Public Enemy
JF-Expert Member
- Aug 18, 2011
- 2,905
- 3,255
Nilianza na PHILLIPS moja kubwa sana silikumbuki aina gani hii ilikua ya nyumbani hadi mwaka 2007 nilipobahatika kuwa na simu binafsi ambayyo nilipewa na dada yangu nakumbuka ilikua SIEMENS ina kimtambo kama kieria hivi unakivuta juu, hii ilikua swafi sana inatuma sms na ilikua na infrared pia bahati mbaya ikadondokea kwenye maji wakati huo nipo Mbeya nikampelekea Fundi mmoja maarufu maeneo ya Soweto barabara ya moon dust akijiita Shololo.com haikupona kamwe. Baada ya hapo nikahamia kwenye kinokia cha kufunua hiki hakikudumu nikakilalia kikavunjika katikati spea kupata ikashindikana niliambiwa mkanda umekuwaje sijui sikumbuki. Nikapata kinokia kingine jeneza kilikua, toka hapo nikabadili badili nokia baadhi sikumbuki sana mpaka mwaka 2010 nikafanikiwa kununua kwa mtu G-TIDE ya ku slide aiseh hapa nilitamba sana kwa maana ilikua na radio,memory card na bluetooth pamoja na GPRS isivyo bahati haikudumu sana kama ada nikaiharibu mkanda nililalia pia usiku haikupona pia. Kutoka hapo nikarudi kwenye nokia kitochi nikacheza sana game la nyoka mpaka 2011-2012 nadhani nikafanikiwa kupata Motorola L6 kama sikosei ya kufunua zile zilionekana sana kwenye Prison break season za mwanzo, hii MOTO ilikua kila kitu kwa wakati huo kwa maana ilikua na Bluetooth, GPRS naingia online waptrick.com na site kama myspace.com kusaka wachumba wazungu fb nakadhalika nakadhalika. Hii Moto ilikua na uwezo mkubwa kiasi kwamba nilikua naweza ku connect na Dell langu latitude D620 nikapata internet safi usiku nikakesha. Kama ada nayo usiku nikailalia ikakatika kati, ndugu yangu mmoja akaja kuniazima Samsung AT&T hii ilikua unai slide juu ndio unaona buttons zake na hapo juu ilikua kioo tupu nikaiharibu kwa kuidondoshea kwenye maji ikaisha habari yake na kurudi kwenye Nokia kitochi. Mwaka 2012-2013 nikajichanga nikanunua Nokia X2-02 Double line MPYA Dukani Morogoro hii ilikua full boxed. Hii ilinifanya nikeshe Fb na site zingine kwa maana ilikua na uwezo mkubwa zaidi ya Simu zote nilizowahi kutumia mpaka wakati huo baadaye nikaja kumuuzia Msukuma mmoja mara mbili ya bei niliyonunulia na kuhamia kwenye Ulimwengu wa Tecno kwa maana wakati huo Whatsapp imeshika kasi nikaona nisipitwe nayo kama BBM ya Blackberry ilivyonipita. Tecno nimetumia karibia herufi zote za Alphabeti kuanzia sijui N mara P zilikua nyingi kwakweli. Nimedumu kwenye matoleo mbalimbali ya TECNO mpaka mwaka 2015 nilipobahatika kununua simu ya gharama kubwa Samsung Galaxy Note 3. Hii niliuziwa na jamaa mmoja alitoka China nikampa 490k iliniuma mno lakini ndio nikawa nimenunua. Huu Mtambo ulikua 2 ama 3gb kwa 32GB na ulikua unapiga kazi sana hadi mwaka 2016 Nilipobahatika kumuuzia Ndugu yangu mmoja kwa 550k ambapo nilipiga faida tena bahati ilikua upande wangu. Nikanunua OPPO moja 3/32GB haikudumu sana nikauza pia. Kutoka hapo nikahamia kwa INFINIX NOTE 2,3 na X5 kama sikosei hadi mwaka 2018 kama sio 2019 pale nilipohamia kwenye XIAOMI REDMI NOTE 5 PRO, ambayo sikudumu nayo sana nikauza nika advance kwenda XIAOMI REDMI NOTE 8 nayo nikakaa nayo kwa muda hadi mwaka jana msimu ule Corona imeshika kasi April nikauza nikarudi Kwenye TECNO What a Joke! Tecno ilinishinda ilikua 1/16GB nikauza nikanunua SAMSUNG GT E1207Y duos 55K,sifa kuu ni kina redio na betri yake inakaa sana sababu hakuna matumizi ya mara kwa mara ambacho niko nacho mpaka sasa. Nikitoka hapa kama nitatoka by the way nitaenda kwa ndugu zangu XIAOMI aina gani itategemea na ipi kwa wakati huo itakutana na bajeti yangu.