Hats off to Jenerali Twaha Omar Ulimwengu

hivi inashindikana nini kwa jenerali kutaja hata hospitali aliyozaliwa...na mlolongo wa maisha yake.nimesoma makala yake vizuri lakini kuna vitu nadhani anaruka,kuna mchangiaji mmoja hapo juu ameeleza siku che nkapa anatangaza nia walikuwa pamoja. Nami nakumbuka sana
lakini kilichofuata ni chinga kuwatema kutoka katika ufalme wake na ndipo jenerali alipoaanza kutumia kalamu kuusulubu uongozi wake!! malalamiko hayo pia niliwahi kumsikia mwandishi mwingine mwandamizi(mzee wa je tutafika?)akisema wao walimsaidia chinga kujenga mikakati na walitegemea wangekuwa Think Tank yake lakini akawayeyusha..Lazima kiongozi yeyote angependa kuhoji uhalali wa jenerali kuendelea kuusulubu uongozi wake!!!na sio hivyo tu kuna pub wakati huo ikiitwa kwa mama lily pale kijitonyama nilikuwepo wakati jenerali akibishana na Rugumamyeto kama sikosei by then akiwa katibu mkuu karibu na ikulu hadi wakatiana adabu...yote hayo pamoja ukichanganya na hilo alilosema mwenyewe la kitine hata ungekuwa wewe.......ngoma INOGILE!!!!!!! VIONGOZI WA NCHI SIO MALAIKA.
 
Nami nilikuwepo pale Kwa Mama Lili (amabaye ni mke wa rafiki yangu marehemu Joshua) siku hiyo.Ukweli ni kuwa Ruguhyamheto alizidiwa kihoja na Jenerali na akaamua kumuita Jenerali kuwa ni Mtusi na serikali itamshughulikia...naye Jenerali akamwambia (over a drink ofcourse) kama mimi ni Mtusi basi wewe ni Mhutu kitu ambacho kilimuuma Ruguhyamheto na kuja juu na kutaka kupigana...na kweli walimshughulikia yeye Jenerali,Balozi Bandora(Nigeria) na Mama Maudline Castico kuwa sio Raia.
 
Naifahamu vizuri hadithi ya kumtoa nishai Twaha...Mwenyewe ni mchunguliaji mzuri humu ipo siku atayaweka sawa mambo yote hadharani.Lakini always mabaya hulipwa hapa hapa duniani.Huyo Hans nae wajanja walimtoa Nishai walipomripoti mkewe kwa matumizi ya Uongo ya pesa za walalahoi.Kesi hiyo ilimuumbua Kitine.Anayejua vizuri mchezo huo ni Membe kwani wakati huo alikuwa special assigned officer ktk Embassy yetu Toronto.Hawa watu serikali huumizana wenyewe kwa wenyewe!

Alilianzisha Membe kule Canada...apparently Mmembe nae aliwahi ku-cross roads ana Kitine huko nyuma na akawa dealt with severely....Membe akiwa a junior UwT na Hassy akiwa ndio top
 
Wakuu,
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa makala za 'Rai ya Jenerali' toka zilipoanza nadhani 1994(Gazeti la Rai wakati huo)...zinanivutia lakini hizi za toleo lililopita(Na.146 Raia Mwema) na wiki hii (Na.147 Raia Mwema)...zimenigusa sana hasa hii ya leo....huyu bwana alikaa kimya sana kuhusu sakata lake la uraia lililoibuliwa na serekali ya Mkapa....lakini leo kwa upeo wa hali ya juu na kwa utaalamu mkubwa wa kiuandishi amenifanya nimuelewe vizuri sana....nimeshindwa kuiweka makala hii hapa....lakini amemmaliza Chiligati kwa hoja ya kumhusisha yeye Jenerali na suala la Bashe.....laiti waandishi wetu wengine wangeandika kama huyu bwana basi mabanzi ya mbao katika macho yetu,kutu katika bongo zetu na nta katika masikio yetu vingetokomea kabisa.

Thank you Jenerali if you are in the forum!!!

Huyu ni tapeli tu mojawapo labda kwa wale ambao hawamfahamu, anaganga njaa tu. Hili ni tatizo kubwa sana Tanzania hatufahamu ni nani hasa wenye uchungu na hii nchi ambao kwa moyo na dhati wangeweza kusukuma gurudumu la maendeleo. Hence tunapata uchwara kama huu ambao unaangalia mitumbo yao zaidi.
 
Mhh...labda utufafanulie kidogo anaganga njaa vipi na amemtapeli nani na kama ameshawahi kufikishwa mahakamanai kwa hilo pia...mimi ningeshukuru pia kama ukatusaidia hilo tatizo kubwa sana Tanzania kutowajua wenye uchungu...tutajie ni nani hao maana wengine hatutojua
 
Haya maswala ya uraia Tanzania Yanatokana na roho za kimaskini... Na siku zote mimi napinga maneno ya watu wanaosema ati maskini ni wastaarabu na wenye huruma sana kwa sababu hawana nguvu ya fedha. Lakini ukweli ni kwamba ukitaka kuwapima, weka sinia la ubwabwa utawaona wanavyotiana makucha ya macho na hata kutoana roho kwa sababu ya pande moja la nyama. Na mara zote huwa hakuna atakaye shiba kati yao isipokuwa kujiongezea maradhi kwani katikati hupindua sinia na wali wote huishia mchangani..

Hizi sheria zetu za kuwaita wazawa sio Watanzania hadi wazazi wao hasa baba awe Mtanzania inatokana na mila inayokumbatia Ukabila zaidi ya Uraia..Ni vichekesho sana kuona ati baba Mtanzania aliyekwenda kusoma Urusi na kuzaa mtoto ambaye hajawahi fika Tanzania anapata uraia wa baba kuliko Mtoto aliyezaliwa Tanzania na kukulia Tanzania kwa sababu tu baba yake sio Mtanzania. Kwa maana hii wapo watoto nje waliozaliwa wana haki ya Utanzania ingawa hawajawahi kukanyaga nchini kuliko watoto waliozaliwa nchini na wanaishi nchini kwa vibali.

Kama kweli sheria yetu ndio inasema hivi basi tumechemsha sana kwa sababu Tanzania ina mchanganyiko wa makabila sijapata kuona na kama tukianza kuwachambua kila mmoja wetu nina hakika tutafukuza wengi sana. Na hata madai ya kwamba wale wote waliokuwepo nchini kabla ya Uhuru wamepata uraia moja kwa moja ni uongo tu kwa sababu wakoloni wengi tu walikuwepo nchini (wawekezaji) wakati wa Uhuru wetu na bado waliondoka ama kuondolewa wakihesabiwa kama ni raia wa nje. Hivyo historia ya Utanzania haina kipimo isipokuwa kwa jinsi viongozi walioko madarakani wanavyojisikia.

Toka mwaka juzi rais JK akitembelea nchi za nje, aliwaomba kwa msisitizo Watanzania warudi nyumbani kuwekeza...Ebu nirudie tena WATANZANIA warudi NYUMBANI kuwekeza... hii inaingia akilini kweli.

Haya maajabu ya Mussa Watanzania hao hao wakiingia nchini hupewa visa ya miezi MITATU tu kukaa nchini hata kama wamekuja kuwekeza laa sivyo wachukue kibali cha kuhamia kwa gharama isiyopungua dollar za Kimarekani 1,600. Na hata kama wamekuja wekeza kwa mtaji unazidi kiwango cha dollar 300,000 bado watu hao walishindwa kukamilisha taratibu za usajili ktk miezi hiyo mitatu hivyo kuwalazimu kutoka nje ya nchi na kuomba visa tena. Ni adhabu kubwa kuwekeza Tanzania kwani hakuna matayarisho ya aina yoyote ile kwa wawekezaji kama huna rangi na lafidhi ya mkoloni mtawala wetu.

Sasa wakati nchi yetu inahitaji vijana wenye uwezo mkubwa ktk maswala yote ya ujenzi wa nchi yetu na hakika badala ya serikali kutumia mabillioni kwenda kuwasomesha nje hawa vijana wamechukua jukumu lao wenyewe na familia zao kutafuta elimu nje, leo wanaitwa ni WAKIMBIZI.. ati wameikimbia nchi hali vijana hao wasingeweza kupata elimu hiyo pasipo kuchukua hatua walizochukua. Na kibaya zaidi leo tunaambiwa ati kina Rostam ndio Watanzania kuliko hawa vijana waliokwenda nje kutafuta elimu na kadhalika.

Kwa sababu ya mfumo huu mbovu vijana wengi wameingia shule feki ili kupata elimu haraka na kurudi nyumbani ili mradi wasipoteze Uraia wao. Ni vigumu sana kwa kijana Mtanzania kuweza kujisomesha UK, US au Canada akiwa raia wa nje kwa muda wa miaka mitano au zaidi... Ni karibu na haiwezekani ama ndio kujiunga na vyuo vya mitaani na kupata cheti kisichojulikana kimataifa.

Na kwa bahati mbaya wale walioweza kusoma kweli hawana sababu ya kurudi nchini ikiwa kweli wanakuwa treated kama foreigners hali baba zao ni Tanzania Citizen. sasa ebu nyie nambieni huyo Bashe sio Mtanzania kwa sababu baba yake hakuwahi kuukana Usomali, iweje Mzawa mwingine anayeishi nchi za nje asiwe raia wa Tanzania ikiwa baba yake hakuwahi kuukana Utanzania!

Jamani nachoweza kusema tu ni kwamba kwa kila mtu aliyefikisha umri zaidi ya miaka 18 huyu ni mtu mzima na ana uweo wa kuchagua Uraia kwa utashii wake ikiwa ktk nafasi tata kama ya Bashe. Iwe hata hatukubali Uraia wa nchi mbili lakini tuwe na maamuzi ya kisheria yanayochuja rabsha kama hizi za kutazama Upande mmoja tu wa sheria kama kisu butu..
 
Jenerali Ulimwengu kama nimemuelewa vizuri kwanza hakutaka kuelezea umma kilichotokea huko nyuma,ila imemlazimu atoe ufafanuzi wa vipengele fulani vilivyofananishwa na swala lake enzi za Raisi Mkapa na Bw Chilligati wakati akitoa tamko la CCM kuhusu Bashe.Alichosema Ulimwengu ni kuwa swala la Bashe na Ulimwengu ni tofauti,si kama alivyodai Chilligati.Chilligati alitoa majibu yasio sahihi,kutaka kuhadaa umma,kwa majibu butu.
 
Ukisoma kwa undani hii makala ni Jenerali yeye anataka kumlipua KITINE period, kwani hajaongelea kabisa mapungufu ya sheria kama yapo. Kingine anachoongelea ni kuwa mbona wengine hawachunguzwi uraia wao? Sasa inanipa shida hapa tunaanza kusheherekea kuwa kintine alikuwa ndo amemmaliza, kwa nini tusiombe waandishi wengine wamfate KITINE wamuulize ili tupate upande mwingine. N ni kwa nini Twaha hataki kueleza kwa undani, wakati ule si aliambiwa sheria huwa hivi, kama kuna mahali unaona umeonewa basi nenda mahakamani, sasa kwa nini alivyata? Hili swala liko open saana kwa nchi kama yetu ambayo watu hawako registered ni rahisi saana kuwa mamluki, lakini inapofikia unaingia kwenye nafasi nyeti na watu wakaja kuhoji uraia wako ni lazima watu wafuatilie, na hii ndo imemkuta Bashe.

Shaka yangu ni, je ndani ya chama hawana neno kuwa na viongozi mchanganyiko wa raia na wasio raia? Au katiba yao ni silence on issues za uraia?
 
Toka mwaka juzi rais JK akitembelea nchi za nje, aliwaomba kwa msisitizo Watanzania warudi nyumbani kuwekeza...Ebu nirudie tena WATANZANIA warudi NYUMBANI kuwekeza... hii inaingia akilini kweli.
Lini na wapi Kikwete akitembelea nchi za nje alisema Watanzania rudini nyumbani?

....Alichosema Ulimwengu ni kuwa swala la Bashe na Ulimwengu ni tofauti,si kama alivyodai Chilligati.
Ulimwengu, kama Bashe, hakuwa raia, aliishi kimazoea.
 
Bravo Jenerali Ulimwengu!! You dare speak openly!!! Ila I am afraid nchi yetu haina uhuru wa habari, na sitashangaa wakikuandikia barua za kukuonya eti usiandike masuala ya kuwachanganya wananchi na kuleta vurugu!! Nchi kama Rwanda inatamani sana iwapate watanzania waende kule kufanya kazi hata zile sehemu nyeti, na Kagame alishatangaza hilo. Alisema atafurahia sana hii Federation maana atafaidi sana vichwa vya kutoka nchi nyinginezo!! Vijembe vijembe ndani ya chama. Je tutafika!!

Usidanganyike, wewe Rwanda huijui na hujafanya kazi kule! Hayo mambo ya kuongea ni ya kuongea tu. Kwani hizo kazi anazokaribisha watu kufanya ziko wapi? Hao majirani wanatoa concession which is a non concession, ili muuvae mkenge ili wote wahamie huku. Na kuhusu Marekani, hivyo vichwa wana uwezo wa kuvilipa, kukaribishana kwenye umaskini ni kuongeza migogoro mingine tu hasa ya ardhi. CCM ni mafia, hayo ya kuzushia watu nayategemea na si mageni, iwapo wafanya biashara wanadaiwa kodi wakikorofishana nao, unategemea nini? Yaani Serikali wanayoongoza ina uwezo wa kukusanya kodi, na sheria wanazijua ila kama uko upande wao hulipi au unalipa kidogo! Wanadumaza nchi na kuongeza umaskini huku wakijua, hawana maana kabisa. Na kuna makada wao, viongozi wahindi na waarabu (ambao rangi yao ni kiashiria cha utata wa uraia) wanaopora kila siku, mbona hawajafuatilia urai wao wakati wengi si raia! Kwani Tanzania haiendelei kwa sababu hakuna watu wa kutoka nje kuja kufanya kazi?
 
kitine alikuwa mwizi sana si ndo huyu alizamisha gari kupoteza ushahidi?

ccm ni genge la wezi.
 
Ulimwengu, kama Bashe, hakuwa raia, aliishi kimazoea.
[/QUOTE]

Wakati wa uhuru Jenerali alikuwepo na hivyo alipaswa kuwa raia by default...
 
Hapana, Katiba haisemi hivyo.

Ulimwengu, kama Bashe, hakuwa raia. Aliishi kimazoea.
 
Huyu ni tapeli tu mojawapo labda kwa wale ambao hawamfahamu, anaganga njaa tu. Hili ni tatizo kubwa sana Tanzania hatufahamu ni nani hasa wenye uchungu na hii nchi ambao kwa moyo na dhati wangeweza kusukuma gurudumu la maendeleo. Hence tunapata uchwara kama huu ambao unaangalia mitumbo yao zaidi.

Hii bila shaka ni kauli ya FISADI Nyangumi
 
Mhh...labda utufafanulie kidogo anaganga njaa vipi na amemtapeli nani na kama ameshawahi kufikishwa mahakamanai kwa hilo pia...mimi ningeshukuru pia kama ukatusaidia hilo tatizo kubwa sana Tanzania kutowajua wenye uchungu...tutajie ni nani hao maana wengine hatutojua

Hivi unafahamu maana ya kuganga njaa? Hebu tueleze matapeli kama RA, BWM, JK, Chenge , Mramba etc wote wamefikishwa mahakamani? kufikishwa mahakamani ndio proof? Mkuu I know this guy ni tapeli wa kutupwa na mjanja mnjanja sana kama utakumbuka wale aliokuwa nashirikiana nao kama Salva, marehemu Rutayisingwa etc. Kama ungekuwa na akili timamu usingeropoka.

Hii bila shaka ni kauli ya FISADI Nyangumi

Khe khe khe mkuu hapa huwa hatumung'unyi maneno ni nondo full time. Sina sababu ya kumsifia kwa sababu anaandika mambo flani ya kweli kuhusu mafisadi na kutaka kuonekana moja katika wapambanaji, hapo ndipo unapotakiwa kuamua kusuka ama kunyoa. Ni sawa na RA aje hapa na kutueleza utumbo wa Chenge, EL au JK unafikiri nitamuamini? Au Malaria Sugu na hadithi zake za abunuwasi kutoka Magogoni.
 
Ulimwengu, kama Bashe, hakuwa raia, aliishi kimazoea.

Wakati wa uhuru Jenerali alikuwepo na hivyo alipaswa kuwa raia by default...

Hivi unaweza kuleta huo ushahidi au unaropokaropoka tu?

Hapana, Katiba haisemi hivyo.

Ulimwengu, kama Bashe, hakuwa raia. Aliishi kimazoea.

Tatizo la wengi hawataki kuona sheria zinafuatwa watakwambia hadithi za Marekani na Canada wakati hizo nchi zinafuata sheria zao na huwezi kuwachezea dana dana ambazo wanatufanyia hawa wakimbizi uchwara.
 
Hivi unafahamu maana ya kuganga njaa? Hebu tueleze matapeli kama RA, BWM, JK, Chenge , Mramba etc wote wamefikishwa mahakamani? kufikishwa mahakamani ndio proof? Mkuu I know this guy ni tapeli wa kutupwa na mjanja mnjanja sana kama utakumbuka wale aliokuwa nashirikiana nao kama Salva, marehemu Rutayisingwa etc. Kama ungekuwa na akili timamu usingeropoka.

Khe khe khe mkuu hapa huwa hatumung'unyi maneno ni nondo full time. Sina sababu ya kumsifia kwa sababu anaandika mambo flani ya kweli kuhusu mafisadi na kutaka kuonekana moja katika wapambanaji, hapo ndipo unapotakiwa kuamua kusuka ama kunyoa. Ni sawa na RA aje hapa na kutueleza utumbo wa Chenge, EL au JK unafikiri nitamuamini? Au Malaria Sugu na hadithi zake za abunuwasi kutoka Magogoni.

Mbona uanaleta kashfa ndugu....wewe hunijui sasa unawezaje kusema sina akili timamu...nmekuomba utueleze huyu Jenerali ni tapeli kivipi wewe unakuwa mbogo...sikatai yeye ni binadamu na labda alipata kukukosea huko nyuma lakini huwezi ukam-generalized kwa wengine tusiomjua hivyo umjuavyo....kwa busara tu tueleze hafai vipi na tukiridhika basi nasi tutamuita tapeli

Nijuavyo mtu anaeganga njaa ni yule ambae daima kwake ni kukamilisha mlo kwa juhudi za wengine .... nimjuavyo Ulimwengu sidhani kama yuko hivyo...yes Mramba yuko mahakamani...Mkapa ana kinga hawezi kupoelekwa mahakamani....Chenge yuko mahakamani....RA atafika tu usijali....ila nimekwambaia pale awali kama Jenerali ni tapeli kama unavyodai je amewahi kushatakiwa? kama ni hivo tueleze hapa...JF THE HOME OF GREAT THINKERS
 
Back
Top Bottom