Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,715
- 729,889
Hapa nazungumzia uumbaji wa uundaji japo kuna mfanano wa ajabu kwamba dunia iliumbwa kwa siku sita na ya saba ikawa mapumziko...lakini ukija kuangalia hiyo siku ya saba Aliyepumzika ni Mungu na si vile alivyoumba
Kimsimgi uumbaji hauna mwisho kazi ya kuumbwa inapokamilishwa na muumbaji, kilichoumbwa huanza safari ya kujiendeleza uumbaji...sasa kabla hatujafika huko hebu tuone hatua hizi sita za uumbaji
1. Hatua ya kwanza ni wazo... binadamu hushauriana na nafsi yake na ufahamu wake! Hapa ni yeye pekeyake baadae huwajulisha wengine nje ya ufahamu wake na nafsi yake au hufanya mwenyewe, dhana ya umoja na wingi! Mungu akasema na 'tuumbe mtu kwa mfano wetu'
2. Matayarisho: wazo linapokubalika matayarisho huanza ya vifaa ya pesa ya watu ya eneo nk nk...Mungu yeye alikwisha andaa bustani ya eden
3. Uumbaji: baada ya matayarisho yote muhimu kukamilika kazi ya uumbaji/uundaji huanza hapa Inategemea na ukubwa au udogo wa kitu , uundaji wa meli ni tofauti na uundaji wa kitanda, Mungu alitumia siku sita kuumba ulimwengu na kuunda kila kilichopo (siku sita hizi hatujui kwa hakika kama ni hizi tunazozijua ama la)
4. Kitu kipya hutokea baada ya uumbaji kukamilika, hiki ni kitu kipya baada ya kukamilika kazi ya uumbaji, kamwe hakiwezi kuwa kipya tena daima dawamu, wala huwezi kurudia ule mchakato hata iweje....kwamba kilichoumbwa kimeumbwa na ndio maana hata Mwenyezi Mungu baada ya uumbaji ule na maudhi aliyofanyiwa na nyoka kule mbinguni na Adam na Eva kule Eden hakuweza tena kuwateketeza au kuwarudisha alikowatoa au kutengua uumbaji wa dunia na kila kilichopo
5. Uchakavu: chochote kipya kitapotoka kuundwa huanza kuchakaa hapo hapo hata kama hakitatumika kitachakaa tuu....mtoto anapozaliwa amezaliwa huwezi kumrudisha tena tumboni mwa mama yake
6. Mwisho wa matumizi, kifo kuoza na kuanza mchachato mwingine wa uumbaji...kwamba ipende unavyoipenda gari yako au nyumba yako au nguo nk..kila siku inayopita ndio inaelekea kaburi la uchakavu, au chuma chakavu uzee na hatimaye kifo na kuwa recycled tayari kwa matumizi mengine mapya aidha kwa mtindo ule ule au(reborn) au kwa matumizi mengine (reincarnation)
Kwahiyo uumbaji hauna mwisho vitu vinaundwa vinatumika vinazeeka kuharibika na kutumiwa kwa matumizi mengine
Upende mwili wako uupendavyo lakini kamwe hutakuwa wewe wa jana na wa sasa hutakuwa wewe wa kesho
Tunakuwa na mapenzi yaliyopitiliza kwenye vitu...vile tuvipendavyo sana hatutaki vituondoke, na hutumia hata nguvu za ziada kuvihodhi, vile tusivyovipenda tunataka vituondoke haraka...ni kanuni ya kiasili ya binadamu
Hakuna kidumucho milele, hatua sita za uumbaji huzunguka kwenye gurudumu lisilo na mwisho...
KUMBUKA: ZIJAPOPITA SIKU ZA FURAHA USIHUZUNIKE BALI UFURAHI KWAKUWA ZILIKUWEPO
Ishi kwa tafakuri kuu...Alamsiki...!!!