Hatua 7 kuelekea udikteta kamili

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,587
9,665
(sio lengo langu kumkosea heshima yeyote, ni uhuru tu wa mawazo kwa mujibu wa katiba)

Kwa viongozi waliochaguliwa kidemokrasia kujilimbikizia madaraka huwa changamoto kidogo kwao, lakini wengi hupiga hatua zifuatazo kuelekea kuwa ma dikteta kamili

1. Kujiongezea wigo wa mamlaka kupitia undugu/ukabila na rushwa
kwakua katika mfumo wa kidemokrasia swala la kujiongezea madaraka lina ugumu kidogo, madikteta huhakikisha wanazungukwa na watu wao wa karibu kwenye vitengo nyeti ili kujihakikishia usalama wao na familia zao, na pia inawarahisishia kupindisha sheria inapowabidi

2. Kujihakikishia mamlaka ya juu zaidi kwenye vyombo vya dola ili kuzima sauti za wananchi
madikteta hawawezi ku survive kunapokuwa na uhuru wa watu kujieleza na kutoa maoni yao, hivyo basi wao hujihakikishia wanavishika vyombo vyote vya dola na kutoa maelezo ya namna ya kuwashughulikia wananchi wanao onekana kupingana na sera zao (maelezo toka juu)

3. Kuboresha miundo mbinu na huduma za kijamii kwa minajili ya kujiongezea umaarufu
pengine hii ndio sababu kuu kabisa inayosababisha watu wengi wavumilie tu kutawaliwa na dikteta, siku zote madikteta hujitahidi kuanzisha miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu na wakati mwingine hufanikiwa vizuri sana kwenye kukuza uchumi wa nchi, hii hua ni kete muhimu sana kwao kwani huitumia kuwaaminisha wananchi kua hakuna haja ya kutafuta kiongozi mwingine wakati aliyepo ana preform vizuri

4. Kuwapoteza maadui zao wa kisiasa
hapa kuna njia tatu zinazo tumika, ya kwanza ni kuwa angamiza kabisa (wanazo resources za kuweza kufanya hivyo), ya pili ni vitisho (wale waoga hukaa kimya wenyewe) na ya tatu ni kuwateua wakosoaji wako kwenye nafasi mbalimbali serikalini hivyo kuwanyamazisha kabisa kwakua watakua bize kulinda matumbo yao.

5. Tengeneza matatizo/maadui na kisha kujifanya wanayatatua/kuyashinda
hili linajieleza

6.Kujiongezea madaraka zaidi na zaidi kwa kucheza na mioyo na akili za wananchi wao
Hapa madikteta hucheza na vyombo vya habari, watahakikisha wana minya uhuru wa habari na kugeuza media kuwa mashine ya propaganda na hivyo kueneza propaganda zitazo wafunga wananchi vichwa vyao na kukonga mioyo yao.

7. Kuanzisha itikati itayo halalisha nafasi na madaraka yao
movement kama vile uzalendo, utaifa na nyinginezo huanzishwa si kwasababu madikteta ni wazalendo sana au labda wanaipenda nchi kuliko watu wengine, bali ni harakati tu za kuhakikisha wanakua na itikadi ya kuwafanya waonekane

/*loosely based on an article published by Mark van Vugt, Ph.D, a professor of social and organizational psychology at the VU University Amsterdam and a research associate at Oxford University.*/
 
Building a nation vs dictatorship : case study on Mwalimu Nyerere by Dr. E. Michael Jones


Source: E. Michael Jones
 
Utawala huu watu wataokotwa sana Coco Beach. Polisi kwanini hawaongezi ulinzi kwenye ufutwe ule ili kuwakamata wauaji?
 
Madikteta wote wanapita njia ileile
Pia Sifa zao kuu,huwa hawana Furaha,Amani wala utulivu wa moyo wako frastuated sababu ya masharti wapewayo,ni waoga ukali ndo silaha yao,uogopa jela ndo maana hawataki kuachia madaraka sababu wamejijengea maadui wengi, wazulumati,washirikina eg yule wa Gambia,Iddi amin nk,wazinzi.huwa na mwisho mbaya sababu dunia ni ya Mungu.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom