasa kabla hatujafika huko hebu tuone hatua hizi sita za uumbaji
1. Hatua ya kwanza ni wazo... binadamu hushauriana na nafsi yake na ufahamu wake! Hapa ni yeye pekeyake baadae huwajulisha wengine nje ya ufahamu wake na nafsi yake au hufanya mwenyewe, dhana ya umoja na wingi! Mungu akasema na 'tuumbe mtu kwa mfano wetu'
2. Matayarisho: wazo linapokubalika matayarisho huanza ya vifaa ya pesa ya watu ya eneo nk nk...Mungu yeye alikwisha andaa bustani ya eden
3. Uumbaji: baada ya matayarisho yote muhimu kukamilika kazi ya uumbaji/uundaji huanza hapa Inategemea na ukubwa au udogo wa kitu , uundaji wa meli ni tofauti na uundaji wa kitanda, Mungu alitumia siku sita kuumba ulimwengu na kuunda kila kilichopo (siku sita hizi hatujui kwa hakika kama ni hizi tunazozijua ama la)
4. Kitu kipya hutokea baada ya uumbaji kukamilika, hiki ni kitu kipya baada ya kukamilika kazi ya uumbaji, kamwe hakiwezi kuwa kipya tena daima dawamu, wala huwezi kurudia ule mchakato hata iweje....kwamba kilichoumbwa kimeumbwa na ndio maana hata Mwenyezi Mungu baada ya uumbaji ule na maudhi aliyofanyiwa na nyoka kule mbinguni na Adam na Eva kule Eden hakuweza tena kuwateketeza au kuwarudisha alikowatoa au kutengua uumbaji wa dunia na kila kilichopo
5. Uchakavu: chochote kipya kitapotoka kuundwa huanza kuchakaa hapo hapo hata kama hakitatumika kitachakaa tuu....mtoto anapozaliwa amezaliwa huwezi kumrudisha tena tumboni mwa mama yake
6. Mwisho wa matumizi, kifo kuoza na kuanza mchachato mwingine wa uumbaji...kwamba ipende unavyoipenda gari yako au nyumba yako au nguo nk..kila siku inayopita ndio inaelekea kaburi la uchakavu, au chuma chakavu uzee na hatimaye kifo na kuwa recycled tayari kwa matumizi mengine mapya aidha kwa mtindo ule ule au(reborn) au kwa matumizi mengine (reincarnation)
Kwahiyo uumbaji hauna mwisho vitu vinaundwa vinatumika vinazeeka kuharibika na kutumiwa kwa matumizi mengine
Upende mwili wako uupendavyo lakini kamwe hutakuwa wewe wa jana na wa sasa hutakuwa wewe wa kesho
Tunakuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwenye vitu...vile tuvipendavyo sana hatutaki vituondoke, na hutumia hata nguvu za ziada kuvihodhi, vile tusivyovipenda tunataka vituondoke haraka...ni kanuni ya kiasili ya binadamu
Hakuna kidumucho milele, hatua sita za uumbaji huzunguka kwenye gurudumu lisilo na mwisho...
KUMBUKA: ZIJAPOPITA SIKU ZA FURAHA USIHUZUNIKE BALI UFURAHI KWAKUWA ZILIKUWEPO
Ishi kwa tafakuri kuu...Alamsiki...!!!
Hivi mwenyezi mungu mwenye uwezo wa kuumba kitu kwakusema "KUA NA KINAKUA" anaweza kufanya kazi na kuchoka mpaka kufikia hatua ya kuamua kupumzika kwa uchovu?

Quran 46:33
Je! Hawaoni ya kwamba Mwenyezi Mungu, aliye ziumba mbingu na ardhi, na hakuchoka kwa kuziumba, kuwa ni Muweza wa kuwafufua wafu? Kwani? Hakika Yeye ni Muweza wa kila kitu.
 
Jitahidi usipingane na imani Za wengine ila uziheshimu
 
Kimsingi ni ngono lakini kuna mitazamo mingi sana ndio maana hata kanisa la leo dhambi ya kutubu rasmi ni kuzaa nje ya ndoa
Sasa kama ni ngono alikua na maana gani?kuwaambia enendeni mkazaliane muijaze nchi?
 
Na ndio maana nikasema hapo kwenye mada kuwa uumbaji wa kwanza ulikamilika baada ya siku sita baada ya hapo kila kitu kiliingia kwenye automation mode
-mwanadamu aliyeumbwa na Mungu si huyu wa sasa..! Sasa hivi kuna Kituko
-Dunia iliyoumbwa na Mungu sio hii ya sasa... sasa hivi kuna mfano wa dunia, wanyama mimea hata vitu vunavyotuzunguka
Kimsimgi kilichopo sasa ni
Binadamu toleo la mwisho
Wanyama toleo la mwisho
Mimea na nk toleo la mwisho watu wameji edit mpaka wamekuwa kama vinyago
Teh teh teh! Hua nikitazama mambo wanayofanya wanadamu mpaka napataga ukakasi wa kusema MUNGU kawaumba,maana watu ni wanamatendo ya ajabu etii..ah acheni tu,binadamu?! ni hatari
 
Teh teh teh! Hua nikitazama mambo wanayofanya wanadamu mpaka napataga ukakasi wa kusema MUNGU kawaumba,maana watu ni wanamatendo ya ajabu etii..ah acheni tu,binadamu?! ni hatari
Sidhani kama hiki ndio kile kizazi cha Mungu tunayemfahamu na kuhubiriwa sana! Kiuhalisia hiki ni kizazi kingine kabisa
Kizazi cha elimu dunia na maisha ya pesa na vitu ! Ndio maana kufuru haiishi ya kumkana Mungu ! Bahati mbaya sana wanafanya hivi wakiwa bukheri wa afya huko mjini kwenye mataa na mwendokasi, natamani siku moja niwachukue ziara niwalete huku niliko usiku huu (search location utajua )
 
Wanyama wanazaana na kuongezeka je ile ni ngono?
Nazungumzia adamu kula tunda la katikati,ni kwamba walifanya ngono?au anaposema tunda la mti wa mema na mabaya alikua na maana gani?

Hebu nijibu kwanza maana tukienda kwa muktadha wa kuulizana maswali bila majibu haitatusaidia sisi na wasomaji
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom