Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

Jenerali amesema kitu nilichowahi kusema hapa, watwawala wetu si kweli kwamba hawawezi kuondoa umasikini wetu, bali hawana nia hiyo tu.
 
RWANDA ya KAGAME. Mimi naishangaa Tanzania yetu. Nchi kama Marekani ina raia wa nchi zote duniani na imeendelea kwelikweli tena kwa kuzitumia mbongo na vipaji vya raia hawa "wakuja"!

Wildcard; you have a point!
Na ukijiuliza vizuri, ni yupi anayetufaa, mtu asiye raia ila productive kwetu au mtu ambaye ni raia ila fisadi?
 
Mmmmh, kumbe Kitine ndiye aliyeanzisha ishu ya uraia wa Jenerali...
 
Wapendwa huwa sipendi kuweka nakala za gazeti hapa kwa sababu naona kama si kuwatendea hako wenye gazeti ila kwa hii nakala naona nivunje mwiko hapa hiyo para ya mwisho
Shalom aksante kwa makala hii imetulia sana...!
 
Mmmmh, kumbe Kitine ndiye aliyeanzisha ishu ya uraia wa Jenerali...

ningependa kuongelea kitu kimoja tu hapa, Pamoja na Tanznaia kuwa ni kama nchi isiyo na misimamo na ufisadi mkubwa, lakini ni ukweli usipingika kuwa idara ya usalama kitengo cha kuwafatilia watu kina dat za kutosha sana, hii issue ya kuwa huyu ni raia na huyu sio, sidhani kama hawa jamaa huwa wanakurupuka tu, wana evidence za kutosha katika haya mambo, na kuna kitu kingine ambacho watu wengi tunashindwa kukijua kuhusu hizi sheria za uraia au ni vipi mtu anakuwa raia na vipi anakuwa sio raia,
mfano mdogo tu ambao ndio nahisi uliomtokea Ulimwengu ni kuwa, kama wazazi wake hawakuwa raia wa Tanganyika say ni wa Rwanda, na walikuwa Tanganyika wakati wa wakati wa kuform Tanzania, basi automatically nao wanakuwa raia wa Tanzania (kWA MUJIBU WA SHERIA) LAKINI WAKITAKA SIO KWA KUWALAZIMISHA, KAMA WAZAZI WAKE HAWAKUKUBALI KUCHUKUA URAIA WA TANZANIA BASI WALIKUWA WANAKAA TANZANIA KAMA WAGENI JAPO WALIKUWEPO WAKATI KUFORM TANZANIA, sasa mtoto atakaye zaliwa atakuwa na haki ya uraia wa nchi mbili ama tatu kutokana na asili za wazazi wake, kama baba na mama yake ni wa nchi moja basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi mbili, nchi ya wazazi wake na nchi aliyozaliwa, kama wazazi wake wanatoka nchi tofauti basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi tatu (baba, mama, ya kuzaliwa), LAKINI MTOTO ANAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NANNE NI LAZIMA AKANE RAIA ZINGINE NA KUBAKI NA URAIA WA NCHI MOJA, HAPA NDIPO KWENYE TATIZO KUBWA, WATU WENGI HUWA WANAJISAHAU NA KUJIONA NI RAIA WA KUZALIWA BILA KUCONSIDER URAIA WA WAZAZI WAKE
NA WATU WENGI WANAISHI HIVYO NA TUNAO MITAANI, TATIZO KUBWA LINAKUJA UNAPOTAKA KUINGIA KWENYE SIASA NA SIO KUINGIA TU BALI KUFUKUNYUA NA KUTAFUTA HAKI KUTOKA KWENYE SIASA, HAPO NDIPO MAKABRASHA YATAKAPOENDA KUFUNGULIWA NA KUAMBIWA WEWE SIO RAIA
 
Bravo Jenerali Ulimwengu!! You dare speak openly!!! Ila I am afraid nchi yetu haina uhuru wa habari, na sitashangaa wakikuandikia barua za kukuonya eti usiandike masuala ya kuwachanganya wananchi na kuleta vurugu!! Nchi kama Rwanda inatamani sana iwapate watanzania waende kule kufanya kazi hata zile sehemu nyeti, na Kagame alishatangaza hilo. Alisema atafurahia sana hii Federation maana atafaidi sana vichwa vya kutoka nchi nyinginezo!! Vijembe vijembe ndani ya chama. Je tutafika!!
 
Wapendwa huwa sipendi kuweka nakala za gazeti hapa kwa sababu naona kama si kuwatendea hako wenye gazeti ila kwa hii nakala naona nivunje mwiko hapa hiyo para ya mwisho

Nimeisoma ile habari nikapata picha halisi kuwa CCM ni chama cha kihuni yaani wanakuvictimise just kwa kuwa hutakiwi ndani ya chama. Na nimeipenda statement ya kuwa kama Bashe si raia mbona Mkulo hakujatolewa tamko lolote kuhusu uraia wake. Ikiwa Bashe msomali mbona kuna wanachama waandamizi ni wasomali na hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa (i.e. Kinana). Hizi ni zama za anguko la CCM wananchi tunaanza kuona uozo wa ndani ya CCM na inasikitisha kwa kweli
 
ningependa kuongelea kitu kimoja tu hapa, Pamoja na Tanznaia kuwa ni kama nchi isiyo na misimamo na ufisadi mkubwa, lakini ni ukweli usipingika kuwa idara ya usalama kitengo cha kuwafatilia watu kina dat za kutosha sana, hii issue ya kuwa huyu ni raia na huyu sio, sidhani kama hawa jamaa huwa wanakurupuka tu, wana evidence za kutosha katika haya mambo, na kuna kitu kingine ambacho watu wengi tunashindwa kukijua kuhusu hizi sheria za uraia au ni vipi mtu anakuwa raia na vipi anakuwa sio raia,
mfano mdogo tu ambao ndio nahisi uliomtokea Ulimwengu ni kuwa, kama wazazi wake hawakuwa raia wa Tanganyika say ni wa Rwanda, na walikuwa Tanganyika wakati wa wakati wa kuform Tanzania, basi automatically nao wanakuwa raia wa Tanzania (kWA MUJIBU WA SHERIA) LAKINI WAKITAKA SIO KWA KUWALAZIMISHA, KAMA WAZAZI WAKE HAWAKUKUBALI KUCHUKUA URAIA WA TANZANIA BASI WALIKUWA WANAKAA TANZANIA KAMA WAGENI JAPO WALIKUWEPO WAKATI KUFORM TANZANIA, sasa mtoto atakaye zaliwa atakuwa na haki ya uraia wa nchi mbili ama tatu kutokana na asili za wazazi wake, kama baba na mama yake ni wa nchi moja basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi mbili, nchi ya wazazi wake na nchi aliyozaliwa, kama wazazi wake wanatoka nchi tofauti basi mtoto anakuwa na uraia wa nchi tatu (baba, mama, ya kuzaliwa), LAKINI MTOTO ANAPOFIKISHA UMRI WA MIAKA KUMI NANNE NI LAZIMA AKANE RAIA ZINGINE NA KUBAKI NA URAIA WA NCHI MOJA, HAPA NDIPO KWENYE TATIZO KUBWA, WATU WENGI HUWA WANAJISAHAU NA KUJIONA NI RAIA WA KUZALIWA BILA KUCONSIDER URAIA WA WAZAZI WAKE
NA WATU WENGI WANAISHI HIVYO NA TUNAO MITAANI, TATIZO KUBWA LINAKUJA UNAPOTAKA KUINGIA KWENYE SIASA NA SIO KUINGIA TU BALI KUFUKUNYUA NA KUTAFUTA HAKI KUTOKA KWENYE SIASA, HAPO NDIPO MAKABRASHA YATAKAPOENDA KUFUNGULIWA NA KUAMBIWA WEWE SIO RAIA

Hivyo bwana Kituko unataka kutwambia kuwa wazazi wa Bashe walikuwa hawalijui hilo? Au unataka kujistify decision ya Kamati kuu ya chama? Na je kama hakuwa raia mbona CCM walikuwa wakimpa vyeo lukuki tu inamaana ndani ya CCM hakuna mtu aliyeliona hilo akaliweka sawa kabla haijafika huku? Huu ni unafiki tu acha kutuzingua.
 
Ukisoma kwa undani hii makala ni Jenerali yeye anataka kumlipua KITINE period, kwani hajaongelea kabisa mapungufu ya sheria kama yapo. Kingine anachoongelea ni kuwa mbona wengine hawachunguzwi uraia wao? Sasa inanipa shida hapa tunaanza kusheherekea kuwa kintine alikuwa ndo amemmaliza, kwa nini tusiombe waandishi wengine wamfate KITINE wamuulize ili tupate upande mwingine. N ni kwa nini Twaha hataki kueleza kwa undani, wakati ule si aliambiwa sheria huwa hivi, kama kuna mahali unaona umeonewa basi nenda mahakamani, sasa kwa nini alivyata? Hili swala liko open saana kwa nchi kama yetu ambayo watu hawako registered ni rahisi saana kuwa mamluki, lakini inapofikia unaingia kwenye nafasi nyeti na watu wakaja kuhoji uraia wako ni lazima watu wafuatilie, na hii ndo imemkuta Bashe.
 
Hapana...nia haikuwa hivyo ndio maana makala nzima hakuna pahala jina la Kitine kutajwa....ni sisi tumeelewa hivyo....nia ya Jenerali ni kumwonya Chiligati asifananishe suala la utata wa uraia wa uchaguzi wa 2010 na la kwake kwa kuwa yeye alipopata matatizo ya uraia hakuwa anagombea cheo na nyakati na mazingira ni tofauti...angetaka kumuumbua au kumlipua kama utakavyo wewe Kitine angefanya hivyo years ago.....Kama Kitine nae anayake ya kusema aseme na wala si jukumu la JF kufanaya hivyo kwa sababu Jenerali hakumtaja Kitine kwenye makala yake...Tusitoke nje ya mada
 
Safai_ni_safari
Naomba urudi ukaisome tena mtu anyetajwa hapo ni Kitine, ametumia fani yake tu kumzunguka na kutumia kauli ya Chiligati ili amlipue KITINE. Sasa mimi nakuomba wewe hebu muulize ni kwa nini aligoma kwenda mahakamani?
 
Nami nimemsoma Jenerali. Lakini angetutendea haki zaidi kama angeeleza alilimalizaje sakata lile. Pengine ingekuwa msaada mkubwa kwa wengine ambao naamini wako wengi wanaokumbana dhahma kama hii. Kuwashambulia Kitine na Mkapa ambao tayari ni "spent forces" hakujatusaidia sana mashabiki na wasomaji wake. Baadhi yetu tulikuwa tunajua waliomwandama.

hao wawili ni spent forces mkuu...

kuna mmoja msomali kamtaja... he is still in force...

unamjua? ni ofisa mstaafu wa jeshi...

yupo kila pahala nyeti... kamati kuu.. halmashauri kuu...

na hata kwenye kamati ya mwinyi nae alikuwemo.........
 
Nimeisoma ile habari nikapata picha halisi kuwa CCM ni chama cha kihuni yaani wanakuvictimise just kwa kuwa hutakiwi ndani ya chama. Na nimeipenda statement ya kuwa kama Bashe si raia mbona Mkulo hakujatolewa tamko lolote kuhusu uraia wake. Ikiwa Bashe msomali mbona kuna wanachama waandamizi ni wasomali na hakuna ufafanuzi wowote uliotolewa (i.e. Kinana). Hizi ni zama za anguko la CCM wananchi tunaanza kuona uozo wa ndani ya CCM na inasikitisha kwa kweli

hapo kwenye bold mkuu...

mimi najitoa katika wenye kusikitika kuona CCM ikianza kujichinja yenyewe kwani ni kawaida kuwa milki zote za kidunia hatimaye huanguka na milki mpya kunyanyuka..

nenda CCM kale ugali na mwalimu
 
Safai_ni_safari
Naomba urudi ukaisome tena mtu anyetajwa hapo ni Kitine, ametumia fani yake tu kumzunguka na kutumia kauli ya Chiligati ili amlipue KITINE. Sasa mimi nakuomba wewe hebu muulize ni kwa nini aligoma kwenda mahakamani?

Hapana..hata pamoja na sourness ya hiyo paragraph inayomlenga Kitine,the main issue kwake kwa uelewa wangu ni kwa nini Chiligati ameunganisha issue ya Bashe na ya Kwake...kama angalitaka kumlipua Kitine kwa nini wakati huu amabapo yeye na Kitine hawana mgongano wowote uwe wa kimaslahi au kiitikadi? KITINE mwenyewe kwishney kwa sasa
 
hapo kwenye bold mkuu...

mimi najitoa katika wenye kusikitika kuona CCM ikianza kujichinja yenyewe kwani ni kawaida kuwa milki zote za kidunia hatimaye huanguka na milki mpya kunyanyuka..

nenda CCM kale ugali na mwalimu

Kaka humo mie simo nimeamua ni bora nikae sina chama chochote kwani CCM kumeoza na upinzani siwaamini nawaona kama opportunist wanakuwa na hidden ajenda behind nilishasema tangia zamani. Nasikitikia wale walamba miguu wanaokubali kula kila kitu nawatakia kila la kheri
 
Jenerali T.K.O. Ulimwengu alikuwa prefect wa bweni fulani pale Tabora School mwanzoni mwa miaka ya sitini, nadhani ilikuwa ni kati ya mwaka 1963 au 1965 hivi- watu walioko TS wanaweza kunikumbusha kama bado ile list majina ya maprefect wa zamani imetundikwa pale dining hall. Niliposikia kuwa eti yeye siyo raia wa Tanzania, nilishangaa sana kwani wakati ule tulikuwa na serikali ambayo ilikuwa inafanya kazi zake sawasawa kiasi kuwa isingekuwa rahisi kwa raia wa nje kusoma kwenye sekondari za serikali bila kufahamika.
 
Rai ya Jenerali said:
-------------------
WIKI jana nilijadili suala la watu wazito, wenye nyadhifa kubwa, wenye historia zinazoeleweka, na wenye wingi wa miaka inayowatambulisha kama wazee, lakini hujidharaulisha kwa kutoa matamko ya kipuuzi yasiyofanana na sifa hizo alimradi wajibu hoja za kudumu kwa majibu mepesi ya mpito. Wiki jana ilikuwa ni ya Pius Msekwa, Makamu wa Mwenyekiti wa CCM na matamko yake kuhusu uoza ndani ya chama chake.

Wiki hii tena, mzee mwingine wa CCM, Katibu wa Uenezi, John Chiligati, naye ameamua kujiingiza katika kundi hilo la kujisemea ‘bora liende".

Chiligati, yeye, ameamua kumzungumzia kijana wa CCM, Hussein Bashe, ambaye hivi majuzi tu, mjini Dodoma, amekatizwa safari yake ya kuwania ubunge kutokana na kile kilichoelezwa kuwa tatizo la uraia.

Chiligati aliwaelezea waandishi wa habari mjini Dodoma alfajiri ya Jumapili kwamba Bashe ameachwa katika mchujo wa wagombea kwa sababu yeye ni raia wa Somalia, na kwa hiyo si raia wa Tanzania. Aliongeza kusema kwamba chama chake kilifanya uchunguzi kikishirikiana na Idara ya Uhamiaji na ndipo ikagundulika kwamba Bashe si raia wa Tanzania, hata kama alizaliwa Tanzania.

Hadi hapo sioni tatizo. Tatizo linakuja pale Chiligati alipotamka kwamba kesi ya Bashe ni sawa na ile ya mwandishi wa makala hii , "aliyekuwa kada wa CCM" na akavuliwa uraia wake katika miaka ya nyuma.

Nakiri kungali na mapema kwamba haipendezi kwa mwandishi wa makala hii kutumia safu hii kuzungumzia suala linalomhusu binafsi. Nasema haipendezi, lakini ni halali katika hali fulani fulani. Nitajaribu kueleza hapa chini.

Wahaya husema kwamba mtu akibanwa mbavu kuhusu jambo alilotenda na akataka kusema uongo atasema, nkaba nyin'embwa yange. Nilikuwa pamoja na mbwa wangu. Maana yake ni kwamba, kama mnataka ushahidi wa hili ninalosema muulizeni mbwa wangu.

Kwa mitindo mbali mbali na katika mazingira tofauti hii ni silaha inayotumiwa na watu wanaotaka kusema uongo unaofanana na ukweli. Kwa mfano, inawezekana kweli Bwana Bigambo alikuwa na mbwa wake wakati wa tukio husika, lakini haiwezekani kwa mbwa wake kutoa ushahidi, kwa hiyo kuwapo au kutokuwapo kwa mbwa huyo hakuna uhusiano na ushahidi wa Bigambo. Anapoteza lengo tu, na ingawa kwa juu juu anasema ukweli (mbwa wake alikuwapo) lakini anasema uongo (mbwa hawezi kutoa ushahidi).

Ili kuwafariji akina Chiligati, ninaweza kuwaarifu kwamba hawako peke yao, kwani hata wakubwa wa dunia wanatumia vijisilaha kama hivyo wanapokuwa wameshikwa ‘pabaya.' Miaka kadhaa iliyopita, wakati Marekani wanang'ang'ana kwenda Iraq kumwondoa Saddam Hussein, Marekani walipambana na upinzani mkali mno kutoka kwa maswahiba wao wa Magharibi waliokataa kubariki vita ya Marekani dhidi ya Iraq. Tunamkumbuka Dominique de Vilpein, waziri wa mambo ya nje wa Ufaransa na jinsi walivyoshikana mashati (kwa maneno) ndani ya mkutano wa Baraza la Usalama.

Katika mabishano makali yaliyofanyika katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kila aina ya mbinu zilitumika kutetea upande huu na ule, kila mmoja akivutia upande wake. Ilikuwa dhahiri kwamba dunia haikukubaliana na mantiki ya Marekani kuivamia Iraq, na kwamba Marekani walikuwa wamedhamiria kufanya kile walichoazimia na kwamba wangetumia maguvu, hata kama Umoja wa Mataifa ungewakataza.

Lakini, kwangu mimi binafsi, tamko lililoashiria kuchoka kwa uchovu na ubabaishaji wa mantiki ya Marekani ni pale ofisa wake mwandamizi alipoiingiza Tanzania katika ubishi huo, kwa kutamka kwamba hata Tanzania ilipoivamia Uganda haikufanya hivyo kwa kibali cha Umoja wa Mataifa. Ati nkaba nyin'embwa yange.

Huyu msemaji wa Marekani alifanya purukushani (hii ndiyo maana halisi ya neno hili) kuhusu chanzo cha vita baina ya Tanzania na Idd Amin, yaani uvamizi alioufanya Amin dhidi ya Tanzania, na kwamba ilichofanya Tanzania ilikuwa ni kutumia haki yake ya msingi ya kujibu mapigo katika ulinzi wa ardhi yake. Msemaji wa Marekani alisema ukweli (Tanzania haikupata ridhaa ya Umoja wa Mataifa) wakati papo hapo akisema uongo (Iraq haikuivamia Marekani).

Mantiki ya nkaba niny'embwa yange huweza kupata mashiko miongoni mwa wasemaji na wasikilizaji waliojijengea utamaduni wa fikra nyepesi zinazotafsirika katika matamko mepesi sawia. Katika jamii iliyojizoeza kufanya mambo yake (pamoja na kufikiri) fasta-fasta, muhimili mmoja wa mtazamo wa maisha ni kwamba hutakiwi kuumiza kichwa chako kufikiri. Unachotakiwa ni kuwa mjanja ili uweze kubakia bambucha.

Hebu tuangalie Chiligati anasema nini kuhusu kijana Bashe na mwandishi wa safu hii. Kijana huyu alikuwa, hadi juzi (sijui leo) kada wa chama-tawala, tena kada wa msitari wa mbele ambaye amekifanyia kazi chama hicho hadi juzi. Mwandishi huyu wakati akivuliwa uraia hakuwa tena kada wa chama hicho, akiwa amehitilafiana na uongozi/utawala wa juu wa chama hicho kuhusu masuala ya msingi.

Kijana Hussein Bashe, ambaye sasa anatolewa kafara na wale alioamini ni wazee wake, alikuwa bado anayo hamu ya kukitumikia chama chake katika wadhifa wa juu zaidi. Mwandishi huyu alikuwa amestaafu ubunge na ujumbe wa NEC na alikuwa amejikita katika harakati za asasi za utetezi pamoja na uandishi na uchapishaji wa magazeti makini ambayo hayakusita kuiambia serikali na chama-tawala kwamba "mfalme yu uchi, na korodani zinaonekana."

Utamaduni wa uroho na kunyang'anyana matonge ndani ya chama-tawala, kama tulivyoushuhudia siku za hivi karibuni huzaa uchafu wa kila aina kiasi kwamba mtu anahitaji pua zenye sugu iliyoingia sugu ili asisikie uvundo unaotoka huko. Katika utamaduni huo, watu hutafunana wenyewe kwa wenyewe, wakubwa wakiwatafuna wakubwa wenzao, wakubwa wakivimeza vitoto vyao, na vitoto navyo viking'atang'ata visigino vya wazazi wao.

Naamini kwamba wamo watu ndani ya chama-tawala ambao hawakumtaka Hussein (kwa sababu walitaka mbunge wao) na wakaona kwamba mbinu ya kumzuia ni hiyo ya uraia, hasa kwa sababu sura yake inaashiria asili yake. Huyu wamemuweza, kwa sababu, pamoja na maneno ya Chiligati, bado ni dagaa, hajawa hata kambale, achilia mbali papa. Mbona wengine hawawagusi?

Katika majungu wanayopikiana ndani ya chama-tawala, baadhi ya wanachama wasiomtaka Mustafa Mkulo walipeleka pingamizi dhidi yake na wakaenda Dodoma kushadidia pingamizi yao wakati wa kikao cha NEC. Chiligati hakusema kama uamuzi juu ya Mkulo ulitoka ndani ya Idara ya Uhamiaji au ndani ya NEC. Kati ya Bashe na Mkulo bila shaka ipo tofauti.

Shauri analoliingiza Chiligati katika sakata ya Bashe ambalo linamhusu mwandishi huyu lilianza kwa watawala kutafuta njia ya kunyamazisha baadhi ya sauti za ‘kuudhi.' Kinara wa kampeni kuhusu uraia wa mwandishi huyu alikuwa ni kachero mwandamizi mstaafu ambaye kwa wakati huo alikuwa amelazimishwa kujiuzulu uwaziri katika serikali ya rafiki yake, Benjamin Mkapa, kwa sababu alikuwa amegundulika na gazeti la mwandishi huyo kuhusiana na wizi wake wa fedha za Serikali kwa kisingizio cha ugonjwa bandia wa mkewe.

Waziri huyo mwizi (labda tumwite ‘mwiziri'), badala ya kwenda jela, akawa anahaha mitaani na kuapa kwamba ama zake ama za mwandishi huyu. Waziri huyo akafunga safari hadi mikoa ya magharibi, na hata katika nchi jirani, kutafuta ‘ukweli' kuhusu mwandishi huyu, na kufikia hitimisho kwamba mwandishi huyu si raia wa nchi hii, wakati wote akiungwa mkono na mkuu wa nchi wa wakati huo. Wote wanajua kilichofuatia.

Mwandishi huyu, tofauti na Bashe, hakuwa anatafuta cheo wala nafasi ya uongozi; alikwisha kuchoshwa na unafiki uliokuwa umemzunguka kila mahali, na hususan wanasiasa uchwara wanaoingia madarakani kwa ahadi ambazo, ukiwachunguza kwa undani, si kwamba wanashindwa kuzitekeleza, bali hawajawahi kuwa na nia yo yote ya kuzitekeleza.

Tusichanganye mambo, hata kama utamaduni wetu ni wa ‘chakachua.' "Usomali" wa Bashe hauna uhusiano na uamuzi wa NEC (mbona chama-tawala kinao ‘Wasomali' wengi tu, tena waandamizi na hawazungumzwi?) na wala hauna uhusiano wo wote na tatizo lililompata mwandishi huyu. Na wala maamuzi mengine yaliyochukuliwa na NEC kwa visingizio (sababu zina sehemu zake) kadhaa hayafanani na maamuzi mengine ambayo hayafanani na visingizio hivyo:

Watoa rushwa na wanunua kura wamo ‘kibao' ndani ya orodha iliyopitishwa na chama-tawala, na pia majangili maarufu na maharamia mashuhuri wa kila aina. Wakabila, wadini, wabaguzi wa rangi, washirikina, walaghai, wauaji wa albino, wauza unga.. kama kuna dhambi isiyowakilishwa ndani ya orodha ya wagombea waliopitishwa juzi na NEC, dhambi hiyo haijateremshwa duniani.

Wakubwa, kwa kuamini kwamba wananchi wanaowatawala ni wajinga, wanaendelea na kauli zao nyepesi, ambazo zinaashiria fikra nyepesi.

hs3.gif
 
Back
Top Bottom